Skip to main content

FATMA MGWALI: ULEMAVU HAIKUA KIKWAZO KUISAIDIA JAMII YAKE

 



NA TATU MAKAME, ZANZIBAR@@@@


LICHA ya ulemavu alionao hakuwahi kukata tamaa katika kupambania maisha yake na jamii inayomzunguuka katika kupata huduma za jamii ikiwemo maji safi na salama katika jamii yake.

Unapomuona hali yake na ushujaa wake ni tofauti na uwezo wake kutokana na tatizo la uoni hafifu wa macho aliokuwa nao lakini ana ndoto za kufanikisha yale aliyojipangia katika maisha yake hasa kuwapatia wananchi wa eneo lake huduma ya maji safi na salama ili waondokane na adha ya maji.

Unapomuona huwezi amini kama anauwezo na ujasiri wa kusimama akapigania haki yake licha ya umaskini wake pamoja na kubezwa na kudharauliwa kwa sababu ya ulemavu wake.

Huyo si mwengine ni Fatma Mgwali Khamis mkaazi wa kijiji cha Fukuchuchani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Fatma alizaliwa mnamo mwaka 1977 katika kijiji cha Fukuchani ni mtoto wa tano katika watoto wanane wa Mama mzazi wa Fatma aliyefahamika kwa jina la Tatu Haji Khamis ambae alijaaliwa kupata watoto watatu wanaume na watoto watato wanawake.

Fatma alipata elimu ya msingi katika skuli ya uhuru mchanganyikao iliyopo Tanga Korogwe mwaka 1981 hadi 1991 alipoacha kusoma kwa sababu ya kutoondelezwa kusoma kwa sababu ya umaskini kutoka kwa wazazi wake na ulemavu alionao.

Ndoto za Fatma zilimfanya amalizie kidato cha pili licha ya kuwa na hamu ya kuendelea na masomo kito cha tatu na nne na kuendelea.

Fatma anaeleza kuwa mwaka 1993 alifunga ndoa huku akiwa na huzuni ya kupoteza ndoto zake za kufikia maendeleo yake na kusaidia jamii ya watu wenye ulemavu.

“baada ya kuolewa ndoto zangu ziliishia njiani kuendelea na masomo licha ya kuwa na hamu ya kuendelea na masomo.

HALI YA MAISHA YA FATMA

Fatma anasema katika maisha yake ya ndoa amebahatika kupata watoto wanane ambao watano kati ya hao ni walemavu.

“mtoto wangu wa kwanza nilimzaa mwaka 1994, wa pili 1996, watatu 1996, wa nne 2003 na mwengine miaka tofauti”

“, alisema.

Anasema watoto wake wawili ambao aliwataka kwa majina ya Rehema na Abdalla walimalizia kidatu cha nne katika skuli ya Uhuru mchanganyiko iliyopo Korogwe Tanga na baadae kumalizia skuli ya Old Sekondari iliyopo Moshi Tanga ambao wote ni walemavu wa uoni.

Alisema watoto wengine ambao ni walemavu wa uoni ambao wanaendelea na masomo ni Shafii Haji Zubeir (10) anasoma darasa la sita na Zahoro Haji Zubeir (13) wa darasa la nne ambao wote wanasoma katika skuli ya Uhuru mchanganyiko Tanga.

“Alisema kuwa mtoto mwengine mlemavu ni Yussuf Khamis Bakari ambae anaishi na mlezi wake katika kijiji cha Uroa Mkoa wa Kusini Unguja ambae hakuendelea na masomo kutokana na ulemavu wake.

Alisema kuwa watoto wengine watatu ndio wanaosoma katika kijiji cha Fukuchani kutokana wao wako katika hali ya kawaidi kama watoto wengine.

Fatma anaeleza kuwa licha ya ulemavu alionao matarajio yake kuwaendeleza watoto wake ambao wanaendelea na masomo ili wafikie ndoto zao za baadae.

MAISHA YA KUSOMA KWAKE NA KUSOMESHA

Fatma anaeleza kuwa kutokana na ulemavu wake alisomeshwa kwa shida kwa kuwa wazazi wake hawana uwezo.

“Mamaangu sasa keshakuwa mtu mzima na baba tayari ametangulia mbele ya haki lakini shughuli zao ilikuwa ni ukulima na uvuvi lakini walinisomesha hadi kufikia hapa”, alisema.

Alisema hakuendelea na masomo kwa kuwa uwezo wa wazazi mdogo.

Alisema kuwa kwa upande wake anasomesha kwa kutegemea kufanya kazi za ujasriamali kwa kuuza mifugo ya kuku kwa kuwa ni mjasriamali.

Alisema licha ya kupeleka barua ya kuomba msaada ili kusaidiwa kusomesha watoto wake katika maeneo tofauti lakini wengi wao hushindwa kumsaidia na kubakia kupambana na hali yake ya maisha.

SAFARI YA UJASRIAMALI.

Fatma alisema aliingia kwenye kazi ya ujasriamali kwa kufuga kuku mnamo mwaka 2010 ili kujisaidia katika maisha yake na familia yake.

Alisema alianza na mtaji wa 600,000 kwa kufuga kuku 200 kwa hatua ya awali ambao walimsaidia kuendeleza maisha yake.

Hata hivyo alisema kazi hiyo imemsaidia katika kuwasomesha watoto wake hadi leo wanaendelea na masomo.

“Baada ya kuingia kwenye ujasriamali nilipata kuendeleza maisha yangu kwa kupata kujisaida mimi na familia yangu licha ya changamoto niliyopata ya kukosa eneo sahihi la kufanyia shughuli zangu za ufugaji”, alisema.

Hata hivyo anasema kwa sasa tayari amejenga banda jengine ambalo baadae ataendeleza kazi yake kuendesha maisha yake na familia.

NYADHIFA ALIZOSHIKA

Fatma licha ya kuwa na ulemavu wa uoni bado ni Katibu wa Jumuiya ya wasioona wilaya ya Kaskazini ‘A’ nafasi aliyoshikilia tangu mnamo 2005 hadi sasa.

Kuwa diwani mwanamke wa kwanza Wilaya ya Kaskazini ‘A’ baada ya kuteuliwa kupitia jumuiya ya wanawake Tanzania (UWT) Wilaya hiyo ili kuwakilisha nafasi ya watu wenye ulemavu kwa uchaguzi wa mwaka 2000.

KWA NINI FATMA AWE KTIBU WA JUMUIYA YA WASOOONA

Fatma anasema alipatiwa elimu ya kushika nafasi ya uongozi na jumuiya ya wasioona Zanzibar zanab pamoja na Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Tanzania Tamwa ZNZ na kuwania nafasi hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa 2020.

SABABU ZA KUKOSA NAFASI YA UDIWANI 2025

Fatma anasema aliingia kwenye kinyang’anyiko mnamo 2025 lakini alikosa nafasi kutokana na kutotambulika kwa nafasi ya wanawake kwenye nafasi za uongozi kupitia udiwani.

“Mimi naamini nilishinda kwani nilipata kura 275 lakini sikuzingatiwa hali yangu ya ulemavu kwa kuwa ni mlemavu”, alisema.

Alisema alisikitishwa na kutenguliwa nafasi kwenye kinyang’anyiro na kupewa mtu mwengine licha ya kuonyesha ujasiri wake katika kupambania nafasi hiyo.

“Kwa kuwa waliniona mlemavu kura zangu walimpa mtu mwengine kushika nafasi na kusema sisi watu wenye ulemavu hakuna sheria wala katiba inayosema kuwa kuna nafasi za watu wenye ulemavu”, alisema.

KAZI ALIZOFANYA AKIWA DIWANI

Kuchimba kisima katika kijiji cha Kigongoni shehia ya ya Fukuchani na kuwafikishia huduma hiyo watu zaidi ya 500 wa shehia hiyo.

Anasema lengo la kuchimba kisima hicho wakati alipokuwa diwani kuona wananchi wa kijiji hicho wanafaidika na huduma ya maji safi na salama kutokana na kutumia maji ya kisima cha kuvuta kwa Kamba kwa miaka kadhaa.

CHANGAMOTO

Fatma anasema changamoto kubwa mtaji mdogo alioanzia biashara na kuomba msaada kwa watu wenye uwezo aendeleze mtaji wake.

MAFANIKIO

Fatma anasema kuwa amefanikiwa kusambaza maji kwa wananchi zaidi ya 1500 wa kijiji cha Fukuchani na kuhamasisha utafutaji wa waji katika eneo hilo.

Kupata uzoefu wa masuala ya wanawake wenye ulemavu na makundi mengine pamoja na kushirikiana na viongozi wengine katika kutatua changamoto za watu wenye ulemavu na jamii.

MASHIRIKIANO ALIYOPATA KWA VIONGOZI WENGINE.

Kushirikiana kufuatilia huduma za kijamii licha ya kuwa na ulemavu wa uoni pamoja na viongozi wa jimbo la Nungwi.

KAULI YA MRATIBU WA WASIOONA ZANZIBAR

Mratibu wa jumuiya ya wasioona Zanzibar Zanzb Adil Mohamed Ali alisema bado kuna mtazamo finyu kwa jamii kuwaona watu wasioona hawawezi kuwa viongozi ispokuwa kwa nafasi maalum tu kama Ubunge na uwakilishi na sio udiwani.

Alisema bado Zanab inawapatia elimu ya kuwataka wasioona hasa wanawake kuingia kwenye nafasi za uongozi.

TAKWIMU ZA SENSA

Kwa mujibu wa sensa ya watu na makaazi ya 2022 inaeleza kuwa kijiji cha Fukuchani kina watu 2360 wanaume 1169 na wanawake 1191 huku kijiji cha kigongoni kikiwa na watu 1634 wanawake 792 wanaume 842

Hata hivyo Fatma alisema vijiji hivyo vinakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa muda mrefu na kueleza kuwa katika shehia hiyo ya Fuchani zaidi ya watu 500 wanakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Aidha alisema jitihada za kushirikiana na viongozi wa majimbo kutatua tatizo hilo zimezaa matunda kwa kuwa watu wa vijiji hivyo hivi sasa vinapata maji.

“Zaidi ya watu 2000 wanapata huduma ya maji safi na salama kupitia kisima kilichochimbwa kwa mashirikiano na viongozi wa jimbo Akiwemo Fatma Ngwali ambae kwa sasa anahitaji zaidi ya milioni 2,000,000 kufatuta vifaa vya kusambazia maji ili kisima hicho kitoe huduma stahiki ya maji kwa wananchi wa kigongoni”, alisema.

Kazi nyengine kusikiliza changamoto za watu wenye ulemavu pamoja na kutoa elimu kwa jamii inayomzunguuka ya kuwataka wananchi kuacha kuwafungia ndani watoto wenye ulemavu.

KAULI YA CHAMA CHA WAANDISH WA HABARI TAMWA ZANZIBAR

Mkufunzi kutoka Chuo kikuu cha Zanzibar SUZA Imane Duwe anasema licha ya elimu inayotolewa na taasisi mbalimbali bado mfume dume unawakandamiza wanawake.

 Ofisa programa na mawasiliano kutoka Chama cha waandishi wa habari Tamwa Zanzibar Nairat Ali Haji alisema mradi wa kuimarisha uongozi wa wanawake SWIL kupitia Tamwa ZNZ una lengo la kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusiana na masuali ya wanawake na uongozi, haki za kidemokrasia, na uandishi wa habari za takwimu ili kuandika habari zinazohusiana na uongozi kwa wanawake.

Alisema habari hizo pia zitaangalia wanawake jinsi walivyopiga hatua za maendeleo kupitia nafasi za uongozi na kuachana na mfumo dume.

HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU

Takwimu zinaonyesha kuwa wanawake waliopo katika nafasi mbalimbali za uongozi Zanziba ni asilimia 38 pekee kwa mujibu wa sensa ya watu na makaazi ya mwaka 2022 wanawake ni zaidi ya asilimi 51 ya wakazi wa Zanzibar.

SERA NA SHERIA YA WATU WENYE ULEMAVU

Kwa Zanzibar haki za watu wenye ulemavu zinalindwa kwa mujibu wa sheria namba 8 ya 2022 ambayo inalenga kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata fursa sawa katika nyanja mbalimbali ikiwemo ushiriki katika uongozi na maamuzi ya umma.

Hata hivyo licha ya kuwepo kwa sheria hiyo lakini hakuna nafasi maalum za udiwani zilizotengwa moja kwa moja kwa watu wenye ulemavu.

Usawa wa asilimia 50 kwa 50 mbali na kuwajengea uwezo wanawake pia unatekeleza malengo ya mikataba na ahadi mbalimbali za kimataifa ambazo Tanzania na Zanzibar zimeridhia kuhusu usawa wa jinsia.

Miongoni mwa nyaraka hizo ni itifaki ya Maputo ya mwaka 2003 na ajenda ya Afrika tunayoitaka 2063, ambayo zinasisitiza umuhimu wa wanawake kushiriki kwa usawa na wanaume katika mifumo ya uongozi na kufanya maamui.

Nyaraka hizo zinataka nchi wanachama kuhakikisha wanawake waanze na wanaume wanawakilishwa kwa uwiano katika vyombo vya maamuzi ili kuimarisha demokrasia na maendeleo endelevu.

IDADI YA MADIWANI WANAWAKE KWA ZANZIBAR

Jumla ya madiwani 20 waliingia katika nafasi za udiwani kupitia viti maalum wanawake vilivyoteuliwa na Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) kati ya hao 16 walitoka Chama cha Mapinduzi na wanne walitoka ACT wazalendo ingawa idadi hiyo haikuoanisha idadi ya madiwani wanawake.

HITIMISHO

Jamii ielimishe umuhimu wa viongozi wanawake katika jamii kwani wana mchango mkubwa wa kufuatilia huduma za jamii.

Watu wenye ulemavu waendelee kupatiwa elimu ya umuhimu wa kugombania nafasi za uongozi na pia waungwe mkono wakati wanapoingia kwenye kinyang’anyiro kwani na wao wananafasi sawa kama walivyo wanawake wengine.
mwishooooo

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...