Skip to main content

BIZUME: MWANAMKE ANAEPAMBANA KUFIKIA TAIFA KIUONGOZI

 


IMEANDIKWA NA ZUHURA JUMA, PEMBA 

 

BIZUME Haji Zume, mkaazi wa shehia ya Kinyasini Jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, ni miongoni mwa wanawake mashuhuri wenye nia ya kufika mbali kiuongozi.

 

Ingawa matarajio yake yeye mpaka sasa, ni kugombea nafasi za ndani ya chama tu kuanzia tawi hadi Taifa, na sio Jimboni kwa kile anachodai kwamba ni lazima kwanza ushikilie nafasi hizo ili uwe imara zaidi.

 

Atapojijenga zaidi kwa nafasi za ndani ya chama, hapo ndipo ataanza kutafuta njia ya kusonga mbele kwani, huwezi tu kufika huko ikiwa hukuanza nafasi za chini.

 

"Nataka na mimi nifikie kugombea Uwakilishi na Ubunge katika Jimbo lakini, huwezi kufika huko ikiwa bado kwenye chama hujashika nafasi yeyote," anasema Bizume.

 

Lengo la mama huyo kugombea nafasi hizo, ni kuhakikisha anajijengea uwezo zaidi wa kiuongozi, kujenga mahusiano mazuri na wanachama, pamoja na kukubalika kwenye chama chake.

 

Anasema, hiyo itampa fursa ya kusonga mbele kiuongozi kuanzia tawi hadi Taifa, na hatimae kupata nafasi ya kuwasaidia wananchi kuwatatulia changamoto zinazowakabili.

 

"Hizi hizi nafasi za kwenye chama, ukifika ngazi za juu unapata fursa ya kuingia kwenye vyombo vya maamuzi, hivyo nitawatetea wananchi, ili kuhakikisha matatizo yanaondoka katika majimbo yote kwenye mkoa wetu," anaeleza.

 

Bizume anaeleza, nafasi za Ubunge na Uwakilishi huwezi kugombea ikiwa hujaanza kwenye chama na kujulikana, ndio maana wanaanzia ngazi hadi ngazi mpaka wafikie huko na kuapa kwamba hatorudi nyuma.

 

Anasema, kwanza ni wakati wa kukichangia chama kwa kufanya shughuli za chama na kuwa mzalendo, ndipo zitakuja tu nafasi nyengine na sio kukurupuka tu.

 

"Naendelea kujiimarisha kwenye chama change, ili nipate kuwa mzuri katika kupambana na harakati za chama cha Mapinduzi, na kuna siku naamini nitafanikiwa," anafafanua Bizume.

 

Kutokana na uwanaharakati wake kwenye chama na Serikali, watu wengi kwenye jamii, husema mama huyo anaweza kusimamia na ana moyo wa kujitolea.

 



Hivyo linapotokea jambo kwenye jamii, wananchi wanapenda achukue yeye nafasi ya kuwa kiongozi kwani hata kwenye suala la michango yupo mstari wa mbele, kufuatilia na kusimamia.

 

Bizume anasema, nafasi anazokamata kwa sasa, zote ni za kinyang'anyiro cha kugombea na anafanikiwa kupata, ingawa bado ana safari ndefu ya kufika ngazi ya Taifa.

 

Alijiunga kwenye chama cha Mapinduzi CCM mwaka 1992, ingawa tangu miaka hiyo, hakuwa nyuma katika kupambana na kuwa mwanaharakati bora.

 

Baada ya kujiunga na chama, Bizume hakuridhika kukaa tu nyumbani, bali alishiriki shughuli mbalimbali za chama, hivyo ilikuwa anaposimama kiongozi kuzungumza na yeye anapata hamasa ya kuwa kiongozi.

 

"Ilikuwa nasema kwa nini na mimi nisigombee wakati naweza kuzungumza, ndipo nilipoanza kuingia kwenye mchakato na nashkuru nimeshaanza kufanikiwa katika ngazi za chini," anaeleza.

 

Bizume alianza kuwa Mjumbe wa Jumuiya ya UWT tawi la Kinyasini na mwaka 2017, aligombea na kuwa Mwenyekiti wa UWT Jimbo la Pandani mpaka 2022 alipogombea nafasi nyengine.

 

Anasema, aligombea nafasi nyingi ingawa kura hazikutosha na kubahatika kuwa Mjumbe wa Kamati Tekelezaji Tawi la Kinyasini UWT, ambapo pia ni Mjumbe wa siasa Tawi hilo.

 

"Kwa sasa ni Mjumbe wa Kamati Tekelezaji Jimbo la Gando, Mjumbe wa Kamati Tekelezaji wilaya ya Wete, lakini pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu CCM wilaya ya Wete," anaeleza.

 

"Hivyo unaona zile harakati zangu ninazopanda ngazi hadi ngazi juu ya kuimarisha masuala ya chama, naamini ndizo zitakazonifikisha ninapopataka," anasema.

 

Lakini pia mama huyo amewahi kugombea nafasi ya Wadi UWT na alipitwa kwa kura moja, ingawa hakuishia hapo aligombea nafasi nne za wajumbe wanne wa Jimbo, ingawa nako kura pia hazikutosha.

 

Bizume aligombea Baraza kuu, aligombea Kamati Kuu ingawa pia kura hazikutosha, na kusema bado hajakata tamaa kwani mwaka 2027, atagombea kuanzia Tawi mpaka Taifa ndani ya chama bila kurudi nyuma.

 

Anasema, kutokana na hali ilivyo kwenye Dunia ya sasa, utandawazi, unawaathiri sana vijana wao, hivyo atatumia fursa ya uongozi atakayoipata kuhakikisha wanakuwa na muelekeo nzuri wa maisha yao.

 



Kwa sababu kwenye chama kuna nafasi ya malezi, itikadi na uenezi, ambayo inazungumzia suala la malezi kwa watoto na wapi waelekee katika mustakbali mzuri wa malezi yao.

 

Vilevile anafafanua, kuna mambo yanayoweza kumtayarisha kijana ili aweze kujua wapi aelekee na kitu gani anatakiwa atafute kwa mustakbali bora wa maisha ya baadae.

 

"Hivyo nikifanikiwa kuwa kiongozi wa juu nitawasaidia vijana katika masuala yanayowahusu wao, watoto na wanawake, ili kuhakikisha tunakuwa na Taifa lenye wananchi wanaofuata maadili mema," anafafanua.

 

Changamoto zilizomkumba Bizume wakati wa kugombea anasema, ni pale mwanzo tu alipokuwa hajajulikana baada ya Wadi yao kuhamishwa wilaya ya Micheweni na kwenda Wete.

 

Lakini kutokana na uchangamfu wake, wanachama wameshaanza kumjua, viongozi wote wanashirikiana vizuri, hivyo anaamini atafika anapopatarajia.

 

"Pia nimepata mafanikio ya kujuana na watu mbalimbali kwani napenda sana uhamasishaji na kujitolea, naonesha uzalendo na kukipenda chama changu," anafafanua.

 

Mbali na nafasi anazoziongoza kwenye chama, Bizume pia ni Afisa Maendeleo ya jamii wilaya ya Micheweni, na amekuwa akipambana na udhalilishaji, kuhamasisha mambo ya kimaendeleo kwenye jamii, malezi bora na ushirikiano.

 

Kwa upande huo, anawasaidia wanajamii kuwapa elimu, ushauri, mapendekezo, maelekezo na wakati mwengine hata kuwapa misaada kwa mujibu wa uwezo wake.

 

Bizume ameolewa na ana watoto sita, ambapo amepata elimu ya cheti katika masuala ya Maendeleo ya vijana.

 

Mtoto wake Bizume, Fatma Omar Juma mkaazi wa Kinyasini Wete anasema, mama yake ni mwanaharakati kwa muda mrefu sasa, kwenye chama, serikali na hata kwenye jamii.

 

‘’Hapa tunapoishi likifanyika jambo yeye ndio anakuwa mstari wa mbele na wanajamii wanamuani sana, kwani anasimamia majukumu vizuri, hivyo kazi ya uongozi anaiweza,’’ anaeleza.

 

Raiye Amour Othman mkaazi wa Kinyasini Pemba ambae ni Mjumbe wa Kamati Tekelezaji wa UWT Mkoa wa Kaskazini Pemba anasema, Bizume ni mwanamke anaejali, kuthamini na wala hamdharau yeyote katika harakati zake za chama.

 

‘’Anaweza kuongoza na kushughulikia sana mambo ya uongozi kwenye chama, Serikali na jamii, na ni mwanamke anaekubali kukosolewa, hivyo yupo tayari kujifunza mambo mbalimbali,’’ anaeleza.

 

Katibu wa CCM Jimbo la Gando Panya Yahya Ali anasema, Bizume ni mchapa kazi na anaependa kujitolea popote katika kuhakikisha kazi zinaenda vizuri.

 

‘’Bizume ni kiongozi mzuri ambae sio mvivu na ni mwenye kupenda maendeleo, hivyo atakapofika mbali kiuongozi, naamini ataisaidia jamii katika kufikia maendeleo tunayoyataka katika nchi yetu,’’ anamsifia.

 

Mratibu wa Programu ya SWILL kutoka TAMWA Zanzibar Sabrina Ali Mwatanga anafafanua, wanaendelea kuelimisha na kuhamasisha uongozi kwa wanawake ili waingie kwa wingi katika vyombo vya maamuzi na kusimamia mambo yanayowahusu na kuiletea maendeleo jamii.

 

Hiyo ina lengo la kuongeza ushiriki wao katika uongozi na siasa, kuimarisha mipango ya maendeleo jumuishi na kuweka msingi imara wa maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2030.

 

‘’Itakapofika mwaka 2030 tunataka tuwaone wanawake wengi wanaingia kwenye mchakato wa uchaguzi na kufanikiwa, hii itasaidia kutetea mambo yao yanayowahusu na masuala mengine ya kijamii ,’’ anasema.

 

Mwatanga anawanasihi wanawake wote ambao wana nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, wasivunjike moyo, bali waendelee kupambana, ili kuona kwamba kunakuwa na usawa kwenye vyombo vya maamuzi.

Mkurugenzi wa Jumuiya ya Utetezi wa Mazingira na Jinsia Pemba ‘PEGAO’ Hafidh Abdi Said, anasema wanaamini kwamba lengo lao la kufikia 50 kwa 50 katika safu ya uongozi litafanikiwa, kwani elimu inayotolewa itaendelea kuwajengea ukakamavu na kujiamini. 

Serikali kwa kutambua umuhimu wa mwanamke, sera na sheria mbalimbali za Zanzibar zimeeleza kuhusu haki ya wanawake kushiriki katika demokrasia na uongozi.

Kifungu cha 21 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kimeeleza kwamba, kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu mwanamke na taifa lake.

Azimio la kimataifa juu ya haki za binadamu la mwaka 1948 ambalo ndio msingi wa haki zote za binadamu, ikiwemo haki za kiraia na kisiasa linatoa haki kwa kila mtu katika uongozi wa nchi.

                               MWISHO.

 

 

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...