Skip to main content

"JE, UNAJUA MTOTO WAKO ANAANZA KUJIFUNZA TANGU AKIWA TUMBONI?

 


   

NA SULEIMAN SAID, PEMBA

“Fikiria mtoto anapokuwa tumboni, macho yake bado yamefumba,’’inafahamika.

 

Ingawa ndani ya kichwa chake kuna mabilioni ya seli zilizo tayari kumsaidia kujifunza.

 

Cha kushangaza ni kwamba, msingi wa seli hizo, uliwekwa wiki chache, tu baada ya mama kutunga mimba.

 

Lakini cha kujiuliza je, unajua kipindi hiki ndicho kinachoweka msingi muhimu wa maendeleo yake ya baadaye?’’.

 

Mtaalamu wa eneo hilo hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani, anasema wazazi wengi huamini kuwa elimu ya mtoto huanza siku ya kwanza, anapoingia darasani, lakini ukweli wa kisayansi ni kwamba kujifunza huanza sambamba na safari ya ukuaji wa ubongo.

 

Tena inafahamika kuwa ni, wiki chache baada ya mimba kutungwa, na kadiri ujauzito unavyokuwa mtoto huanza pia kuitikia na kujifunza kutokana na mazingira yake akiwa tumboni.

 

Anasema kuanzia takribani wiki ya tatu, baada ya mimba kutungwa, ubongo wa mtoto huanza kukua kwa kasi.

Katika kipindi hiki, mabilioni ya miunganiko ya seli za ubongo, huundwa na kuweka msingi wa uwezo wa mtoto wa kufikiri, kujifunza, kuwasiliana, kutatua changamoto, kudhibiti hisia.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni na ‘WHO’ na UNICEF kuhusu malezi na makuzi ya mtoto, hasa kipindi kinachoanzia ujauzito, hadi mtoto anapofikisha miaka mitatu, takribani asilimia 80 ya ukuaji wa ubongo hutokea.

Anaeleza kuwa, hili ina maana kwamba, kila siku ya ujauzito, ni muda muafaka wa kumuandaa mtoto kwa maisha ya baadaye.



Kila familia inaweza kuchagua makuzi ya ubongo kwa mtoto wao

Anaeleza kuwa, fikiria familia mbili katika kijiji kimoja, mfano cha Mtambile Pemba au Matemwe Unguja, na hata watoto wenye vina sawa vya afaya, wanaweza kukua tofauti.

 Ndio maana katika familia ya kwanza, mama mjamzito hupata chakula chenye lishe, huhudhuria kliniki/kituo cha afya mara kwa mara, hupata muda wa kupumzika na baba au familia humtia moyo na kumsaidia kazi zake.



Katika familia ya pili, mama hubeba mizigo mizito, hukosa chakula chenye virutubisho, hahudhurii kliniki na hukabiliwa na migogoro ya kindoa na kifamilia.

Anaeleza kuwa, ingawa watoto hawa wanaweza kuzaliwa siku moja, makuzi yao ya ubongo yanaweza kuwa tofauti.

 

Kumbe hilo ni kutokana na mazingira waliyokulia kabla hata ya kuzaliwa, ambapo kitaalamy hiyo ndiyo sababu wataalamu wa maendeleo ya mtoto hutaka kuandaliwa tangu tumboni.

Lishe bora kwa mjamzito

Mtaalamuy huyo anasema, mjamzito anapopata mlo kamili, si mwili wake pekee unaonufaika, bali hata ubongo wa mtoto anayekua tumboni.

Anasema kwa bahati nzuri, Zanzibar ina vyakula vingi vinavyoweza kusaidi ukuaji wa ubongo wa mtoto, kama samaki, dagaa, mayai.

Vyakula vingine ambavyo sio adimu ni maharage, kunde, ufuta, njugu, mboga za majani, nafaka, papai, embe, ndizi, chungwa na parachichi.

Ndio maana dk. Fadhila kupitia mradi wa makuzi na malezi ya watoto amesisitiza kuwa, lishe bora haihitaji vyakula vya gharama, kama wingi wanavyofikiria.

 

Utulivu wa mjamzito na faida ya mtoto aliyetumboni  

Mama anayepitia msongo mkubwa wa mawazo, kwa muda mrefu, anaweza kupata athari zinazoweza kuathiri ukuaji wa mtoto.



Dk. Fadhila, anasema tafiti zinaonyesha kuwa mazingira salama, yenye upendo na msaada wa familia, huchangia ukuaji wa ubongo wa mtoto tangu akiwa tumboni.

Akaeleza kuwa, katika jamii mara nyingi, ujauzito huonekana kuwa jukumu la mama pekee, na kusahauliwa baba kwamba nae ana mchango sio gtu wa ukuaji, bali hata mtoto kuzaliwa hai.

 

 Hivi karibuni akizungumza kwenye moja ya mafunzo ya ukuaji wa mtoto, Afisa Ustawi wa jamii na hifadhi ya mtoto Chakechake Rashid Said Nassor, anasema baba anapomuhimiza mama kwenda kliniki, ni jambo jema.

Eneo wajibu wa baba ni kuzungumza na mtoto akiwa tumboni, kusaidia kazi za nyumbani na kuwa karibu na mama ambapo yote hayo, hujenga furaha na kuepusga msongo wa mawazo.

‘’Kwa mfano, baba anayechukua dakika chache kila jioni, kuzungumza na mke wake, kuuliza hali yake na kupanga pamoja mahitaji ya ujauzito, huchangia kujenga mazingira yenye utulivu na makuzi bora ya ubongo wa mtoto,’’anasema.

Kila ziara ya kliniki ni fursa ya kulinda afya ya mama na ukuzaji wa ubongo wa mtoto

Wapo wanaoamini kuwa, kliniki ni sehemu ya kujifungulia tu, jambo ambalo sio sahihi, ukweli ni kwamba, ni eneo la ushauri na mafunzo ya kuchochea makuzi ya ubongo wa mtoto.



Kliniki hufanya uchunguzi wa makuzi na afya ya mtoto, mama hupatiwa virutubisho muhimu, chanjo na elimu ya malezi.

Huduma hizi husaidia kugundua changamoto mapema na kulinda afya ya mama na mtoto, kwa ajili ya kupata watoto wenye afya njema.

Haya hapa mambo matano ya kukumbuka

Kwenye ukuaji wa ubongo wa mtoto, huanza kukua wiki chache baada ya mimba kutungwa, jingine ni kipindi cha ujauzito hadi miaka mitatu ni muhimu zaidi kwa ukuaji wa ubongo.

 


Jambo la tatu ni lishe bora na mahudhurio ya kliniki huchangia ukuaji mzuri wa ubongo wa mtoto, huku eneo jingine ni msaada wa baba na familia hupunguza msongo wa mawazo kwa mama na malezi bora huanza kabla mtoto hajazaliwa.

Hitimisho

Ubongo wa mtoto hauanzi kujengwa siku ya kwanza ya skuli; huanza kujengwa tangu tumboni.

Kila mlo wenye lishe, kila ziara ya kliniki, na kila neno la faraja ni uwekezaji katika kizazi kijacho.

Kuwekeza katika mama mjamzito leo ni kuweka jiwe la msingi la viongozi, walimu, na wabunifu wa kesho.               

       mwisho                                      

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...