Akizungumza mmoja kati
Maafisa kutoka Divisheni ya Maendeleo ya
Jamii ndugu Omar Haji Omar wakati walipofika kutambulisha kazi za Idara ya
Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto katika shehia, kwa Mashesha na Waratibu wa
shehia kwa Wilaya ya kati Unguja, amesema mashirikiano yao yatawezesha kutatua
changamoto kwa haraka.
Amefahamisha kwamba shughuli
zote za maendeleo au changamoto ya jamii
katika shehia zao zinapaswa kuripotiwa katika Wizara husika lakini mashirikiano
yao yatawezesha Wizara ya maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kufanya
kazi kwa ufanisi.
Amesema utaratibu huu
umekuja baada ya kuundwa kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto ikiwa miongoni mwa shughuli zake ni kutambua na kusimami shughuli zote
za maendeleo ya jamii katika shehia zao zinatambuliwa na Wizara hiyo.
Amesmea ni lazima
kuhakikisha kuwa shughuli zote zinazofanyika katika shehia zao wanaziwasilisha
kupitia katika Wilaya ili nao waweze kuziwasilisha katika Wizara husika.
Amesema wanatambua kuwa
masheha wanafanya kazi kubwa katika jamii, hivyo katika kuendeleza maendeleo
mbalimbali katika shehia zao, ni lazima kuondoa changamoto baina ya masheha na
waratibu ili wafanye kazi zao vizuri kwa
kwa kuleta ustawi mzuri kwa jamii.
Amesema lengo ni kuona maendeleo
yote yanayotaka kufanyika na yaliyofanyika yanatambuliwa na kuona kila penye
uhitaji wa huduma zinafikiwa kupitia shehia zao ili kupunguza matatizo madogo
madogo yanayojitokeza.
Kwa upande wao Masheha
wameonesha kufurahishwa kuwepo kwa utaratibu huo kwani awali haukuwepo na
kusema kuwa wamepata usaidizi mzuri juu ya utendaji wao wa kazi.
Wamesema suala la kuripotiwa masuala ya Maendeleo ya Jamii katika shehia zao haufanyiki kwani hata wao baadhi ya shughuli hawashirikishwi, hivyo utaratibu huo utawasaidia wao katika kupata taarifa sahihi za kumsaidia mhe Rais katika kuelezea masuala mbalimbali ya Maendeleo yanayofanyika katika nchi kwa ujumla.
Nao waratibu wamewaomba
Maafisa hao kuwafikishia utaratibu huo viongozi wao wa siasa wakiwemo Wabunge na
Wawakilishi kuhusu miradi yao wanayoitoa katika shehia zao kuwashirikisha na Masheha
pamoja na waratibu kwani wao ndio wahusika wakuu wa shehia.
Comments
Post a Comment