NA ASHA ABDALLA, PEMBA@@@@
UDHALILISHAJI ni kile kitendo ambacho hufanyiwa mtu yoyote bila ya ridhaa
yake.
Na wakati mwingine kitendo hicho, kikashusha hadhi,
thamani, utu, kuvurugika kwa ajili, kimwili, kijamii na hata kiuchumi kwa
mtendewa.
Katika ulimwengu wetu wa sasa, kesi za
udhalilishaji zimezidi kushamiri kila siku zikenda mbele, watuhumiwa wanaongezeka
mitaani kwa kila leo.
Tatizo kubwa linalowakumba wanajamii ni kuoneana muhali
kutokana na watendaji wa matukio hayo aidha ni watu wa karibu na familia, hivyo
ikigundulika kua ni baba au mjomba aliebaka basi kesi inamalizwa
kifamilia.
Haya si matukio mapya masikioni mwetu, ambayo
yanafanyika na badala yake watuhumiwa wanakimbia na kupelekea waathirika
kushindwa kupata haki yao.
WALIOPATA UKATILI WA UDHALILISHAJI WA KUBAKWA
Kwa mujibu wa mama mzazi wa Halima Juma (si jina lake
halisi) mkaazi wa kijiji cha Kidemeni wilaya ya Chake Chake, alisikitishwa
kutokana na tukio kama hilo, ambalo amelipata mwanawe, kwa kufanyiwa na baba
yake mzazi.
Akizungumza na mwandishi wa makala hii, anasema, alipata
mitihani huo kwa mwanawe mwenye umri wa miaka 22, ambae alikua akifanya kazi
kwenye ofisi ya mjomba wake.
Ingawa baadea mjomba wake kujua kama amefanyiwa
udhalilishaji na kapata ujauzito, aliamua kumfukuza kazini hapo.
"Ndio nilifanyiwa na baba yangu mzazi na alikua
akinipa vitisho vya kutaka kuniuwa, akawa ananambia nimeweza kukuzaa kwa hiyo
na kukuua naweza, hivyo ukija ukimwambia mamako au mtu yoyote nakuua,"
alieleza huku akifuta machozi.
Anaeleza kuwam kutokana na kutishwa huko, aliendelea
kunyamanza hadi alipopata ujauzito, ndipo ilipogundulika na hasa baada ya kuhojiwa.
Baada ya kujulikana kuwa ni mjamzito, baba yake
alikimbia na yeye alifukuzwa kazi na mjomba wake, kwa madai ya kushindwa kutoa
taarifa mapema ya udhalilishaji aliokuwa anafanyiwa.
“Baada ya yote kutokea, mzazi wangu alikimbia na
kutuacha pekeyetu, na hata kule nilipokuwa nafanyia kazi, nilifukuzwa eti kwa
sababu sikusema mapema niliyokuwa nafanyiwa,” anaeleza.
Kwa upande wake mama mzazi wa kijana huyo, anasema
aliumia kutoka na madhila aliyoyapata mwanawe, baada ya kusikia kuwa baba yake
ndiye mhusika wa ujauzito huo.
‘’Niliumia sana kitendo hiki na hasa kufanyiwa na baba
yake, ambae amemzaa, maana nilitarajia awe mlinzi wa kweli na mwadilifu kwa
mtoto wetu, leo amemvunjia ndoto na maisha yake,’’anasema.
Alifuatilia sana kesi hiyo, kwa muda mrefu lakini alivyoona hakuna matumaini ya mtoto wangu kupata hake, kisha nilikata tamaa na kuendelea na shughuli zangu nyingine,’’anasimulia.
Sasa anasema ni kazi ya serikali kuu, kuongeza nguvu na
kuwasaidia waathirika kuwafuatilia watuhumiwa wa kesi hizo wanaokimbia, ili
wakamatwe na kurejeshwa kwa lengo la kuwezesha haki kupatikana.
Anaona kuendelea kwa utamaduni wa muhali katika jamii,
inachangia kwa kiasi kikubwa kesi hizo, kushindwa kufikia hatua nzuri kutokana
na watu kufichiana maovu.
"Tatizo letu kubwa bado tunaoneana muhali na tuna
uwelewa mdogo juu ya suala kama hili, tunalichikulia kama kawaida tu, kwasababu
mbakaji anatoka ndani ya familia japokua watoto wetu wanaathirika kiakili na
kimwili,” alieleza.
KUTOKA MAHAKAMANI
Kwamujibu wa Mrajisi kutoka mahakama maalum Chake
Chake, Faraji Shomar Juma, anasema kwa miaka ya karibuni, hakujawahi kupelekwa
kesi kama hizo na itatokea mtuhumiwa akitoroka, kiupande wao kesi hawaifuti.
"Hukumu nyingi za watuhumiwa kutoroka zipo
kwasababu wanahusika huwatafuta na wakiwapata huwarudisha mahakamani ili
kusomewa adhabu yake ili wakatumikie vifungo vyao,” anaeleza.
Aliitaka jamii kuripoti kwa wakati tukio linapotokea,
ili kudhibiti watuhumiwa kukimbia na kuwezesha kuchukuliwa hatua kabla ya
kukimbia.
KUTOKA AFISI YA MKURUGENZI WA MASHTAKA
Mwendesha mashtaka wa ofisi hiyo, Ali Amour Makame anasema
kwa mwaka 2022, kesi kama hiyo ilitokea moja (1), ambayo mtuhumia alitoroka
ndani ya mikono ya Jeshi ka Polisi, baada ya kufika katika kituo cha Polisi Chake
chake.
Anasema kesi kama hizo, zinakwamisha wahanga na
kujikuta wapo katika kipindi kigumu cha maisha na wengine hata kuamua
maamuzi mabaya katika maisha yao.
‘’Kwa ujumla kesi ambazo zimefika mahakamani, ikiwa
zimesomwa na kupatiwa hukumu, mwaka jana zilikua 40, na mwaka huu wa 2023 hadi
sasa zimefika kesi 48, ingawa hizi za kutoroka mwaka huu hatujapata hata moja,’’anaweka
wazi.
WANAHARAKATI WA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO
Nae Mkurugenzi mtendaji wa Jumuia ya TUMAINI JIPYA Tatu
Abdalla Msellem anasema wameweka mfumo wa kutoa taaluma kwa jamii, kwa sababu bado
ina uwelewa mdogo kuhusiana na mambo ya udhalilishaji.
Wametshatoa taaluma katika sheihia mbali mbali kwenye
mkoa wa Kusini na Kaskazini Pemba, ingawa hawajawahi kupokea kesi ya mtuhumiwa
kutoroka.
Alisema ikiwa taasisi yake inatimiza miaka mine ya
kushughulikia kesi hizo katika wilaya ya chake chake, mkoa wa wakusini Pemba
wamepata shehia 14 na kwa upande wa mko wa kaskazini wilaya ya
Micheweni wamepata shehia nne, ambazo wamefikisha taaluma hiyo.
Mkurugenzi wa Chama cha waandishi wa Habari Wanawake
Tanzania TAMWA-Zanzibar Dk. Mzuri Issa Ali, anasema jamii kama haijaamua kwa
vitendo, wadhalilishaji wataendelea kukosekana kila siku.
‘’Zipo baadhi ya familia, mara linapotokezea tukio
huanza kukaa chini pamoja kutafuta sulhu, na ikishindikana wanakimbilia Polisi
na mtuhumiwa anapa mwanya wa kukimbia,’’anasema.
Wamekuwa na miradi mbali mbali ikiwemo ya kuwawezesha
waandishi wa habari, namna bora ya kuandika habari hizo kwa ufanisi, jamii ipate
kujua njia za kupunguza matendo hayo,’’anaeleza.
Akaligeukia Jeshi la Polisi kuzidisha kasi ya ufuatiliaji
wa matukio hayo, ili jamii ipate kuwaamini na kuona ni sehemu salama ya kukimbilia,
yanapotokezea matendo hayo.
‘’Tunachoomba kwa jamii na vyombo vya sheria, ni
kuzidisha ushirikiano na TAMWA, ili kile ambacho tunakifanyaka kama kuiunga
mkono serikali kuu, kifanikiwe,’’anasema.
Mratibu wa Jumuia kwa ajili ya watu wenye Ulemavu wa
akili Zanzibar ZAPDD, ofisi ya Pemba Khalfan Amour Mohamed, anasema mzigo wa
udhalilishaji na kisha watuhumiwa kukimbia, zaidi huwaathiri ambao ni walemavu
wa akili.
‘’Hata familia inapotokezea aliyedhalilishawa ni binaadamu
mwenye ulemavu wa akili, ushughulikiaji wa kesi hiyo, huwa hafifu na hata
ikifikishwa mbele ya vyombo vya sheria, mwisho wa siku hufutwa,’’anasema.
Mratibu wa Baraza la taifa la watu wenye ulemavu Zanzibar
ofisi ya Pemba Mashavu Juma Mabarouk, anasema athari ya wadhalilishaji kukimbia,
lazima itafutiwe suluhisho la kudumu.
KUTOKA KITENGO CHA MKONO KWA MKONO
Afisa mshauri kutoka Wizara ya Afya Hospitali ya
Chakechake katika kitengo chamkono kwa mkono, Tatu Abass Machano anasema kesi
nyingi zinazohusu familia zinazoripotiwa kituoni hapo, zinafika kwa kuchelewa
na kupelekea ushahidi kupotea.
‘’Kwa mfano mtoto kabakwa tangu Oktoba 3, wazazi watuleta
baada ya siku10 au kuzidi, wanakua kwanza wakijishauri nini wafanye na hata
wakija kwetu, zile alama za muda ule alofanyiwa lile tendo hazipo tena, jambo
linalokwamisha upatikanaji wa ushahidi,”anasema.
Ndio maana anaiomba serikali na wadau wingine, kuendelea
kutoa taaluma kwa jamii, kupitia makundi mbali mbali, ili ielewe umuhimu wa
kuripoti kwa wakati matukio ya udhalilishaji.
MWALIMU WA MDRASSA
Mwalimu mkuu wa Madrassatu Nurul -Huda iliopo
kijiji cha Mjengo wa banda shehia ya Wawi, Omar Mohamed Omar, anasema bado
jamii inashindwa kulitatua suala hili, kwa sababu wao wanalichukulia kawaida.
‘’Kutokana na visa kama hivi, sisi walimu wa Madrassa
tunaziomba taasisi zote kuongeza juhudi ya kutoa elimu kwa umma, ili kukomesha
vitendo vya udhalilishaji wa watoto,”anafafanua.
Hivyo basi serikali ihusishe mashirika mbalimbali nayo
yaweze kuendelea kutoa elimu juu yasuala hili kwani baadhi ya matukio ya
udhalilishaji, huhusishwa na imani za kishirikina.
VISA NA MIKASA YA UDHALILISHAJI
Khamis Ali Diri wa Ukunda shehia ya Kengeja wilaya ya
Mkoani, hadi sasa anatafutwa na Jeshi la Polisi, kwa tuhma za kumpa ujauzito mmoja
wa shemegi yake ambae ni mwanafunzi wa darasa la nne.
Haji Mjaka Hashim wa Wawi, sasa anatimiza miaka minne, akiwa
hajarudi kwao, tokea alipodaiwa kufanya tukio la udhalilishaji kwa mtoto mwenye
ulemavu mchanganyiko kijijini hapo.
Hassan Iddi Othman na wenzake wawili nao kwa sasa
wanatafuta na Jeshi la Polisi baada ya kudaiwa kubaka kwa kundi, eneo la Wesha
miaka miwili iliyopita.
Ingawa Mossi Othman Mossi wa shehia ya Mchakwe Mwambe
wilaya ya Mkoani, baada ya kikumbia kwa mwaka mmoja, hivi karibuni alikamatwa
na Jeshi la Polisi, na kufikishwa mahakamani akikabiliwa na tuhma za kumpa
ujauzito mara mbili shemegi yake.
MWISHO.
Comments
Post a Comment