NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR@@@@
MOJA ya jambo muhimu ambali wazazi na walezi
waliowengi ambalo hawalifanyi hasa kwa miaka ya siku hizi, ni kukosa kuwa
karibu na watoto wao.
Ni tofauti kabisa na karne zilizopita, ambapo wazazi na walezi
hao walitenga muda kukaa na watoto wao, kama sio wajukuu na kuwapa maelekezo ya
hatma ya maisha yao.
Wapo walikuwa wakithubutu kuwapa hadithi za mafundisho, namna
bora ya kukabiliana na maisha na au wakati mwengine hata jinsi ya kupambana na
adui.
Kwa karne ya sasa
wazazi hujifanya hawana nafasi hiyo, wengi wakisingizia ugumu wa maisha, na hao
wachache wanaokanaa nao, hukosa kuwapa dunia ilipofikia.
Ndio maana mwanaharakati wa masuala ya kupinga ukatili na
udhalilishaji Aisha Muhidin Juma wa Fuwoni, anasema kwa kule wazazi kukosa
nafasi hiyo, husababisha watoto kuwa wapweke.
Kisha kinachofauta anasema ni kugubikwa na madhara makubwa kwa
watoto hao, tena hasa ikiwa wameshafanyiwa vitendo vya ukatili na
udhalilishaji.
Anaona wapo wazazi wamekuwa wakali kipitiliza, iwe tayari
wameshagundua udhalilishaji kwa mtoto wake, au wakati anataka kugundua jambo
hilo.
Hali hii inatokea kuwepo kwa ukimnya, ambao huibua madhara
mengi kwa mtoto huyo, ikiwemo madhara ya kisaikolajia pamoja na kukosa haki ya
sheria.
Je, unatambua madhara ya kisaikolojia ni nini?
Ni ile hali inayojulikana na mawazo yasiyo ya kawaida, hisia,
na tabia hali hii humkumba mtoto na kusababishia kupata ugonjwa wa akili
ikiwemo wasiwasi.
Watoto,
wa kike kwa kiume, wa umri hadi wa balehe, wanachezewa sehemu zao za siri,
wanabakwa, kulawitiwa na kutelekezwa kiasi cha kuzusha tatizo kubwa zaidi la
umasikini na unyimaji wa haki zao za msingi.
Bint
Chausiku sio jina halisi mwenye umri wa
miaka 22, sasa hivi, akiwa kidato cha tatu, alifanyiwa kitendo cha udhalilishaji
na mjomba wake.
Anasimulia
kuwa, tukio hilo lilitokea mwaka 2012, na kwa wakati huo anasema hakuweza kumueleza
mtu yoyote nyumbani kwao, kwasababu ilikuwa naogopa.
Anasema
mjombo wake huyo, alikuwa na tabia ya kwenda chumbani kwake, kwa mtindo wa kunyatia
nyatia, na kuanza kumshishika shika sehemu zake za siri.
Wakati
mwengine alikuwa akishtuka na kisha mjombo wake huyo, huanza kujisogeza pembeni,
huku yeye machozi yakiwa yanamtoka kwa kuumia kufanyiwa kitendo hicho.
"Alikuwa
haji siku zote, bali alikuwa anatenga muda nisahau na kunisogelea siku nyingine,
ilikuwa ni kawaida yake kipindi chote hicho hadi mama yangu alivyo aga dunia mwaka
2017,’’anasimulia.
Sababu
iliyopelekea kushindwa kutoa taarifa, ni kwasababu mama yake alikuwa ni mgonjwa
wa figo, hivyo alihofia kumzidishia maumivu mingine.
Lakini
hata familia yao, anasema ilikuwa na thamani ndogo mno kwa marehemu mama yake,
hivyo alijiona ni mtu wa kuteseka kila siku katika maisha yake.
Bint
huyo anaeleza athari alizozipata, ikiwemo kukumbuka mara kwa mara, kupatwa na
hasira, kulia pamoja na kumchukia mjomba wake huyo hadi watoto wake.
"Na
tukiwa tunapewa elimu kuhusina na matendo ya udhalilishaji katika makongamo
yoyote ikiwemo skuli, hua nakuwa mnyonge na kujilaumu katika nafsi yangu, na
kujificha mtu asijenigundua kua na mimi nishawahi kufanyia vitendo vya
udhalilishaji,’’anasema,
Naye
Mkuu wa Division ya Afya ya Akili wa Kidonge Chekundu Khadija Abdulrahmani Omar,
anasema mtoto ambae amefanyiwa vitendo vya udhalilishaji kwa muda mrefu, bila
ya tukio kuripotiwa anatakiwa kupata tiba ya afya ya akili.
“Mtu
yoyote atakaefanyiwa vitendo vya udhalilishaji, anapata athari mbali mbali
ikiwemo utumiaji wa dawa za kulevya, kukumbuka mara kwa mara na hasa akisikia
matukio hayo kutokea, kuchukia wanaume wote,’’anaeleza.
Anasema haijalishi, hata kama mtoto alikosa kutoa taarifa kwa
wakati kutokana na ukimnya wake, anaweza kupatiwa matibabu ya afya ya akili, na
kurudi katika hali yake ya kawaida.
"Kituo chetu cha Mkono kwa Mkono, wapo wataalamu wa saikolojia
ambao wanasaidia kuwapatia huduma ya afya ya akili, wahanga ambao wameathirika
kisaikolojia na huduma hizi zipo za aina tatu ikiwemo tiba ya biolojia,
sykolojia na ustawi wa jamii,’’anasema.
"Tiba ya biolojia ikiwa mtu amepata wasiwasi kutokana na
tatizo hilo, anapewa dawa na kuenda kutumia, sykolojia itamsaidia kuondoa zile
hisia, ambazo zinamjia ikiwemo kujiona
hana thamani kwa jamii,’’anasema.
Wameshapokwa matokeo 11, ambayo yametokea kwa muda mrefu na
kwa sasa wahanga hao, wanapatiwa huduma katika kituo cha Kidonge Chekundu.
"Watoto saba, wasichana wa nne chini ya umri wa miaka18
na wa watatu wavulana chini ya umri wa 15 ndio walifanyiwa vitendo vya ukatili
na udhalilishaji, kwa miezi sıta iliyopita,’’anafafanua.
Pamoja na wanawake wanne chini ya umri wa miaka 35, hawa
wamefanyiwa miaka 10 iliyopita, na sasa hupata matibabu katika hospitalni hapo.
Aidha aliwasaa wazazi kuwapeleka wahanga katika vituo vya afya ya akili, kwa ajili ya
kupata matibabu kwani wanapochelewa humsababishia maradhi ya afya ya akili .
Sheha wa shehia ya Urusi Yussuf Juma Mtumwa, ansema wapo wahanga,
ambao wanafanyiwa vitendendo vya udhalilishaji na kuchelewa kuripotiwa na
kupelekea wahanga hao kuathirika kisaikolojia.
"Ni kweli matukio ya udhalilishaji yapo katika wilaya
zetu, na wahanga wanashindwa kutoa tarifa na kupelekea kuathirika kisaikolojia,
ikiwemo kujitenga na makundi ya watu,’’anafafanua.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Mtakwimu mkuu wa serikali, iliyotolewa na
afisa wao, Asha Mussa Mahafudhi, anasema kwa mwaka huu pekee ya 2023, tayari
kumseharipotiwa matukio 1,421.
Ambapo
hii ni tofautai na mwaka jana, ambapo kulikuwa na matukio 1,361 yalioripotiwa,
na wengine wa wathirika hao ni watoto sawa na
asilimia 84.4, wanawake asilimia 11.4 na wanaume ni asilimia 4.2.
Wilaya
ya Magharib ‘A’ iliongoza kwa kuwa na matukio 328 ikifuatiwa na wilaya ya Mjini,
iliyoripoti matukio 322 na wilaya ya Magharibi ‘B’ matukio 294.
Katika matukio yote 1,421 ya udhalilishaji yaliotokea mwaka
huu, matukio ya ubakaji yaliongoza kwa kuripotiwa 682, ambapo wanawake chini ya umri wa miaka 35 walikua 65 na
wasichana chini ya miaka 18, yalikuwa 619.
Ingawa kwa upande wa makosa ya shambulio la ilikuwa 267 sawa
na asilimia 18.8, huku wanawake chini ya miaka 35, yakiripotiwa 54 wasichana yalikuwa
matukio 79, wavula chini ya miaka 15, yaliripotiwa 85, huku wanaume yalikuwa
matukio 49 kwa wale chinia ya umri kunzia miaka 18.
Mkurugezi
wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Siti Abasi Ali, anasema kuna umuhimu wa
kuwapatia elimu ya kisaikolojia wahanga, waliofanyiwa vitendo vya udhalilishaji.
Hii
anaona itawaweka sawa na kusaidia kwa kiasi ikukubwa afya yao ya akili na
kuacha kijitenga wenyewe, kw akule kufikiria ukubwa na tatizo lililowakuta.
Hata
hivyo, anasema serikali imeweka waalimu maalum katika skuli zote, kwa ajili ya
kutoa huduma ya kwanza ya elimu ya saikolojia, pindi wanafunzi wakikumbwa na
ukatili.
Hapa
akawageukia wazazi na walezi, kuwa karibu na watoto wao kwa lengo la kuweza
kujua changamoto mbali mbali anayopitia mtoto huyo.
“Baadhi
ya wazazi wanakuwa wakali hadi mtoto anamuogopa na kushindwa kumueleza kitu
chochote, ambacho amekumbana nacho," anasema.
Mwanachi
Kombo Ali Haji, anasema unapokutwa na changamoto ya afya ya akili, ni vyema
kutafuta msaada kwa wataalamu, kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa changamoto hizo.
Mzazi
Aiman Juma Mlenge wa Kikwajuni anasema, kama wazazi hawakujitengea muda wa
kukaa na watoto, wanaweza kuwapa wakati mgumu, hasa kwa wale waliopata shida ya
ukatili na udhalilishaji.
Mkuu wa Dawati la Jinsia la watoto Inspector Mohamed Mwadini anasema
kuna athari mbali mbali, zinatokea ikiwepo mtu amefanyiwa vitendo vya udhalilishaji
na kukaa kiminya, ikiwemo kukosa haki yake ya msingi.
"Eneo ambalo amefanyiwa kitendo cha udhalilishaji inakua
lishabadilika, kwa hiyo inakua ngumu kupata ushahidi, kupata maambukizi kwa
urahisi, vilevile anaweza kuendelezwa kufanyiwa vitendo hivyo kutokana na ukiminya
wake,’’anasema.
‘’Akiwahi kutoa tarifa mapema atapelekwa hospital kwa ajili ya
kuangaliwa ikiwa ameshaambukizwa magonjwa ama laa, na hasa kwa vile pia zipo
dawa na kumkinga na baadhi ya maradhi,’’anasema.
Elimu juu ya athari za vitendo hivi vya udhalilishaji inatakiwa
itolewe kwa upana sana kwenye jamii zetu, haswa kwa wazazi kujua ni namna gani
wanaweza kuwagundua watoto walio athiriwa na vitendo hivi.
Ukaribu wa wazazi kwa watoto wao, ndio nguvu kuu itakayo
saidia kurudisha uhuru wa mtoto kumfikia mzazi wake na kumuelezea juu ya
changamoto ambazo atakutana nazo kwa watu watakao onesha dalili zozote za
udhalilishaji kwake.
Mwisho
Comments
Post a Comment