Na Sabiha Keis:::
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema itawanyang'anya umiliki
wa ardhi wanyenji na wageni ambao walipewa kwa ajili ya kuekeza lakini wameshindwa
kuyaendeleza hivyo sheria itachukua
mkondo wake bila ya kumonea mtu muhali.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Wizara ya Ardhi na
Maendeleo ya Makaazi Zanzibar Juma Makungu Juma huko Wilaya ya kati Mkoa wa
Kusini Unguja katika ziara maalumu ya kuyatembelea maeneo ambayo wageni na
wenyeji walipewa kwaajili ya kuekeza lakini bado hawajaekeza.
Alifahamisha kwamba sheria ya Umiliki wa Ardhi, sheria Nam:
12 ya mwaka 1992 kifungu Nam 48 (1a) kinaeleza ukiukaji wa ukodishwaji ardhi
(Violetion of the Restrictions in a lease) hivyo wizara yake itahakikisha
inafata sheria kwa wawekezaji wakigeni na wazawa ambao walipewa maeneo kwa
ajili ya uwekezaji na kutoyaendeleza kwa muda uliowekwa.
Alifahamisha kwamba lengo la ziara yake ni kuangalia pamoja
na kuyatambua maeneo yote ya ardhi ambayo yametolewa na Serikali na kuwapa watu
kwaajili ya kuekeza lakini bado wahusika wameshindwa kuyaendeleza kwa muda uliyowekwa.
Alisema Serikali haina
nia ya kumdhulumu mtu lakini kuna baadhi ya watu wameshindwa kuyaendeleza
maeneo ambayo walipewa hivyo hakuna sababu ya kuwaachia umiliki wa ardhi
mwekezaji huyo kwa sababu hakuna faida inayopatikana.
Aidha Naibu waziri Juma
ametoa wito kwa wawekezaji wote
walipewa maeneo ya ardhi kuhakikisha wanayaendeleza maeneo hayo kwani uwekezaji
hutoa fursa nyingi za ajira kwa vijana pamoja na kuiongezea nchi mapato.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji Kamisheni ya Ardhi Khamis
Juma Khamis amefahamisha kuwa zoezi hilo
linatarajiwa pia kufanyika katika maeneo yote ya uwekezaji ambapo hapo awali
Kamisheni ya Ardhi ilishatoa taarifa kwa wawekezaji wote waliopatiwa lease ya
ukodishwaji kuyaendeleza maeneo yao vyenginevyo sheria itachukua mkondo wake.
"Tulishawahi kutoa indhari kupitia vyombo vya habari kwa
wawekezaji wote kuhakikisha wanayaendeleza maeneo yao lakini ziara ya leo
tumebaini kuwa kuna maeneo bado yako vilevile nahayajaendelezwa chochote hivyo
kwa sasa kinafuata ni utaratibu wa kisheri utatumika"Alisisitiza Khamis"
Nae Sheha wa Shehia ya Uroa Muhsini Amour Adam ametoa wito
kwa wawekezaji ambao mpaka sasa bado hawajayaedeleza maeneo yao kuitumia fursa hiyo kwa kuyaendeleza katika
shughuli mbalimbali zikiwemo utalii kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi.
Maeneo yaliyotembelewa na kuonekana kuwa bado hayajaendelezwa
hadi sasa ni pamoja na pongwe,uroa na marumbi . Aidha kwa upande wa Wilaya ya Kati
Mkoa wa Kusini Unguja ziara kama hiyo inatarajiwa kufanyika Mkoa wa Kaskazini
Unguja.
Mwisho.
Comments
Post a Comment