NA HAJI NASSOR, PEMBA:::
MDAU wa amani Abubakar Kabogi, amesema dunia inavutiwa
mno na juhudi za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kusimamia amani nchi.
Alisema, dunia imekuwa ikifuatilia kwa karibu mno namna serikali inavyohamasisha
utunzaji wa amani na utulivu, iwe kabla, baada ya uchaguzi au wakati wa
uchaguzi mkuu wa vyama vingi.
Mshauri huyo
wa masuala ya amani barani Afrika aliyasema hayo
ukumbi wa Samail Gombani Chake chake wakati akisalimiana na mabalozi wa amani
kisiwani humo.
Alisema,
bado wadau wa ndani na wale wa kimatifa wanaendelea kuunga mkono juhudi za mabalozi hao pamoja na serikali
kwa ujumla, katika mradi wa amani yangu, ambao upo Tanzania kwa muda mrefu.
Mdau huyo
alieleza kuwa, bado mabalozi hao wanawajibu wa kuendelea kufanyakazi kwa karibu
na serikali yao, ili kuhakikisha amani iliyopo Zanzibar inaendelea kudumu.
‘’Visiwa
hivi ni vizuri na ni sehemu yenye utulivu kuishi, hii ni kwa sababu ya kuwepo
kwa amani ya kudumu,’’alieleza Abubakar.
Katika hatua
nyingine Mdau huyo wa masuala ya amani barani Afrika, aliipongeza Ofisi ya Mufti mkuu Zanzibar, kwa kuendelea kuwalewa mabalozi
hao wa amani.
Mratibu wa
ofisi hiyo Pemba Sheikh Said Ahmad Mohamed, alisema, sasa suala la kuinadi
amani limekuwa jambo la kila siku katika jamii.
‘’Maana
wanachi wa Unguja na Pemba wanapoona madhara ya machafuko ya nchi jirani na
jinsi watoto na wanawake wanavyohangaika, huwa wanaitunza amani
hiyo,’’alieleza.
Mwakilishi
wa mabalozi hao Bakar Mussa Juma, alisema elimu waliyoipata ya utatuzi wa
migogoro, imesaidia sana kuona Zanzibar kunafanyika chaguzi za amani.
‘’Tuliwaelewa
sana kuwa, kumbe suala la utunzaji wa amani sio kwenye uchaguzi pekee, iwe
inahubiriwa kila wakati na kila pahala, na hilo limefanikiwa,’’alieleza.
Hata hivyo
amemuomba Mshauri huyo wa masuala ya amani baraani Afrika kutoka serikali ya
Uswis kuendelea kuinga mkono Zanzibar, katika kutunza na kuaendeleza amani
iliyopo.
Mwisho
Comments
Post a Comment