NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
AFISA Mdhamini wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Pemba, Zuhura
Mgeni Othman, amesifu zoezi la awali la utambuzi wa ulemavu, kwa wanafunzi wa
darasa ya kwanza wa skuli za Birikau na Michakaini, lilioendesha na Milele
Zanzibar Foundation, kwa kushirkiana na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chake chake.
Alisema zoezi hilo, ndio ambalo
litawaibua mapema wanafunzi wenye magonjwa mbali mbali pamoja na wale wenye
ulemavu, na kuanza matibabu mapema.
Afisa Mdhamini huyo, aliyesema hayo
skuli ya Michakaini, wakati akilifunga zoezi hilo la siku nne, ambalo
liliwafikia wanafunzi zaidi ya 500 kwa skuli hizo.
Alieleza kuwa, upo baadhi ya aina ya
ulemavu unaweza kupona na kumuacha mtoto akiwa salama, kama hali hiyo
itatambulika mapema, kama ilivyofanya Milele chini ya ofisi ya watu wenye
ulemavu ya wilaya ya Chake chake.
Alifafanua kuwa, msingi mkuu wa
mwanafunzi kuweza kusikiliza kwa umakini, kupata ufahamu na kufikia lengo lake
akiwa masomoni, afya njema na imara ni jambo la lazima.
‘’Mimi niwapongeza sana wenzetu hawa
wa Milele pamoja na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Chake chake, kupitia ofisi ya
watu wenye ulemavu wilayani humo, kwa kuandaa zoezi hili, ambalo ni jema kwa
afya na makuzi ya watotowetu,’’alieleza.
Katika hatua nyingine, Afisa Mdhamini
huyo wa Utalii na Mambo ya Kale Pemba Zuhura Mgeni Othman, aliwaumbusha waalimu
hao, kutowanyanyasa wanafunzi wenye uwezo mdogo wa usikivu, uoni na ufahamu.
Hata hivyo amewakumbusha wazazi na
walezi, kuchangamkia fursa kama hizo, kwani kama sio zoezi hilo kufanyika,
gharama kubwa yengehitajika kufanyiwa vipimo hivyo watoto wao.
Aidha amewakumbusha wanafunzi wa kike,
kusoma kwa ushindani na wenzao wa kiume, kwani kiongozi mwema na jemedari wa
kike, anaanzia kwenye kwenye elimu.
Mapema Afisa Miradi kutoka Milele
Zanzibar Foundation Fatma Khamis Silima, alisema taasisi hiyo imekuwa karibu
mno na jamii, kwa kuimarisha maisha yao kwa ujumla.
Alisema, zoezi hilo ni eneo moja
ambalo Milele imekuwa ikisaidia, lakini hata kwenye eneo la elimu, afya na
stahiki nyingenza jamii na hata mtu mmoja mmoja.
‘’Tulipofuatwa na ofisi ya Mkuu wa
wilaya, chini ofisi ya watu wenye ulemavu wilaya ya Chake chake, hatukurudi
nyuma, maana Milele, inaguswa mno na afya kwa jamii,’’alieleza.
Hata hivyo alisema tokea kuanzishwa
kwake mwaka 2014, hadi sasa imeshajenga vituo vya afya, nyumba za madaktari
pamoja na skuli mbali mbali, na sasa ikiwa na mipango kadhaa, ya kuongeza
ufafamu kwa wanafunzi.
Akisoma risala ya zoezi hilo, Afisa
Mipango wilaya ya Chake chake Kassim Ali Omar, alisema zoezi hilo limeibua
changamoto kadhaa, kwa wanafunzi wa madarasa ya kwanza wa skuli za Birikau na
Michakaini.
Alisema, baada ya zoezi hilo,
wanafunzi wengine walipatiwa dawa na wengine wameunganishwa na hospitali mbali
mbali, kwa matibabu na uangalizi wa kina.
Alieleza kuwa, zoezi hilo limeibua changamoto
mbali mbali kwa wazazi, wanafunzi na madaktari, ikiwa ni pamoja na kuonesha
umuhimu wa kufanyika kwake kila baada ya muda.
‘’Utamaduni wa kuchunguuza afya
umepotea, na ndio maana katika zoezi hili, zipo kesi za kiafya zilipaswa
zigundulike mapema, lakini ni tofauti na hali ilivyo,’’alieleza.
Wawakilishi kutoka wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Amali pamoja na wizara ya Afya, wamepongeza zoezi hilo, na kuahidi
kutoa kila aina ya ushirikiano, kila wakati.
‘’Kwanza niwapongeze madaktari wetu
kwa moyo wao wa ujasiri na wa kujitolea, ambao umefanikisha zoezi hili, ambalo
sasa limewasaidia wanafunzi wetu katambua afya zao,’’walisema.
Zoezi hilo la utambuzi wa awali wa ulemavu
kwa wanafunzi wa madarasa ya kwanza wa skuli za Birikau na Michakaini,
lililoanza Febuari 28 na kumalizika Machi 3, limewafikia wanafunzi wa skuli za
Michakani ‘A’ 213, Michakaini ‘B’ 251 na skuli ya Birikau wanafunzi 96.
Mwisho
Comments
Post a Comment