Skip to main content

SUNGURA: 'WELEDI, UMAHIRI KADA YA HABARI NI NGUZO MUHIMU

 


NA MWANDISHI MAALUM, MCT-ZAZNAIBAR@@@@

Waandishi wa habari wametakiwa kufuata kwa kina maadili ya waandishi wa habari ili kukuza weledi na umahiri wa kada ya habari na kuzifanya taasisi za kihabari ziweze kuaminika na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.

Akizungumza na wadau wa habari katika ziara yake iliyofanyika Zanzibar tarehe 23 na 24 Machi Katibu Mtendaji wa Baraza la Hbbari Tanzania MCT  Ernest Sungura amesema kuwa  katika kufuata maadili hayo pia suala la kuzingatia vyanzo anuai vya habari havina budi kupewa kipaumbele.

“Mara nyingi waandishi wetu wamekuwa na maradhi ya chanzo kimoja cha habari hali hii inapaswa kubadilika ili habari zetu ziweze kuwa na mawanda mapana zaidi na vyanzo vingi na tofauti vya habari”, alisisitiza.



Amesema kuwa nguvu ya vyombo vya habari haina budi kutumika katika kujenga jamii iliyo bora na hivyo sauti za watu hazina budi kupewa kipaumbele.

“taasisi za habari na vyombo vya habari havina budi kubadilika ili sauti za makundi ya pembezoni ikiwemo wanawake na vijana ziweze kusikika tuwape sauti wale wasio na sauti”, aliongeza.

Akizungumzia kuhusu masuala ya jinsia katika vyombo vya habari amesema kuwa bado waandishi wa habari wanawake hawakupewa fursa zinazostahiki na hivyo kunatakiwa juhudi zaidi katika kuimarisha waandishi hao.

Wahariri wana dhima na dhamana ya kuwanyanyua waandishi wanawake ili wawe mahiri katika kazi zao lakini na wamiliki na viongozi wawape nafasi ya kuwemo katika nafasi mbali mbali za uhariri ili usawa na haki kwa jinsia zote uweze kupatikana.

Baraza la habari linathamini mchango wa wanawake katika kuimarisha kada ya habari na baraza lina mradi maalum ya kuimarisha haki na usawa wa jinisia katika vyombo vya habari., alifafanua

Hata hivyo alikiri kuwa utafiti wa baraza la habari Tanzania wa mwaka 2019 umebainisha kuwa ingawa wanawake wapo katika vyombo vya habari lakini bado nafasi za ngazi za juu ikiwemo wahariri bado zimedhibitiwa na wanaume.



“HIvyo basi ili kuimarisha hayo katika mradi maalum wa baraza la habari  wa kuwanyanayua wanawake katika vyombo vya habari unaofadhiliwa na shirika la Vikes la serikali ya finland kuna mkakati maalum wa kuwajengea uwezo katika masuala ya uongozi kwa wanawake katika vyombo vya habari “, alifafanua.

Alivitaka taasisi za kihabari kufanya kazi kwa pamoja katika kuimarisha kada ya habari pamoja na kuwafanya waandishi wa habari wafanye kazi zao kwa weledi na umahiri.

Mkurugenzi wa tamwa Zanzibar Dk. Mzuri issa amesema kuwa Tamwa itaendelea kufanya kazi kwa karibu na MCT katika suala zima la kuimarisha kada ya habari lakini pia kukuza na kuimarisha weledi wa waandishi wa habari wanawake.

“Tuna umoja wa taasisi za habari unaojulikana ZAMECO chini ya umoja huu tunafanya kazi za kuimarisha kada ya habari  ikiwemo kufanya uchechemuzi wa shaeria za habari za Zanzibar “ alifafanua.

Mhariri mtendaji wa shirika la magazeti ya serikali Ali Mwadini amesema kuwa weledi na umahiri ni muhimu katika kada ya habari na kuimarisha kwa kina vyumba vya habari ili kuwe na madawati maalum ya kushughulikia habari tofauti.

“Kunahitajika madawati ya habari za uchunguzi, habari za vijijini ili kuvifanya vyombo vyetu viweze kuandika habari ambazo zitaibua kero za wananchi na hususan wa vijijini”, aliongeza.

Vyombo vyetu vya habari vimetawaliwa na habari za mjini na habari za matukio hali hiyo inatakiwa ibadilike ili viweze kuleta mabadiliko katika jamii.

Katibu wa Zanzibar Press Club Mwinyimvua Nzukwi alisema kuwa kufanya kazi kwa pamoja ni nguzo muhimu ya kuimarisha kada ya habari na hivyo Zannzibar Press Club itaendelea kushirikiana na Baraza la habari ili kuleta maendeleo katika kada ya habari.

Katibu mtendaji wa baraza la habari Tanzania Ernest Sungura amefanya ziara rasmi ya siku mbili hapa Zanzibar ikiwa ni shemu muhimu  ya kukuza na kuimarisha mahusiano kwa taasisi za habari pamoja na kuimarisha kazi za baraza la habari hapa nchini.

Katibu mtendaji alitembelea ofisi ya watetezi wa haki za binaadamu ofisi ya zanzibar, Tamwa Zanzibar, Klabu ya waandishi wa habari Zanzibar, na shirika la magazeti ya serikali.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 mchan

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’’ali

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa ufafan

MADAKTARI KUTOKA CHINA WAOKOA MAISHA YA MTOTO PEMBA

  HABIBA ZARALI, PEMBA TIMU ya 32 ya madaktari wa kichina katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani wamefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa wa mtoto mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Chole Kengeja, baada ya kuchomwa na jiti sehemu ya njia zake za mfumo wa uzazi. Mtoto huyo ambae alianguka hivi karibuni katika mti na baadae kuchomwa na jiti hilo na kumsababishia kutokwa na damu nyingi katika sehemu ya nyonga, alifanyiwa upasuaji uliodumu kwa muda wa saa tatu na   kuokolewa maisha yake. Akizungumza mara baada ya operesheni huo kiongozi wa timu hiyo Dr Jiang Jinhua, alisema mara baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini hapo na kufanyiwa vipimo na kuonekana   ilibidi apatiwe rufaa ya kwenda katika hospitali nzuri yenye kutibu tatizo lake huko nchini Kuwado ambapo haikuwezekana kutokana na hali ya umaskini wa f amilia ya mtoto huyo . Alisema timu ya madaktari hao itaendelea kutowa huduma za matibabu   kwa wananchi kisiwani humo,   ili kuwaondolea gharama ya kutafuta matibabu nje ya nch