NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
āāTUNA mwaka mmoja sasa, shida ya maji sisi
wananchi wa kijiji cha Kinyasini wilaya ya Mkoani, tunaisikia kwenye vyombo vya
habari,āāwanasema wananchi hao.
Nilipotaka kujua kulikoni, wananchi hawa wanaishi kwenye
vivuli vya raha na burudani, hasa kupitia haki ya msingi ya huduma ya maji safi
na salama, hawakuwa wachoyo kusema ukweli.
Rukia Ramadhan Bakari, akizungumza kwa shauku anasema,
mkutano uliofanyika mwezi Febuari 2023, ulioitwisha na wasaidizi wa sheria wa wilaya
ya Mkoani, ndio chanzo kikuu cha kuzaliwa kwa mradi huo.
Mkutano huo pamoja mambo mingine ya kisheria, wananchi na
hasa wanawake, walielezea changamoto yao ya ukosefu wa uhakika wa huduma ya maji
safi na salama.
āāTulielezea changamoto yetu ya ukosefu wa huduma hiyo,
mbele ya wasaidizi wa sheria, na wao walituahidi kwamba changamoto hiyo
wataifuatilia,āāanakumbushia.
Baada ya kimnya kirefu cha wiki tatu, waliitwa tena
kupewa mrejesho na wasaidizi hao wa sheria, ingawa anasema wengi wao akiwemo
yeye, hakuamini.
āāUnaju dhiki tulionayo hapa kijiji cha Kinyasini wilaya
ya Mkoani ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama, hatukuwa tukimuamini
yeyote, na hata wao wengine tulishindwa kuamini,āāanasema.
Awena Nassor Ali, anasema muda sasa ukafika wa kuanza
kuiyaga shida na dhiki ya maji, baada ya wasaidizi hao wa sheria kuwaleta
kijijini kwao, wafadhili ya mradi wa uchimbaji kisima, ujenzi wa mnara wa tanki
la kuhifadhi maji na usambaazaji pia.
āāLililonifurahisha leo na kusahau dhiki, ni kuona
changamoto zetu zimefuatiliwa na kutekelezwa kwa vitendo, maana hadi mipira ya
kusambaazia huduma hiyo, tumewekewa na wafadhili,āāanaeleza.
Kumbe wananchi wa kijiji cha Kinyasani, na hasa kundi
kubwa la wanawake, ambao walikuwa wanategemea maji yanayozalishwa na
kusambaazwa na Mamlaka ya Maji Zanzibar āZAWAā walikuwa wanaishi kwenye wingu,
la kusaka maji.
āāSisi na watoto wetu, mpango wa kuamka saa 8:00 za usiku
ilikuwa ni jambo la kawaida, kuifuata huduma ya maji, mabondeni umbali ya
kilomita mbili hadi tatu,āāanafafanua.
Anakumbuka vyema, kuwa matumizi ya maji ya kutosha
hawakuwa na nafasi hiyo, kwani visima walivyokuwa wakivitumia vilikuwa na ujazo
mdogo wa chini ya lita 15,000 kwa saa.
Mradi huo uliobuliwa na wasaidizi wa sheria wilaya ya
Mkoani, anasema umekuja kuzima na kuzika kabisa shida na dhiki waliokuwa nayo
kwa muda mrefu, na sasa wanaishi kwa utulivu.
āāHaki zote za kibinaadamu na kinyumba zimetulia kwa
wananchi wa kijiji cha Kinyasani, kwani huduma ya maji, imerudi upya tena kwa
kasi,āāanasema.
Mwanaisha Makama Haji, anaona sasa kila nyumba wananchi
wanafua, kukoga na hata kumwagilia bustani kwa utulivu, kufuatia kilio chao
kupata mnyamazishaji.
āāKama wasiaidizi wa sheria wote Tanzania, watakuwa na
juhudi kama walizonazo hawa wa Mkoani, hakuna kijiji ambacho kitakuwa na shida
ya mradi wa maendeleo, na ufumbuzi usipatikane,āāanasema.
Kwake anaona, mkutano huo ulizaa matunda mengine, lakini
la kupatiwa ufumbuzi wa huduma ya maji safi na salama kwake, ni ndoto iliyopata
jibu.
Ndio maana sasa, anatoa rai kwa wananchi wenzake, kwanza
kuuenzi mradi huo, pamoja na kuuelea kwa nguvu zote, ili vizazi vijavyo,
vifaidike nao.
Mwananchi Hamad Mzee Hamad nae wa Kinyasini anasema, kazi
iliyofanywa na wasaidizi wa sheria, sasa kwake binafsi imemsaidia kupata
utulivu na mpangilio mzuri wa maisha yake.
āāSasa unalala na kuamka kwa wakati uutakao, maana huduma
ya maji safi na salama imo ndani ya nyumba yetu, maana wasadizi wa sheria,
wametusaidia kupatikana kwa mfadhili,āāanafafanua.
Msaidizi fundi mkuu wa mradi huo, Khatib Issa Maalim,
anasema wasaidizi wa sheria wa wilaya ya Mkoani, kupitia mradi huo, wamefanikiwa
kupunguza makali kwa wananchi wa Kinyasini.
āāAnakiri kuwa maji ya āZAWAā wakati mkubwa hukumbwa na
changamoto zinazowakwaza wananchi, hivyo kupatikana kwa mradi huo, ni faraja
kwao,āāanasema.
Hata hivyo anawashauri wasimamizi wa mradi huo, kuongeza
idadi ya matenki ya kuhifadhi maji, ili kulisaidia tenki la sasa lenye uwezo wa
kubeba lita 5000 pekee.
āāZuri zaidi lililomo ndani ya mradi huu, ni kwamba hata
kama huduma ya umeme itazimika, wanaweza kufungua tanki lao na kupata
huduma,āāanasema.
Mkurugenzi wa Jumuiya ya wasadizi wa sheria wilaya ya
Mkoani āMDIPAOā, Nassor Hakim Haji, anasema mradi huo ulitokana na mkutano
walioutisha kwa wananchi hao, na kisha kutaja changamoto yao hiyo.
āāKwa kushirikiana na wananchi, tulifanikiwa kuuibua
mradi huu, baada ya wenyewe kukiri kuwa, changamoto kubwa ni kutokuwa na
uhakika wa huduma ya maji safi na salama katika maisha yao,āāanaeleza.
Anakiri kuwa, baada ya kuundwa kamati na yeye kuwa
mjumbe, kazi ya kuanza kumtafuta mfadhili ilipamba moto, na kisha kufanikiwa
kuwapata, wanamkoani wanaoishi nje ya nchi.
āāBaada ya kuwasiliana nao, walitaka mchanganuo wa
gharama na kuwatumia, na baada ya wiki tatu, ujumbe wao ulifika na kuanza kazi
ya uchimbaji kisima,āāanaeleza.
Kisima hicho, kina zalisha wastani wa lita 35,000 kwa saa,
ambayo maji yake huvutwa kwa mashine, kutoka kisimani hadi kwenye tenki la lita
5000 kila siku, na kisha kusambaazwa kwa wananchi.
Mkurugenzi huyo anakiri kuwa, haikuwa kazi rahisi
kupatikana kwa mradi huo, ambao wafadhili waligharamia hadi utandaazaji mipira
midogo, iliyoingia nyumbani kwa wananchi.
āāHivi sasa nyumba 30 kati ya nyumba 52 zenye wakaazi
wastani wa 210, wananufaika na mradi huu, kupitia awamu hii ya kwanza, ambapo
awamu nyingine, itamalizia nyumba 22 zilizobakia na kufikia wananchi 450 kwa
mradi wote,āāanasema.
Kwa sasa anasema mradi huo, unalelewa na kamati maalum,
ambayo wasaidizi wa sheria ni wajumbe, na kukutana kila baada ya muda, ili
kuelezea changamoto zao.
Mkurugenzi huyo, anasema wamejipanga vyema kwa kuanzisha
mfuko maalum, kwa ajili kuulinda na kuimarisha mradi huo, ikiwemo michango kwa
ajili ya umeme wa kusukumia maji, hadi kwenye tenki.
Afisa sheria kutoka Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria
Zanzibar ofisi ya Pemba, Bakari Omar Ali, anasema uibuaji wa miradi hiyo, ndio
miongoni mwa mafanikio ya kuwepo kwa wasaidizi wa sheria Zanzibar.
Anasema, wapo wananchi waliokwisha kata tamaa, sio kwenye
kufuatilia masuala ya haki zao za kisheria pekee, bali hata huduma za kijamii
kama maji safi na salama.
āāKwa mfano, kuna hao wananchi wa kijiji cha Kinyasini,
walikuwa na kilio cha ukosefu wa huduma ya maji safi na salama, lakini wapo
wingine, wanalalamikia ukosefu wa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi na vyeti
vya kuzaliwa,āāanasema.
Hapa akawataka wongeze juhudi, ili kuhakikisha wanaibua
changamoto nyingine, zilizowazungumka wananchi, ili kuondoa hisia za kuishi kwa
matabaka.
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na
Utawala Bora Zanzibar, Haroun Ali Suleiman, akizungumza hivi karibuni, alisema,
wasaidizi wa sheria wataendelea kuwekewa mazingira rafiki kila hali
inaporuhusu.
āāKwanza, tutaendelea kufuatilia ahadi ya Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, ya kuwapatia
usafiri wa bajaji kila jumuia,āāanafafanua.
āāHili litawapa hamasa na nguvu wasaidizi wa sheria, kwa
kuendelea kuibua changamoto zinazowakwaza wananchi wa Unguja na Pemba.
Wakili Alphonce Gura, kutoka tasisi ya LSF anasema, ikiwa
wasaidizi wa sheria watafanyakazi kwa bidii, manufaa yake kwa jamii hayachelewi
kuonekena.
Mkuu wa wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, anasema āMDIPAOā
ni moja ya jumuia za wasaidizi wa sheria, zinazofanyakazi zake, kwa hamu ya
kutatua changamoto za wananchi.
Mwisho
Comments
Post a Comment