NA MWANDISHI MAALUM, @@@@
Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mwanaasha Khamis Juma wamefanya ziara mkoani Mtwara ya kutembelea miradi ya gesi asilia kwa lengo la kujifunza.
Wakiwa katika ziara hiyo ya siku Moja wametembelea visima mbalimbali ikiwemo miundombinu ya gesi ya Mnazibay pamoja na kiwanda cha kuchakata gesi Madimba.
Akizungumza mara baada ya kuwakaribisha Mkoani Mtwara Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mwanahamis Munkunda amesema kuwa gesi asilia imekuwa chachu kwa maendeleo ya mikoa ya lindi, mtwara na Tanzania kwa ujumla.
Amesema uwepo wa gesi hiyo ni fursa kubwa ambayo watajifunza na wataiona jinsi inavyofanyakazi ambapo ndio malighafi inayotumika viwandani, majumbani na pia ni nishati inayotumika kuzalishia umeme.
"Gesi kwetu ni fursa kubwa ambayo inatumika majumbaji, kwenye magari, viwandani na pia ni nishati muhiimu viwandani uwepo wa nishati hiyo umeongeza fursa nyingi za uwekezaji mkoani hapa nafasi tunazo na tunakaribisha wawekezaji wengi zaidi mkoa huu ni kitovu cha uwekezaji naimani mtatembea na mtajione" amesema Munkunda
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mwanaasha Khamis Juma amesema kuwa wamefika mkoani hapa kujifunza katika sekta ya mafuta na gesi asilia.
"Tumekuja kujifunza kwenye miundombinu ya gesi asilia na sisi kwa sasa tunayo mamlaka inayosimamia gesi asilia tumefurahishwa na tumeona miundombinu ya kuzalisha na kuchakata gesi sisi kama wawakilishi wa wananchi tunaenda kuishauri serikali ili sekta ya gesi iweze kuwa chanzo kizuri cha mapato"
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mkondo wa Juu Pura Mussa Ryoba Itumbo (Mjioligia) amesema kuwa ziara hii Ina lengo la kubadilishana uzoefu na Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutiji wa Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia Zanzibar-ZPRA ili kujifunza kujifunza zaidi.
“Ziara hii ina lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu kwa pande zote mbili ambapo Tanzania bara tayari gesi ipo na tunauzoefu wakati Zanzibar wako kwenye utafiti ambapo tayari baadhi ya vitaru vimeshatangazwa kwaajili ya utafiti” amesema Itumbo
“Mpaka sasa tunayo gesi zaiidi ya futi za ujazo 57 jitihada kubwa zinafanywa na serikali ili kuhakikisha kuwa gesi iliyopo kwenye kina kirefu chini ya bahari inafikiwa na kuanza kutumika kwkauwa ndio eneo pekee lenye kiwango kikubwa cha gesi asilia” amesema Itumbo
Mkurugenzi wa Mwendeshaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Utafutiji wa Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia Zanzibar Adam Abdulla Makame amesema kuwa kwa sasa wamejipanga kuboresha sheria kwa upande wa mafuta na gesi asilia pamoja na mikataba ya utafutaji wa mafuta na gesi asilia ili kuhakikisha kuwa wanavutia wawekezaji.
“Tumeshaanza kutangaza baadhi ya vitalu ambapo mapkaa sasa kimoja cha pemba mnazi tayari kina mwekezaji na vingine jitihada kubwa zinafanyika ili kuweza kuwapata na kuanza utafuti wa mafuta na gesi asili” amesema Makame.
Nae Yusuph Hassan Idd(Masharubu) mwakilishi wa jimbo la Fuoni ambaye ni mjumbe wa kamati ya bajeti amesema kuwa wamekuja kutembelea mahali ambapo gesi asilia inazalishwa na kuchakatwa ili kuona shughuli mbalimbali zinazofanyika katika matumizi ya gesi asilia ambayo kwa kiasi kikubwa yanananyua uchumi wa taifa.
Kikubwa kilichonifurahisha ni kuwa gesi asilia inatumika kwa wingi mtwara hizi ni fursa kuwa ambazo na sisi Zanzibar tunatamani kuwa nazo ili tuweze kutumia kama umeme na pia kwenye magari, viwandani”
nae Rukia Omary Ramadhan Mwakilishi wa Jimbo la Amani Zanzibar amesema kuwa gesi asilia tunaiona ina faida kubwa na pia ina kuza uchumi pamoja na kupunguza gharama nyingi ikiwemo za kupika kwa wanawake ambapo itapugnuza matumizi ya mafuta kwenye magari.
“Serikali imefanyakazi kubwa niipongeze tumekuja kujifunza lakiani pia sasa tumefungua milango ya wawekezaji kwaajili ya uchimbaji wa gesi asilia kwakeli naona mafuta na gesi asilia ni fursa nzuri tukiwa na uchumi wa juu itatusaidia na kutunyanyua kiuchumi kama nchi” amesema Ramadhan
MWISHO
Comments
Post a Comment