Na Mwandishi wetu, Mtwara@@@@
Kamati ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC) imelipongeza shirika la umeme Tanzania –TANESCO kwakuwa wabunifu ili kuweza kuondoa changamoto ya umeme kukatika mara kwa mara kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Baada ya ziara ya Rais kumalizika Septemba mwaka Jana shirika hilo lilichukua hatua za dharula kuleta mtambo wa kuzalisha megawati 20 mkoani hapa ukitokea ubungo ili kuweza kumaliza tatizo la umeme kukatika mara Kwa mara.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya (PIC) Mh. Deus Sangu amesema kuwa mtambo huo unaenda kuondoa tatizo la umeme kwa mikoa ya Lindi na Mtwara.
Amesema kuwa mradi huo unauwezo wa kuzalisha megawati 20 ambapo mitambo ya zamani ikiwa na uwezo wa kuzalisha megawati 21.
“Mradi huu umetekelezwa na Kampuni ya kizalendo ambayo imefanyakazi nzuri na kwa wakati ambapo walitakiwa kikabidhi Machi 30 lakini sassa wameanza majaribio ni vema wakandarasi wengine wakaiga uzalendo huu Mradi huu unaenda kuleta mapinduzi makubwa” amesema Mh. Sangu
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo-hanga amesema kuwa mtambo huo umekuja kuongeza nguvu.
Amesema kuwa kuongezeka kwa megawati kunaongeza ufanisi zaidi wa kazi katika shirika lakini pia litaboresha maisha ya watu kwakuwa na umeme wa uhakika hivyo kuongeza ufanisi zaidi.
Aidha amesema kuwa serikali imejipanga ili kuhakikisha kuwa suala hilo lina malizika kwakuunganisha mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye grid ya taifa hadi kufikia 2026
“Kuanzia mwezi huu tatizo la kukatika umeme kwa mikoa ya Lindi na Mtwara litakuwa limeisha ambapo huduma ya umeme itakuwepo bila kuwa na changamoto yoyote” amesema Nyamo-hanga
Nae Francis Ndulane Mjumbe wa Kamati ya PIC na Mbunge wa Kilwa Kaskazini amefurahia uharaka wa ufungaji wa mtambo huo ndani ya miezi mitatu ili kiweza kumaliza tatizo la umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
"Ni kweli tumekuwa na changamoto kubwa ya umeme kukatika mara kwa mara ambapo tunaamini kuwa ujio wa mtandao huo utatupa nafasi ya kuendelea na shughuli zingine za kimaendeleo ndio maana Rais Samia Suluhu alipofanya ziara yake katika mikoa hii nilipata nafasi ya kuzungumza nilimwambia juu ya adha tunayokutana nayo kutokana na kutokuwa na umeme wa uhakika" amesema Ndulane
MWISHO
Comments
Post a Comment