NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
INGAWA kwa karne moja iliyopita, suala la wanaume
kuhimizwa kuwasindikiza wenzao wao kliniki, halikuwa likisikika, na inawezekana
ni kwa sababu ya afya zilivyokuwa za wajawazito hao.
Maana
tunaelezwa na kusifiwa kuwa, wajawazito wa enzi hizo za mababu na mabibi,
walikuwa ‘fiti’ afya zao, hali iliyopelekea, hata siku moja kabla ya
kujifungua, alikuwa anakwenda shambani kulima.
Na
ukweli unabakia pale pale kuwa, hata kwa wakati huo vyakula vyenye siha, rutba,
damu na kuongeza nguvu kwa wajawazito, vilikuwa bwerere.
Kwa
miaka hii ya sasa, afya za wajawazito walio wengi na hasa ikiwemo ukosefu wa damu,
ndio habari ya mjini, na ndio maana sasa wanaume wakatakiwa wawasindikize
wenzao wao, kliniki.
Tena,
kwani ni kila siku, hapana walau kwa wiki ya kwanza ya kuripoti kliniki, ili
sasa zile changamoto anazokabiliana nazo, na yule mwenza apate kuzijua, ingawa
wapo waliowasugu.
Hapa
wacha niwaulize wale wasugu wa kusindikiza wenzao wao, hilo kwao ni zito, au
wanasubiri hadi itungwe sheria na kanuni ndio watekeleze?
Mbona
ni jambo jema, wanalohimiza wataalamu wa afya, tena bahati nzuri, mwanamme anaemsindikiza
mwenza wake, hata kwenye msusuru yeye hakai.
Hili
je ni dogo, sasa hapa wewe mwanamme unakwamishwa na nini, hata ushindwe
kumsindikiza mwenza wako kliniki?
Naendelea
kusema kuwa, wataalamu wanavyowapenda wanaume, huwataka kufanya hivyo kwa walau
siku moja tu, tena pale tu mwanamke anapojigundua na ujauzito, sasa wapi wanakwama?
Au
ndio wanaume hawa ili kuwasindikiza wenzao wao wanasubiri wizara ya Afya itunge
kanuni, sheria na sera juu ya jambo hili?
Mbona
kama vile ni jambo la kawaida, na pia ndio kunogesha upendo wenu, na hasa ikizingatiwa
kuwa, kilichomo tumboni ni mali yenu pamoja.
Kwani
unadhani ukifika huko kliniki kuna jambo kubwa, hapana ni kuelezwa maendeleo ya
mtoto wenu mtarajiwa, kazi zipi afanye mjamzito huyo, chakula gani atumie na
namna ya kuishi nae kwa kipindi cha ujauzito wake.
Kama
ulionesha mahaba, mapenzi, utulivu, upendo na masikilizano wakati wa kuitafuta
mimba hiyo, sasa iweje ushindwe kumsindikiza kliniki?
Si
dhani kuwa jambo hilo, lazima wanaume wasubiri utungwaji wa sheria na kanuni, eti
ndio sasa hapo waanze kuwasindikiza wenzao wao kliniki.
Hivyo
wewe mwanamme, husijiskii faraja na furaha unapomsindikiza mwenza wako kliniki,
na kisha mtaalamu wa afya ya uzazi, akakwambia kuwa mtoto wenu uko na afya
nzuri.
Au
hupati furaha, mtaalamu huyo akakuelezea njia na namna bora ya kumuendeo mwenza
wako huyo, hasa kipindi cha ujauzito wake.
Maana,
haya na mengine, ndio maendeleo yanayotolewa huko kiliniki, ambako wewe
unasubiri hadi utungiwe sheria, pengine ndio utekeleze.
Kwa
hakika haipendezi, kuona kila siku mwanamke anaharibu ujauzito wake, na pengine
sababu ikiwa ni utendaji wa kazi kupitiliza, ukosefu wa damu au kuendewa
kinyama na mwenza wake, ikiwemo kulaliwa tumboni.
Yote
kwa yote, wanaume ambao hamjaamka, msisubiri kutungwa na sheria wala sera, ya
kuwataka kuwasikindikiza wenza wenu kliniki, bali sasa iwe ndio utamaduni wa
lazima.
Wajawazito
endeleeni kuwapa darsa wenza wenu, waliowapa ujauzito kuhakikisha wanaambatana
na nyinyi hadi kliniki, ili wajue maendeleo ya mtoto wenu mtarajiwa.
Viongozi
wa dini na asasi za kirai kama vile TAMWA, TGNP endeleeni kuwaelimisha wanaume,
kuwa mimba ni ya jamii, ila mtoto amehifadhiwa na mtu mmoja tumboni mwake.
Mwisho
Comments
Post a Comment