HABIBA ZARALI KU@@@PEMBA
NISHATI ya umeme imekuwa ni mkombozi kwa wakulima kwani kunawawezesha kulima kilimo cha uhakika wakati wowote na aina yoyote.
Kauli hiyo ilitolewa na mkulima wa mbogamboga na matunda Mohamed Abdalla Khamis huko Vitongoji Makaani Wilaya ya Chake Chake alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi.
Mkulima huyo mwenye shamba lenye ukubwa wa ekari saba alisema kabla ya kupata nishati ya umeme aliyopelekewa kupitia juhudi za mradi wa Swil alikuwa hana uhakika wa kilimo chake licha ya kwamba alikitegemea kwa ajili ya kujiongezea kipato.
Alielekeza kuwa kupitia mradi huo ameweza kupiga hatuwa moja kwenda nyengine kutokana na uhakika wa kilimo kwa vile umeme utamsaidia kuweza kupata maji ya kumwagilia katika mashamba yake.
Alifahamisha wananchi wengi wamejikita katika kilimo hususan cha mbogamboga lakini wamekuwa wakikata tamaa kutokana na kukosekana kwa huduma ya umeme ambayo huwakosesha fursa ya kupata maji kwa ajili ya kumwagilia mà hamba.
"Kilimo bila maji ya uhakika ni kubahatisha na maji ya uhakika huwezi kuyapata bila ya umeme kwa maana hiyo basi mimi sasa nna uhakika wa kilimo changu Kwa vile tayari umeme nimeshapata", alisema.
Akizungumza suala la soko mkulima huyo alisema soko la ndani la mbogamboga kwa sasaivi inaonekana kukuwa lakini ingawaje kunahitajika mbinu mbadala ya kuweza kusarifu mboga hizo na kuweza kuziuza katika soko la nje.
Kuhusu changamoto inayowakabili kipindi kirefu sasa ni kuwepo kwa joto ambalo linasababisha baadhi ya mboga mboga kutokuzaa na nyengine kufa kabisa pamoja na mabwana shamba kutowatembelea wakulima Kwa muda mrefu jambo ambalo ni tatizo.
"Kama izi tungule kipindi cha nyuma hazitoi kutokana na juwa kali , migomba nayo haizai sasa tazama huku ikiwa huna umeme ambao utaweza kupata maji ya uhakika unadhani kilimo kitaimarika apo",alisema.
Alifahamisha kuwa maji kupitia Mamlaka ya maji ZAWA hayawezi kutosheleza Kwa umwagiliaji asipokuwa wamwagilie kutoka katika visima ambapo bila ya umeme huwezi kufanikisha.
Nae mkulima Hamad Smail Faki alisema ni jambo moja la faraja kuona mradi wa swil kupitia TAMWA na PEGAO umelipigia mbio suala la umeme na hadi sasa wakaweza kupata.
Alisema anaamini kuwepo kwa umeme huo ni chachu ya kuleta mabadiliko ya kilimo kwani watazalisha na kupata kipato na hatimae kuondokana na umaskini .
"Tulikuwa tuna kilio Kwa muda mrefu lakini sasa kimenyamazika tunaahidi kufanya vizuri kama lengo lililokusudiwa,alisema.
Nae Salma Ali mwalimu ambae anajishughulisha na kilimo hicho alisema baada ya kupata maji kupitia umeme huo tayari ameshapanda mbogamboga ikiwemo michicha, mitungule na hata matunda yanayoingiza damu kwa maarufu mikarakadee.
Ujasiri wa kupanda mbogamboga umekuja baada ya huu umeme tulioupata kupitia mradi wa swil maana mashamba tulikushayaacha hayo kwa vile ata tukilima hamna faida mimea hufa",alisema.
"Pamoja na umeme huo kuwasaidia wakulima hata sisi ambao tunajishugjulisha na biashara pia ni mkombozi wetu alisema Khamis Shaame Makame na Juma Khamis Mwalim.
Alielekeza kuwa wake zao majumbani sasa wanaweza kutengeneza malai wakauza na kujipatia kijipato cha kujiendeshea na kuepuka utegemezi mkubwa .
"Awa wanawake wanahitaji kuwa na shughuli japo ndogo ndogo za kufanya wakajiingizia kipato sio kukaa tu na kusubiria kuletewa lakini wakati mwengine ndo wanarudi nyuma Kwa kukosa nyenzo muhimu ila sasaivi kwa kweli tumefarijika kupata umeme tumekomboka",alisema.
Hivyo waliyaomba mashirika na taasisi mbalimbali kuiga mfano huo wa Tamwa na Pegao wa kusaidia jamii katika masuala ya kujiletea kipato na kuondokana na dhiki katika maisha yao.
MWISHO
Comments
Post a Comment