NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MEYA wa jiji la Chake
chake Hamad Abdalla Hamad, amevitaka vilabu vyingine vya mazoezi kisiwani
Pemba, kuiga mfano unaofanywa na wenzao wa ‘Gombani Fitness club’ kwa kule kuwa
karibu na jamii.
Hayo aliyasema leo Machi 30, 2024
mara baada ya kumalizika kwa futari, iliyoandaliwa na klabu hiyo, iliyojumuisha
wawakilishi wa vikundi vya mazoezi vya Pemba, watoto mayatima na waumini wengine
na dini ya kiislamu na kufanyika ukumbi wa ZRA Gombani.
Alisema, Gombani Fitness Club,
imekuwa karibu mno na jamii, kwa kule kujumuika katika shughuli za umma kama za
usafi, uchangiaji damu na futari ya kila mwaka.
Alieleza kuwa, klabu hiyo haipo tu
kwa ajili yakufanya mazoezi pekee, kama vilivyo vilabu vyingine, bali wanakwenda
mbali zaidi, kwa kuwa karibu na jamii kivitendo.
‘’Mfano huu wa futari mlioiandaa,
kuchangia kwenu damu kwenye shughuli mbali mbali za umma, kushiriki usafi ni
mambo ya kuigwa na vilabu vyingine,’’alieleza.
Aidha alieleza kuwa, ibada
walioifanya ya kufutarisha watu wa mkaundi mbali mbali wakiwemo mayatimu na
watu wenye kipato cha chini, wamejikusanyia fadhila kubwa, mbele ya Muumba.
‘’Muumba wetu ameshatuahidi malipo
makubwa kwa mtu anayemfutarisha mwenzake hata kwa tone la maji au kukokwa moja
ya tende, na utamaduni huu uendelee,’’alifafanua.
Katika hatua nyingine, Meya huyo wa
jiji la Chake chake Hamad Abdalla Hamad, alisema mazoezi bado yatendelea kuwa
ndio ngao kubwa kwa afya bora ya mwanadamu, hivyo kila mmoja anaowajibu huo.
Mapema Makamu Mwenyekiti wa Gombani
Fitness Club Hamad Ali Malengo, alisema klabu yao, itaendelea na utamaduni huo
kila mwaka, ili kuyakushanya makundi mbali mbali, kweye futari kama hiyo.
‘’Tunaahidi kuwa, sisi Gombani
Fitness Club, kila mwaka utamaduni huu tutauendeleza, na tutaendelea kuchukua
watu wa makundi mbali mbali, ili
kujumuika nao,’’alieleza.
Katibu wa klabu hiyo Khalfan Amour Mohamed,
alisema futari ya mwaka huu walioandaa, imetanua wigo kwa kuvishirikisha vilabu
vyote vikuu vya mazoezi vya wilaya nne za Pemba.
Alieleza kuwa, waliamua kufanya
hivyo, ili kuongeza urafiki, umoja na mshikamani baina yao na vilabu vyingine
vya mazozi kisiwani humo.
‘’Ndio maana hata mara hii, futari
yetu imechukua watoto mayatima, viongozi wa dini, watu wenye kipato cha chini,
wanachama wetu na wanachama wa vilabu vyingine hapa kisiwani Pemba,’’alieleza.
Miongoni mwa waalikwa wengine ni
Afisa Mdhami wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Pemba, Afisa Mdhamini wizara ya
Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, viongozi wa dini, watu maarufu, waandishi
wa habari, watu wenye mahitaji maalum na mayatima.
Mwisho
Comments
Post a Comment