HABIBA ZARALI, KU-@@@PEMBA
AKINA mama wa madarasa ya kisomo cha watu wazima mjini Kiuyu shehia ya Minungwini wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba wameushukuru mradi wa kumjenga mwanamke katika nafasi za uongozi (Swil) kwa kuwapatia madarasa ya kisomo cha elimu ya watu wazima ambayo yamewawezesha kujuwa kusoma na kuandika.
Walisema mradi huo kwa sasa umekuwa msaada mkubwa kwao huku wakiwa tayari wamedhamiria kuingia katika harakati za uongozi na kugombea nafasi yeyote kwa kujiamini muda utakapofika.
Mmoja kati ya mama hao Ruwaila Ali Haji (26) ambae aliishia darasa la nne katika skuli ya kwake alisema baada ya kujiunga na darasa hilo Kwa muda wa miaka minne sasa ana uwezo wa kusoma na kuandika.
Alifahamisha kuwa hana sababu ya kutogombania nafasi japo kwa ngazi ya shehia kwa vile moja ya sifa za kuomba uongozi ni kujuwa kusoma na kuandika jambo ambalo Kwa Sasa analimudu.
"Sasa najiamini kugombea nafasi yoyote Kwa sababu sifa nnayo najuwa kusoma na kuandika tena kwa ufasaha"alisema.
Alieleza kwa vile anajuwa kusoma na kuandika yuko mstari wa mbele kuwasomesha watoto wake wanaporudi skuli jambo ambalo linawafanya watoto hao kuwa na hamu ya kuendelea na masomo yao kila siku.
"Kusema kweli mradi huu wa swil kupitia chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA na PEGAO wametuokowa sisi wanawake baada ya bidii zao za kutuwekea hili darasa na likatuwezesha tukajuwa kusoma na kuandika"alisema.
Nae Viwe Yussuf Makame (70) alisema kabla ya kujiunga na darasa hilo hakujuwa kusoma wala kuandika lakini kwa sasa ana uwezo wa kumfundisha majukumu wake kusoma masomo ya skuli.
Alisema mradi wa swil umemkomboa na kumuondowa katika hali ya unyonge hasa kwa wakati huu ambapo usipojuwa kusoma na kuandika unaweza kukosa hata haki zako za msingi katika maisha.
"Nawasihi wanawake wenzangu kujiunga na madarasa ya watu wazima hata kama ni wazee kwani mimi kwa umri wangu huu na nimeweza ",alisema.
Asha Omar Issa (35) anajiskia faraja baada ya kujuwa kusoma na kuandika kwani anaweza kusoma ujumbe wa maandishi iwe kwenye karatasi na hata anapotumiwa kupitia simu yake.
"Hata kanga nasoma bila wasi na nikitembea najuwa km hapa pameandikwa hatari au usipite "alisema.
Kwa upande wake mwalimu wa darasa hilo Maryam Juma Hamad aliiomba wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar kuwapatia posho la waalimu wa madarasa ya wanakisomo hao kwa wakati ili waweze kujikimu na Maisha.
Alisema tokea kuanzia darasa hilo miaka minne ilopita tayari ameshawanfundisha wanafunzi 50 ambao alianza nao wakiwa hawajui hata kidogo.
Mratibu wa Tamwa Zanzibar ofisi ya Pemba Fat-hiya Mussa Said alisema mradi huo darasa hilo lilianzishwa baada ya mradi kugunduwa changamoto ya akina mama kutojuwa kusoma na kuandika.
Alisema kujuwa kusoma na kuandika Kwa akina mama na ni jambo la kufurahisha na kutoa tama akubwa ya kuthubutu kuona akina mama hao wanajuwa kuandika na kusoma.
"Kwa Sasa hatuwa inaridhisha kwani walianza wakiwa hawajui chochote na sasa wako vizuri"alisema.
Wakitowa michango yao wanafunzi hao wamewaomba wadau na taasisi mbali mbali kuendelea kuwawezesha kwa kuwapatia miradi itakawasaidia kujipatia kipato na kuwaongezea hamasa katika kusoma.
Hata hivyo Darasa hilo la kisomo linakabiliwa na ukosefu wa ubao wa kufundishia , pamoja na kutokuingizwa kwenye mfumo wa madarasa ya serikali ya elimu mbadala licha ya kuwa na mashirikiano mazuri na wizara hiyo.
Darasa hilo likiloanzishwa kupitia mradi wa swil kwa sasa lina jumla ya wanafunzi 20 , limefanikiwa kuleta mabadiliko kwa akina mama zaidi ya 50 ambao awali hawakujua kusoma wala kuandika ambapo lotawarahisishia katika shughuli zao na kutimiza malengo yao ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Mwisho.
Darasa hilo likiloanzishwa kupitia mradi wa swil kwa sasa lina jumla ya wanafunzi 20 , limefanikiwa kuleta mabadiliko kwa akina mama zaidi ya 50 ambao awali hawakujua kusoma wala kuandika ambapo lotawarahisishia katika shughuli zao na kutimiza malengo yao ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Mwisho.
Comments
Post a Comment