Mkurugenzi Idara ya
Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Makundi Maalumu(SMT) ndugu Badru Abdulnuru amewataka wajasiriamali wanawake
kutumia vyema fursa ya mikopo ili kuendelea biashara zao.
Akizungumza wakati
alipofungua mafunzo kwa wajasiriamali hao juu ya namna ya kuomba mikopo isiyo
na riba katika Benki
ya CRDB, yaliyofanyika jana katika
ukumnbi wa Sebleni kwa wazee ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha siku ya
wanawake duniani, ndugu badru amesema
kufanya hivyo kutawasaidia kuweza kujikwamua na utegemezi.
Amewataka wanawake hao kutambua kuwa katika mikopo hio ya CRDB Serikali nayo imechangia kwa kiasi
kikubwa ili kuwasaidia wanawake kuwainua kiuchumi. Pia amewataka kuwa na nidhamu ya fedha
wanazikopa kwa kufanya jambo walilolikusudia ili waweze kurejesha mikopo hiyo
na kuwasaidia wengine.
Aidha
amewashauri
kuyatumia majukwaa ya uwezeshaji kiuchumi ili kuweza kuwakutanisha na wajasiriamali wengine Pamoja na kutanua wigo wa
kibishara.
Wakati huo huo,
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto kutoka Wizara ya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto (SMZ)
bi
Siti Abass Ali amesema Wanawake
nchini wametakiwa kujitathmini na kujitambua katika kupambana katika kujiletea
maendeleo wenyewe.
Mkurugenzi Siti ameyasema
hayo, wakati alipofungua mafunzo ya wajasiriamali kwa wanawake wa wilaya
mbalimbali za Unguja,
ikiiwa ni shamrashamra za kuadhimisha siku ya wanawake duniani Machi,08.
Amesema wanapoadhimisha
siku ya wanawake duniani kila mwaka nilazima wanawake kujitathmini katika mwaka
mzima ni kitu gani wamefanya katika kujiletea maendeleo na endapo kuna tatizo
ni vyema kulitatua ili kusonga mbele kimaisha.
Amesema Wizara imeamua
kufanya mafunzo kwa wajasiriamali wanawake, ikiwa lengo ni kuwaunganisha pamoja wanawake na kupeana moyo
katika maendeleo, pamoja na kupeana nguvu kwa
kugombania nafasi mbalimbali za uongozi ili kuweza kuwa mbele
kimaendeleo.
Kwa upende wao baadhi ya
wajasiriamali hao, wameishukuru Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto kwa kuweza kuwapatia elimu hiyo ambapo wameomba kusaidiwa katika
kupunguziwa masharti ya upatikanaji wa mikopo ili nao waweze kunufaika.
Pia wamewaomba wafadhili
wanapotoa misaada mbalimbali kwa wajasiriamali kufika vijijini kwani wamedai
kuwa fursa hizo wamekuwa wakizikosa ukilinganisha na watu wanaoishi mjini.
Mafunzo hayo ya siku
mbili kwa wajasiriamali wanawake
yamefanyika katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkoa wa Kaskazini, na Mkoa
wa Kusini, ambapo maada mbalimbali ziimewasilishwa ikiwemo matumizi sahihi ya
fedha, nafasi za uongozi kwa wanwake na nyenginezo.
MWISHO
Comments
Post a Comment