Na Nafda Hindi, Zanzibar@@@@
Ikiwa dunia
inaadhimisha siku ya wanawake, ambayo husherehekewa kila mwaka ifikapo tarehe
08 March yenye mnasaba ya kuonesha mafanikio ya kijamii, kiuchumi, kiutamaduni
na kisiasa huku ikitetea usawa wa kijinsia.
Katika siku hii ya wanawake, ikiwa na kauli mbiu ya mwaka
huu “Wekeza kwa wanawake, harakisha maendeleo”.
Kwa muktadha huo
ikiwa na maana pana kuwekeza nguvu kwa mwanamke kunaharakisha maendeleo kwa mtu
mmoja mmoja na Taifa kwa Ujumla, na kwa kukazia kauli hiyo, hata Viongozi wa
dini ya Kiislam katika hadithi za Mtume Muhammad (S W) inasema “Ukifundisha
mwanamke mmoja ni sawa na kufundisha wanawake kumi.
Kufuatia siku hii hiyo adhimu kwa wanawake TAMWA, ZANZIBAR
hawako nyuma katika kuhakikisha wanatumia nafasi hiyo ili kumkombowa mwanamke
kiuchumi kwa kuwa na uwezo wa kujitegemea na kutunza familia.
Kupitia MRADI wa VIUNGO wenye lengo la kuwainuwa wanawake
kiuchumi TAMWA, ZANZIBAR walifanya ziara ya siku moja kutembelea wanufaika wa
mradi huo wakiambatana na Ugeni kutoka Shirika la Kimataifa linalojishughulisha
na masuala ya ardhi (LANDESA) na kuona harakati mbali mbali zinazofanywa na
wanawake wa Zanzibar kwa lengo la kujikwamuwa kiuchumi.
Aviwe Songoro ni (40) mkaazi wa Kizimbani, Mkoa wa Mjini
Magharibi Unguja ni mmoja kati ya
wanufaika wa mradi huo anasema kupitia kilimo amesomesha watoto wake watatu, ngazi ya Shahada ya kwanza na tayari
wameajiriwa Serikalini, wawili Wizara ya Afya na mmoja Wizara ya Kilimo ambapo
kwa sasa mama huyo anamiliki nyumba ya kuishi ya kudumu.
“Watoto wangu wanakula, wanavaa na nawalipia ada ya school
na madrasa kupitia shughuli zangu za
kilimo,” Aviwe Songoro.
Nae Mwanashamba Ahmed (42) Mkaazi wa Kizimbzni ni mkulima anaejishughuliha na kilimo cha Vanila, Hiliki, Pili pili Manga, Karafuu, Shoki Shoki na Doriani amesema ameanza kupata mafanikio kama vile kusomesha watoto watatu ngazi ya Shahada ya kwanza, wawili wamesoma fani ya Madawa(Phamacy) ambapo mmoja tayari muajiriwa wa Serikali na mmoja amesomea Shahada ya kwanza ya Uhandisi.
“Mimi nina watoto (4) mama mimi na baba ni mimi mwenyewe
(Single Mother) nawalisha, nawasomesha
na mahitaji yote ya msingi wanategemea kutoka kwangu na ninawahudumia kupitia
harakati zangu za kilimo,” Mwashamba.
Nae Rehema John (43) Mkaazi wa Kijichi Unguja, Wilaya ya
Magharibi “A” anaelima Viungo mbali mbali kama vile Vanila, Karafuu, Hiliki na Mdalasini
amesema amejenga nyumba ya kuishi ya
kisasa ikiwa na miundo mbinu ya maji na umeme, na anazalisha mafuta mazuri
(perfume) yenye harufu ya mdalasini, mlangi langi na karafuu na kuingiza kipato
kinachomsaidia kujikimu pamoja na familia.
Kikundi cha Vanila Growing Group kutoka Donge, Mkoa wa
kaskazini Unguja kinachojishugulisha na kilimo cha viungo (spice) wameweza
kubadilisha mitazamo ya baadhi ya wanaume na jamii kuona kwamba mwanamke hawezi
kujishughlisha na kuafanya kazi ya kujiingizia kipato.
“Mwanamke ana haki sawa kama mwanamme kupata elimu, kufanya
kazi na kujiingizia kipato ila kuna baadhi ya wanaume wana mawazo mgando ya
kuwabana wake zao na watoto wa kike kutokufanya kazi, hilo si jambo jema lazima
tubadilike,” Mwanaushirika.
Mratibu wa Mradi wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha
na masuala ya Ardhi (LANDESA) Susan Waruhiu amesema ipo haja kwa wanawake na
watoto wa kike kujiamini katika kutekeleza majukumu yao ili kutimiza ndoto za
maisha yao.
“ Wanawake ni watu wenye akili watakapojiheshimu na kuiamini
watafika mbali katika kutimiza malengo yao, hivyo wasikubali kuwekwa nyuma,”
Susan Afisa Landesa.
Mapema Mkurugenzi Muhamasishaji kutoka Shirika la Kimatifa
linalojishughulisha na masuala ya Ardhi Barani Afrika (LANDESA) Dk Monica Mhoja amesema wanawake waweke mbele
Zaidi vipau mbele vyao kama vile kujifunza, kujiheshimu na kujiamini kwa lengo
la kuleta maendeleo na kutokubali kukatishwa tamaa.
Aidha Afisa kutoka LANDESA Kylie Palzer amewasisitiza
wanawake kuchangamkia fursa na kupambania kugombea nafasi mbali mbali za
Uongozi kuanzia ngazi ya familia, jimbo na hata Taifa.
Afisa Mkuu wa Zone, MRADI wa VIUNGO kutoka TAMWA, Zanzibar
Sabrina Mwintanga amesema wanatoa mafunzo mbali mbali ya kuwajengea uwezo
wanawake pamoja na vijana kujiekeza katika sekta ya kilimo iliodharauliwa kwa
muda mrefu kwa lengo la kulima kilimo cha biashara badala ya chakula pekee na
kujipatia kipato.
Ziara hiyo ya Siku
moja iliyoratibiwa na TAMWA, Zanzibar kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa
linalojishughulisha na masuala ya ardhi (LANDESA) iliwatembelea wanufaika wa
MRADI wa VIUNGO kutoka maeneo mbali mbali ya Zanzibar.
MWISHO
Comments
Post a Comment