NA ASHA ABDALLA, PEMBA @@@@
SERIKALI ya Mapindunduzi ya Zanzibar ya awamu ya nane chini ya uongozi wa Dk.Hussein Ali Mwinyi, inaendelea kufanya harakati kwa makundi mbalimbali katika kuhakikisha kila mzanzibar anapata haki zote za msingi bila ubaguzi wa rangi, silka na itikadi yake .
Ameyasema hayo Mkuu wa wilaya ya Mkowni Khatibu Juma Mjaja kwaniaba ya Mkuu wa Mkowa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Masoud, wakati alipokua akigawa vifaa maalumu vya watu wenye uUlemavu wa ngozi kutoka katika mradi wa ZAHO huko ukumbi wa Manis[paa ya Mji Chake chake Pemba Machi 9, 2024.
Amesema kuwa serekali inaweza kuwawezesha zaidi watu wenyeulimavu wa ngozi kwa miundombinu mbalimbali kwakupatiwa elimu ,afya bora na hata kupatiwa mikopo ambayo itaweza kuwasaidia katika kufanya biashara ndogondogo nakuweza kujikwamua kimaisha.
"Niwaleze wazazi nawelezi kua nikosa kisheria kuwaficha watu wenye ulemavu au kumdalilisha kwani nawao ni watu kama watu wengine duniani."alifafanua
Hata hivyo aliahidi kushirikiana kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa kusini Pemba nao na kutoa wito kwa wazazi wote wajitahidi kuwapatia elimu watoto wenye ulemavu inayostahiki kwa sababu hao ndio taifa la baadae .
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu katika jumuiya ya watu wenye ulemavu wa ngozi ZAHO ambae nimiongoni mwa watu wenye ulemavu Mohamed Rashid Mohamed, alisema kua walemavu wangozi wanazo changamoto mbalimbali, ambazo wanakumbana nazo zikiwemo vifaa vya kutumia ,kudharauliwa na hata kutopata elimu yakutosha kwa watu hao.
Aidha alisema kuwa walemavu wa ngozi wanakabiliwa na ukosefu wa upatikanaji wa ajira wakati wanapomaliza kusoma kwani wanaonekana kama hawezi kushirikiana na watu katika kufanya kazi ya aina yoyote.
Hata hivyo aliomba serekali kupatiwa eneo lakaribu katika wilaya ya Chake chake ambalo litawawezesha kujengewa kituo maalumu cha afya cha watu wenye ulemavu wa ngozi ili waweze kupata huduma kwa wakati bila ya usumbufu wowote.
Nae mwakilishi wa baraza kuu lataifa la watu wenye ulemavu Zanzibar Ayoub Juma Shame alisema kuwa vifaa ambavyo vimetolewa nikwa ajili ya watu wenye ulemavu pekee na nikosa kutumia mtu mwengine kwani itakujapelekea kupata madhara.
Afisa wa watu wenye ulemavu katika wilaya ya Chake chake Mwadini Juma Ali alisema kuwa inapokuja kama hizi waweze kuzitumia vizuri kwani jumuiya ya watu wenye ulemavu wa ngozi wamekuja kwa kuwawezesha kimaendeleo zaidi.
Nae mzazi mwenye watoto wenye ulemavu Rashid Mohamed alisema kuwa wazazi wanatakiwa kuwa na ushirikiano mkubwa na watoto ili weweze kupata elimu na kuweza kujikwamua kimaisha .
Hatahivyo aliishukuru taasisi hiyo na viongozi mbalimbali kwakuweza kushirikiana katika kuwapatia misaada hii ambayo itaweza kuwasaidia watoto hao.
Vifaa hivo vikiwemo lotion, na kofifia vilitolewa na jumuiya mama Maryam Mwinyi foundation kwa ajili ya kuweza kuwasaidia watoto wenye ulemavu ili kuepukana na changamoto zinazijitokeza katika miili yao .
ReplyForward |
Comments
Post a Comment