NA NAFDA HINID, ZANZIBAR@@@@
Maafisa kilimo wameshauriwa kutoa taarifa kamili kuhusu udongo bora wenye kukidhi viwango kwa lengo la kuzalisha mazao bora kwa wakulima.
Kauli hjiyo imetolewa na Mkuu wa Tathmini na Ufatiliaji kutoka mradi wa VIUNGO Ali Abdalla Mbarouk katika kikao cha pamoja kilichowashirikisha wadau wa mradi huo chenye lengo la kujadili mbinu bora na mikakati imara ya kuendeleza kilimo chenye tija kwa wakulima kilichofanyika jengo la Benki ya watu wa Zanzibar katika Ofisi za Mfuko wa Bima .
Amesema ipo haja kwa Wizara ya Kilimo kufanya tathmini kwa wakulima kwa kila Wilaya kugunduwa changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka ikiwemo kutokufahamu udongo sahihi kwa matumizi bora ya kiliomo.
Mwenyekiti wa kamati ya Ushauri ya mradi wa Viungo (ZMAG) ambae pia ni Mkurugenzi Sera, Mipango na Kilimo Makame A. Makame amesema kwa sasa ipo haja kwa Zanzibar kuuza bidhaa zilizochakatwa nje ya nchi badala ya mali ghafi kwa lengo la kuongeza thamani ya mazao yanayotoka nchini
“Ni lazima kuandaa mipango mikakati itakayosaidia wakulima kupata mbinu bora za kumaliza changamoto zinazowakabili ili wazalishe kilimo bora na chenye tija,” Makame A. Makame . Mwenyekiti wa ZMAG.
Nae Mkurugenzi kutoka Umoja wa wakulima wa mboga mboga na matunda (UWAMWIMA) amesema kwa sasa Zanzibar inazalisha bidhaa za matunda bila ya kutegemea msimu ikiwemo bidhaa ya embe kutokana na wakulima kupata Elimu inayowafanya kubadilika na kuacha kulima kilimo cha mazoea,
Mkuu wa Mawasiliano kutoka Mradi wa VIUNGO Sophia Ngalapi amesema Mradi wa Viungo umekuja kuwakomboa wakulima hivyo kunahitajika mbinu Mbadala zitakazo wasaidia wakulima kusonga mbele katika kulima kilimo chenye tija na kubadili maisha yao,
Wakichangia katika kikao hicho wakulima wamesema pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kujenga masoko mbali mbali katika Visiwa hivyo kwa sasa wanahitaji soko la bidhaa za kilimo hai kujitegemea badala ya kuchanganywa na masoko mengine.
“Tunashkuru Serikali imejiandaa kujenga masoko mbali mbali Zanzibar lakini ipo haja kwa sasa kubaguwa soko maalum la bidhaa za kilimo hai na kutofautishwa na bidhaa nyengine”, Mkulima wa mboga mboga na matunda.
Mkutano huo wa nane wa kujadili masuala mbali mbali ya utekelezaji wa mradi na kushauri njia Mbadala ili kufikia malengo ya mradi wa VIUNGO Zanzibar unaotekelezwa na TAMWA ZNZ, Community Pemba Forest (SPF) na People Development Forum (PDF) ni mmradi wa miaka minne ambao uko chini ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Umwagiliaji Zanzibar unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya.
Comments
Post a Comment