Joyce Joliga, Songea::::
Songea. Watoto 398,029 sawa na asilimia 122.2.Mkoani Ruvuma wamepatiwa chanjo ya Polio ili kuwaepusha na ulemavu.
Katibu Tawala Msaidizi ,Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii Mkoani Ruvuma Dk.Lous Chomboko amesema Mkoa ulilenga kuchanja Watoto 325,746 katika awamu ya tatu ya kampeni dhidi ya chanjo ya polio iliyoanza Septemba mosi hadi Septemba nne 2022.
“Utekelezaji wa kampeni ya utoaji chanjo ya polio ya matone awamu ya tatu kwa Watoto chini ya miaka mitano umefanyika kwa mafanikio makubwa,mikakati yetu ni kuongeza wigo wa ufuatiliaji toka ngazi ya Mkoa hadi Halmashauri ili kudhibiti kabisa polio’’,alisisitiza Dk.Chomboko.
Amesema serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Shirika la Afya Ulimwenguni WHO lilitangaza uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa polio Februari 17,2022 katika jiji la Lilongwe nchini Malawi,hivyo Tanzania iliamua kufanya kampeni ya utoaji chanjo dhidi ya polio kwa Watoto chini ya miaka mitano ili kuudhibiti.
Mkoa wa Ruvuma ulikuwa kinara kitaifa katika utoaji chanjo ya polio kati ya mikoa minne ya awamu ya kwanza iliyotekeleza kampeni ya polio,mwaka 2021 kwa kufanikiwa kutoa chanjo ya polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano kwa asilimia 122
Kwa upande wao baadhi ya wazazi, Anastella Jarome na Amon Chiwanda wameishukuru Serikali kwa kutoa chanjo kwa Watoto wao kwani itawaepusha na ulemavu na pia wamewashauri wazazi ambao bado watoto wao hawajapata chanjo kuwapeleka waweze kupatiwa ili kuwaepusha na ulemavu kwani huduma hiyo ni bure.
Mgonjwa wa mwisho wa polio aligundulika nchini Tanzania katika Mkoa wa Mtwara mwaka 1996.
Mwisho
Comments
Post a Comment