Skip to main content

Posts

FIDEL CASTRO, WANANCHI WAPIGA MARUFUKU UZURURAJI HOLELA ENEO LA SKULI

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ UONGOZI wa skuli ya sekondari ya Fidel Castro, wananchi kijijini hapo, pamoja na uongozi wa shehia ya Wawi wilaya ya Chake chake, umekubaliana kupiga marufuku kuanzia sasa, kutoingia kwa mtu yeyote bila ya kazi ya halali, ndani ya eneo la skuli, ili kuepusha athari ambazo zimeanza kujitokeza. Wakizungumza kwenye kikao cha pamoja, kilichofanyika skulini hapo, walisema tayari athari kama za wizi wa vifaa vya wanafunzi, umeanza kujitokeza, hivyo wamekubaliana kuanzia sasa kupiga marufuku, uingiaji kiholela. Mwalimu mkuu wa skuli hiyo Seif Hamad, alisema ameridhishwa na uamuzi uliofikiwa na pande mbili hizo, kwani wamekuwa na hofu kubwa ya kutokezea vitendo vya udhalilishaji hapo baadae. Alieleza kuwa, uamuzi huo unaweza kusaidia sana kuondosha uingiaji holela ndani ya skuli hiyo, ambao kwa kiasi kikubwa, ulikuwa unaanza kutishia hata mali za skuli. ‘’Mimi nimeridhishwa na uamuzi ambao umefikiwa kati yetu, wazazi na uongozi wa shehia, kwamba sasa t...

DK. MWINYI AKIFUNGUA KISIWA CHA PEMBA KIUCHUMI, KIWANDA CHA MAJI CHA KWANZA HICHI HAPA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@   “Waswahili wanasema… ‘Pemba Peremba, ukienda na joho utarudi na kilemba’,.   Wengine wakasema kuwa, “waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba”. Haya ni baadhi ya misemo na misimu, ambayo wananchi wa kisiwa cha Pemba hupenda kuyatumia, kulingana na wakati na kwenye kitu kinachohimiza maendeleo. Karne zimepita, tangu misemo hiyo kutumika, licha ya kuendelea kutumiwa vijijini, kulingana na mazingira au kitu kilichopo. Katika miaka iliyopita, kulikuwa na baadhi ya watu waliweza kudiriki kusema kuwa, hakuna uwezekano wa Pemba, kuwa ya viwanda, licha ya maeneo huru ya uwekezaji kutengwa kwa miaka zaidi ya 20. Sasa ni miaka minne ya uongozi wa Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi, wananchi wa kisiwa cha Pemba wameanza kujivunia maajabu ya kimaendeleo. Tayari miradi ya kimkakati imeanza kuonekana ndani ya Kisiwa cha Pemba, kwa mabadiliko makubwa ya maendeleo, ndani ya kisiwa hicho. Ilikua ni Julai 27 mwaka 2022, jua tayari linaelelekea kuzama, Rais D...

'WEPO' YAZINDUA MRADI KUSAIDIA MAPAMBANO DHIDI YA UDHALILLISHAJI

  SALIM HAMAD, PEMBA@@@@ HAKIMU wa Mahkama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zuwena Mohamed Abdul-kadir amewataka wadau wa mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji, kuongeza kasi katika mapambano hayo, ili kuwakinga watoto wasiharibiwe, ambao ndio kundi kubwa linalokabiliwa na shida hizo. Kauli hiyo ya Hakim wa Mkoa, imetolewa kwaniaba yake na Hakimu wa Mahkama ya Mwanzo Wete Adam Abdalla Faki wakati akizungumza na Wadau wa Mambano ya Udhalilishaji, katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa uwezeshaji wa Kisheria na upatikanaji wa haki unaofadhiliwa na UNDP uliofanyika Baraza la Mji Wete. Alisema  katika kumaliza shidha hizo, wadau kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kusimama imara na kutoa ushirikiano katika kupiga vita vitendo hivyo visiendelee. ‘’Bado vitendo hivi vinaendelea kujitokeza pamoja na juhudi zote zinazochukulia lakini tunatakiwa kuwa wamoja na mashiriano kupiga vita vitendo hivyo,’’alisema . Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo kutoka Jumuia ya wasaidizi wa sheria Wete...

'CONNECTING CONTINENT' YAWAONESHA NJIA WAZAZI KUONGEZA UFAULU

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ UONGOZI wa skuli ya sekondari ya Connecting Continent iliyopo Mgogoni wilaya ya Chake chake, umesema kama wazazi na walezi wataongeza ushirikiano, kati yao na waalimu, uwezekano wa kuondoa daraja la nne na la tatu kwa kidato cha nne upo. Mwalimu mkuu skulini hapo, Mwache Juma Abdalla, alisema waalimu wanaosomesha skuli hiyo, wamekuwa na moyo mmoja wa kuondoa daraja la nne na la tatu kwa wanafunzi wa kidato cha nne, hasa kwa mitihani ya taifa. Alisema, hilo linaweza kuwa rahisi mno, ikiwa kuanzia sasa   wazazi na walezi, watajenga msingi madhubuti ya ushirikiano kati yao na waalimu, skulini hapo. Alieleza kuwa, wapo wazazi na walezi, hawapiti skulini hapo jambo ambalo linalowapa ukakasi waalimu na kuhisi wameachiwa majukumu peke yao ya ulezi. Mwalimu mkuu huyo, aliyasema hayo Julai 6, 20204 kwenye kikao cha kwanza kwa mwaka huu, cha kuwasilisha matokeo ya muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne. Alifahamis...

'MADEO' AIBAKISHA WAWI STAR MSIMU WA LIGI UJAO

NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ TIMU ya Wawi star, imejihakikishia kubakia ligi daraja la kwanza kanda ya Pemba msimu ujao, baada ya jana kuichakaza Azimio SC kwa mabao 3-2, kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Ngere ngere Jeshini, majira saa 10:30 jioni. Kwa timu ya Wawi star, mchezo huo kwao ulikuwa na maana pana, ili wajihakikishie kubakia kwenye daraja hilo, hasa kwa vile mchezo unaofuata wataumana na Junguni anayesaka alama za lazima za kuongoza ligi hiyo. Katika mchezo wa jana, ambao uliohudhuriwa na watazamaji wengi, ulianza kwa kasi, huku kila timu ikiangalia ulipo udhaifu wa mwenzake, ili aondoke na alama tatu muhimu. Katika kuhalalisho hilo, Wawi star ilianza kuwafurahisha washabiki wake, mnamo dakika ya 15, pale mshambuliaji wao hatari Suleiman Seif ‘Madeo’ alipotikisa nyavu kwa bao la kwanza. Lakini Azimio SC, kwa vile walishaazimia ushindi, walisawazisha bao hilo, mnamo dakika ya 34, kwa shuti la mbali lililopigwa na mlinzi wao Salum Kazumar, na kujaa wavuni. Ingawa ‘Ma...

TAMAA YA MAHARI, MKAJA WA WAZEE WAKATISHA NDOTO ZA WATOTO WA KIKE MFIKIWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAHARAKATI wa haki za watoto shehia ya Mfikiwa wilaya ya Chake chake, wamesema tamaa ya mahari na haki ya wazee (kilemba cha wazee), ni miongoni mwa sababu, zinazochangia watoto kukatishwa masomo kwa kuozwa waume mapema. Walisema, baadhi ya wazazi wamekuwa wakikimbilia haki ya wazee na mahari, wakati mtoto wake anapotokezea muume, na hivyo kumkatisha masomo kwa tamaa hiyo. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini hapo, walisema hiyo ni miongoni mwa sababu moja kubwa, ambayo sasa husababisha watoto, kukatishwa masomo. Mratibu wa wanawake na watoto shehiani humo Kheriyangu Mohamed Ali, alisema pamoja na elimu wanayoitoa, lakini bado wapo wazazi wamekuwa wazito kubadilika. Alieleza kuwa, na hasa pale inapotokezea kuna mtoto ni mtoro masomoni, ndipo hapo wazazi huchukua nafasi hiyo, kuwakatisha masomo. ‘’Hapa shehiani, wapo wazazi na walezi wamekuwa wakivutiwa mno na yale mahari na fedha za wazazi (kilemba cha wazee), hivyo huwa rahisi...

RIPOTI: WAANDISHI WA HABARI ZA MAZINGIRA NA HALI YA HEWA WAKABILIWA NA UKOSEFU RASILIMALI NA VITISHO

    Ripoti ya hivi karibuni ya Internews, iliyofanywa kupitia mpango wake wa Uandishi wa Habari za mazingira kupitia shirika lake la Earth Journalism, imetoa tathmini ya kina kuhusu hali ya uandishi wa habari za hali ya hewa na  mazingira duniani . Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi chache zilizojumuishwa katika utafiti huu wa kimataifa, ikitoa maarifa muhimu kuhusu mitazamo na uzoefu wa waandishi wa habari katika eneo hilo. Matokeo yanaonyesha kuwa kwa Tanzania nan chi nyingine uandishi wa habari za mabadiliko ya hali ya hewa na masuala ya mazingira umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Kuongezeka kwa habari hizi kunahusishwa hasa na matatizo ya mazingira yanayozidi kuongezeka na, kwa kiwango kidogo, kuongezeka kwa hamu ya jamii kufhamu kuhusu masuala haya muhimu ya mazingira. Ripoti hiyo inaonyesha kwamba Asilimia 82 ya waandishi wa habari duniani kote walikubali kuwa habari za hali ya hewa na mazingira kwasasa zina umuhimu zaidi ikilinganishwa na miaka kumi oiliyopita.....

KWA NINI SHERIA MPYA YA HABARI NI MUHIMU ZANZIBAR

  NA NAFDA HINDI, ZANZIBAR Ni takriban miaka 20 sasa, shauku ya waandishi wa habari pamoja na watetezi wengine wa haki za binaadamu Zanzibar kuona nchi yao inapata sheria rafiki za habari imekuwa ikitimizwa kwa maneno. Viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini wamekuwa wakitoa ahadi lakini utekelezaji wake unasuasua. Tangu alipoingia madarakani, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekuwa akionesha kutambua umuhimu wa sekta ya habari kusimamiwa kwa kutumia sheria zilizo rafiki, kwa vile si mkosefu wa kujua ukweli kuwa sheria zilizopo ni kongwe zisizoendana na mazingira mapya yanayochagizwa na kasi ya ukuaji wa sayansi na teknolojia. Akiwa amekalia kiti cha Ikulu baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, Dk. Mwinyi hakuchukua muda kusikika akitoa matamshi yenye mtizamo wa kupendelea waandishi wawe na uhuru zaidi wa kufanya kazi zao, kwa kuamini kuwa itarahisisha manufaa ya utendaji wao kuwafikia wananchi kwa ukamilifu. Mara baada ya Baraz...