NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
TIMU ya
Wawi star, imejihakikishia kubakia ligi daraja la kwanza kanda ya Pemba msimu
ujao, baada ya jana kuichakaza Azimio SC kwa mabao 3-2, kwenye mchezo uliopigwa
uwanja wa Ngere ngere Jeshini, majira saa 10:30 jioni.
Kwa timu ya
Wawi star, mchezo huo kwao ulikuwa na maana pana, ili wajihakikishie kubakia
kwenye daraja hilo, hasa kwa vile mchezo unaofuata wataumana na Junguni anayesaka
alama za lazima za kuongoza ligi hiyo.
Katika mchezo
wa jana, ambao uliohudhuriwa na watazamaji wengi, ulianza kwa kasi, huku kila
timu ikiangalia ulipo udhaifu wa mwenzake, ili aondoke na alama tatu muhimu.
Katika kuhalalisho
hilo, Wawi star ilianza kuwafurahisha washabiki wake, mnamo dakika ya 15, pale
mshambuliaji wao hatari Suleiman Seif ‘Madeo’ alipotikisa nyavu kwa bao la
kwanza.
Lakini Azimio
SC, kwa vile walishaazimia ushindi, walisawazisha bao hilo, mnamo dakika ya 34,
kwa shuti la mbali lililopigwa na mlinzi wao Salum Kazumar, na kujaa wavuni.
Ingawa ‘Madeo’
wa Wawi star, aliwanyamazisha washabiki wa Azimio, baada ya mkwaju wake
alioujaribu wa umabli mita kama 25, nao kufanikiwa kuja wavuni, kabla ya Azimio
kuweka mambo sawa, kwa bao la pili, mnamo dakika 42 kwa shuti zito la mchezaji
wao Ali Rashid.
Wanaume hao,
walioonekana kukamiana, huku wakiacha shangwe na wakati mwingine manung’uniko
kwa wapenzi na washabiki wao, walizimaliza dakika 45 za awali, wakitoka uwanjani
wakiwa nguvu sawa.
Dakika 45 za
mwsiho, ndizo zilizokuwa za kasi zaidi, huku Wawi Star wakizitaka alama tatu
kama ilivyo hamu ya Azimio, ambao wako hatarini kuungana na timu sita
zitakazoshuka daraja la kwanza kanda ya Pemba.
Dakika mbili
kabla ya mchezo huo kumalizika, Suleiman Seif ‘Madeo’ ndie aliyeihakikishia
alama tatu Wawi star, safari hii akiukwamisha mpira wavuni kwa mkwaju wa penalti,
baada ya mlinzi wa Azimio, kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Hivyo mwamuzi
wa mchezo huo Suleiman Khatib Kisauti, aliamuru adhabu kubwa, na ‘Madeo’ bila
ya ajizi, aliipa alama tatu, na kujikusanyia alama 43 zinazowabakisha kwenye
lgi hiyo.
Mchezo
unaofuata wa Wawi Star, wataumana na Junguni United yenye alama 71 inayoongoza
ligi, inayopuliwa kwa karibu na Tekeleza FC yenye alama 70, wote wakiwa na michezo
sawa 31.
Timu inayoshika
nafasi ya tatu ni Mwenge SC, yenye alama 65, wakati News stone town na Konde
star zikiwa na alama sawa 46 kila mmoja.
Timu sita ambazo
zinapigiwa mnada wa kushuka daraja la kwanza mwakani, ni Tibirinzi star FC
yenye alama 21 kwa michezo 30, Dynamoo na Mkoroshoni United zina alama 25 kila
mmoja.
Timu nyingine
zinazojitarisha kushuka ni Kifumbi Kai FC na Mila FC zikiwa na alama 33, huku timu
ya Yosso boys ikiwa na alama 33, juu ya Alazzar FC yenya alama 36.
MWISHO
Comments
Post a Comment