RIPOTI: WAANDISHI WA HABARI ZA MAZINGIRA NA HALI YA HEWA WAKABILIWA NA UKOSEFU RASILIMALI NA VITISHO
Ripoti ya hivi karibuni ya Internews,
iliyofanywa kupitia mpango wake wa Uandishi wa Habari za mazingira kupitia shirika
lake la Earth Journalism, imetoa tathmini ya kina kuhusu hali ya uandishi wa
habari za hali ya hewa na mazingira duniani.
Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi chache zilizojumuishwa katika utafiti huu wa
kimataifa, ikitoa maarifa muhimu kuhusu mitazamo na uzoefu wa waandishi wa
habari katika eneo hilo.
Matokeo yanaonyesha kuwa kwa Tanzania nan chi nyingine uandishi
wa habari za mabadiliko ya hali ya hewa na masuala ya mazingira umeongezeka kwa
kiasi kikubwa. Kuongezeka kwa habari hizi kunahusishwa hasa na matatizo ya
mazingira yanayozidi kuongezeka na, kwa kiwango kidogo, kuongezeka kwa hamu ya
jamii kufhamu kuhusu masuala haya muhimu ya mazingira.
Ripoti hiyo inaonyesha kwamba Asilimia 82 ya waandishi wa habari
duniani kote walikubali kuwa habari za hali ya hewa na mazingira kwasasa zina
umuhimu zaidi ikilinganishwa na miaka kumi oiliyopita..
Hata hivyo, licha ya ongezeko hilo ripoti hiyo inaonyesha kwamba
waandishi wa habari wanakubali kwamba habari za mazingira wanazoripoti
hazitoshi ukilinganisha na uzito au ukubwa la mabadiriko ya tabia nchi na hali
ya hewa.
Ripoti imeonyesha kwamba waandishi wengi wanaandika habari
za hali ya hewa na mazingira kwa kuangalia Zaidi katika mtazamo wa
afya (asilimia 70), wakisisitiza uhusiano kati ya uharibifu wa mazingira na
afya ya jamii Mada nyingine zilizopewa kipaumbele mara nyingi ni pamoja na
ukataji miti (asilimia 58), maji na usafi wa mazingira (asilimia 58), uchafuzi
wa maji (asilimia 57), sera za serikali (asilimia 56), na uchafuzi wa plastiki
(asilimia 53).
Pamoja na mafanikio hayo ripoti hiyo imeonyesha changamoto
kadhaa zinazowakabili waandishi wa habari wanaondika masuala ya hali ya hewa na
mazingira. Asilimia 76 kubwa ya waandishi wa habari walitaja ukosefu wa
rasilimali kama kikwazo kikubwa. Aidha, dhana ya "usawa" bado ipo,
ambapo asilimia 62 ya waandishi wa habari waliohojiwa wanajumuisha vyanzo vya
habari vya
Kanuni za kitaaluma kama vile mlengo wa habari zinaendelea kuwa
msingi kwa waandishi wengi wa habari, huku wachache wakitetea misimamo au sera
maalum. Kwa kushangaza, asilimia 39 ya waandishi wa habari waliripoti kutishiwa
au kujizuia kuandika habari zinazohusu masuala ya hali ya hewa na mazingira,
huku vitisho vikijitokeza zaidi kutoka kwa watu wanaofanya shughuli haramu
zinazohusiana na mazingira.
Taarifa za kupotosha ni changamoto kubwa kwa uandishi wa habari
za hali ya hewa na mazingira. Kulingana na ripoti hiyo, asilimia 58 ya
waandishi wa habari waliona ongezeko la taarifa za kupotosha katika muongo
uliopita, ambazo zinasambazwa zaidi kupitia mitandao ya kijamii. Taarifa hizi
za kupotosha zinadhoofisha uelewa wa umma kuhusu masuala ya hali ya hewa,
ambapo asilimia 90 ya waandishi wa habari walikubali athari zake mbaya kwenye
habari zao.
Ili kushughulikia changamoto hizi, ripoti inapendekeza mashirika
ya ndani na kimataifa kuongeza msaada kwa waandishi wa habari wanaofunika
mabadiliko ya hali ya hewa na mazingira na kushirikiana na waandishi wa habari
na vyumba vya habari ili kuhakikisha ufadhili ulioelekezwa na endelevu.
Ripoti imependekeza pia kwamba waandishi wa habari walenge
katika kuandika masuala ya kimataifa ya mazingira kwa kuyalinganisha na maeneo
yao huku wakiepuka kutoa nafasi kwa watu au taasisi zinazopinga mabadiriko ya
hali ya hewa.
Ripoti pia inapendekeza vyumba vya habari na wahariri
kuhamasisha waandishi wa habari kubobea katika uandishi wa habari za hali ya
hewa na mazingira huku wakitoa kipaumbele katika kuchapisha na kutangaza habari
za hali ya hewa na mazingira mara kwa mara.
Na mwandishi wetu
|
ReplyReply allForward Add reaction |
Comments
Post a Comment