Skip to main content

TUZ: YAPOKEA MAONI YA WADAU PEMBA MKATABA WA UTOAJI HUDUMA

 



NA FATMA HAMAD, PEMBA@@@@

TUME ya Utangazaji Zanzibar TUZ, imeanza kupokea maoni, ili kuimarisha  rasimu ya mkataba wa utoaji wa huduma kwa wadau wa habari, ili kujenga ukaribu na uhusiano kwa wadau hao.

Akizungumza katika kikao cha kupokea maoni ya wadau kuhusu mkataba huo kwa wamiliki wa vyombo vya habari  na wadau wa huduma za utangazaji,  kilichofanyika ukumbi wa mikutano ZBC Chakechake, Afisa Utawala wa Tume hiyo Zanzibar Zuwena Mohamed alisema, maoni ya wadau yatasaidia kuwa na rasimu rafiki ya utoaji wa huduma.



Alisema Tume ya Utangazaji imebaini kuwa, kumekuwepo na baadhi ya watu hawaelewi huduma zinazotolewa na Tume hiyo, jambo linalopelekea kukosekana kuwepo kwa uhusiano mzuri kati ya Tume na Wadau.


‘’Tumekua tukipokea malalamiko mbalimbali kutoka kwa wadau wetu, hivyo tumeamua kuleta mkataba huu kwenu ili kuutolea maoni ambayo yataingizwa kwenye rasimu hapo badae yenye lengo la kuondosha malalamiko hayo pamoja na mambo mengine,’’alisema.

Alieleza kuwa, ujio wa rasimu hiyo ya mkataba  huo wa utoaji wa huduma kwa wataka huduma, utaleta mabadiliko makubwa katika sekta ya utangazaji, wandishi, wadau pamoja na watendaji wa Tume yenyewe.


Aliendelea kusema kuwa mkataba huo umegusa vipengele saba muhimu, ambapo moja ni kufanya mawasiliano na wadau pamoja na kuvitembelea vituo vya utangazaji kila baada ya miezi sita.

‘’ Vipengele vyengine vilivyomo ndani ya rasimu ya mkataba wa utoaji wa huduma kwa wadau wa utangazaji ni uwepo wa rufaa kwa mtaka huduma pindi hakupata huduma kwa wakati,’’alifafanua.



Mapema akifungua kikao kazi hicho, Mratibu wa Tume hiyo Ofisi ya Pemba Adam Ramadhan Kombo alisema, lengo hasa la mkataba huo ni kurahisha huduma za utangazaji na wadauwake katika shughuli zao mbalimbali za utangazaji.

Alieleza kuwa kwa kujali maoni ya wadau wake, Tume imeona ni vyema kuwakusanya na kupokea maoni yao, ili kuwa na rasimu rafiki na inayokwenda na wakati.

Hivyo aliwaomba wadau hao kuendelea kutoa maoni yao juu ya uimarishaji wa rasimu hiyo, ambayo ni kiungo muhimu baina ya Tume na wataka wataka huduma za Utangazaji.



‘’Hii ni fursa muhimu kwa wadau wetu, maana chombo hichi ndicho kitakachotuongoza sisi Tume kufikia malengo ya wataka huduma, ili kutimiza ndoto za shughuli zao za kila siku,’’alieleza.

 Nao baadhi ya wadau walioshiriki kikao hicho, walielezea kufurahishwa kwao, na wazo la Tume ya Utangazaji Zanzibar TUZ, kuileta rasimu hiyo kwao kwani wametekeleza takwa la kisheria.

 Mmoja kati ya wadau hao Mustafa Moyo alisema wakati umefika sasa kwa Tume hiyo kuvifuatilia zaidi vyombo vha habari mtandaoni hususani TV, ili kuhakikisha vinafuata kikamilifu kanuni za utangazaji.

‘’Chombo hichi cha mkataba kitakua suluhisho la wale wamiliki wa vyombo vya habari wanaokiuka maadili na kufganya kazi pasi na vibali, leseni pamoja na kutofuata miongozo inayotolewa na TUZ, alieleza.



Nae Maryam Talib Omar alisema kuwa rasimu hiyo itakapokamilika itakua ni daraja lenye ufanisi la mawasiliano baina ya Tume na wadau wa Utangazaji, jambo ambalo kwa sasa sio rafiki.

Tume ya Utangazaji Zanzibar TUZ kwa sasa inaendelea kukusanya maoni kwa wadau wake, ili kuwa na mkataba wa utoaji wa huduma kwa wadau wa utangazaji, jambo ambalo kwa miaka 14 iliyopita halipo.

MWISHO

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...