NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
UONGOZI
wa skuli ya sekondari ya Connecting Continent iliyopo Mgogoni wilaya ya Chake
chake, umesema kama wazazi na walezi wataongeza ushirikiano, kati yao na
waalimu, uwezekano wa kuondoa daraja la nne na la tatu kwa kidato cha nne upo.
Mwalimu mkuu
skulini hapo, Mwache Juma Abdalla, alisema waalimu wanaosomesha skuli hiyo,
wamekuwa na moyo mmoja wa kuondoa daraja la nne na la tatu kwa wanafunzi wa
kidato cha nne, hasa kwa mitihani ya taifa.
Alisema,
hilo linaweza kuwa rahisi mno, ikiwa kuanzia sasa wazazi na walezi, watajenga msingi madhubuti ya
ushirikiano kati yao na waalimu, skulini hapo.
Alieleza kuwa,
wapo wazazi na walezi, hawapiti skulini hapo jambo ambalo linalowapa ukakasi
waalimu na kuhisi wameachiwa majukumu peke yao ya ulezi.
Mwalimu mkuu
huyo, aliyasema hayo Julai 6, 20204 kwenye kikao cha kwanza kwa mwaka huu, cha kuwasilisha
matokeo ya muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha
nne.
Alifahamisha
kuwa, kimsingi matokeo hayo kwa muhula huu, sio mazuri ingawa siyo mabaya ya
kuvunja moyo, ingawa kitu cha kuzingatia ni kwa wazazi kuongeza juhudi za
kufuatilia masomo ya watoto wao.
‘’Leo (jana)
tumewasilisha matokeo haya ya majaribio kwa muhula wa kwanza, lakini ufaulu
wetu umeshuka, ikilinganishwa na miaka mingine,''alifafanua.
Katika hatua
nyingine, Mwalimu huyo mkuu Mwache Juma Abdalla, aliwataka wanafunzi
kushughulikia zaidi masomo yao, kuliko jambo jingine, lolote.
‘’Muelewe kuwa
wazazi na walezi wenu, wanawekeza rasilimali kubwa kwenu na wakati mwingine wanajinyima
kwa ajili yenu, sasa acheni anasa na msome kwa bidii,’’alifafanua.
Mapema
Mjumbe wa bodi ya wazazi ya skuli hiyo Omar Mjaka Ali, alisema kama juhudi za
waalimu hazikuungwa mkono na wazazi, kusitarajiwe kupanda kwa ufaulu.
Hata hivyo,
amesifu mbinu, juhudi, mikakati na dira zinazofanywa na waalimu skuli hapo,
katika kukuza uwelewa na ufaulu kwa wanafunzi.
Mwalimu Nassor
Mohamed Omar wa skuli hiyo, aliwakumbusha wazazi na walezi, kuwa wasiishie
kwenye huduma za chakula, mavazi na kulipa ada pekee, bali wawe karibu na
watoto wao.
Mwalimu Haji
Othman Haji, alisema jambo moja ambalo linawapa mshangao ni baadhi ya wazazi kujilimbikiza
ada, kwa zaidi ya miezi sita, na kisha kupuuza kufanya malipo.
Akiwasilisha
muhutasari wa matokeo hayo, Mwalimu Fadhila Rashid Khamis alisema, ufaulu kwa mitihani
hayo ya majaribio, kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, sio mazuri sana.
Alisema, kwa
mfano kati ya wanafunzi 82 wa kidato cha nne, waliofaulu ni 16, ambapo kati yao
wanawake ni tisa na wanaume saba, sawa na asilimia 19.5 ya wanafunzi wote.
‘’Hili
darasa mwishoni mwa mwaka huu, wataingia kwenye mitihani ya taifa, lakini haya
ya kuwapima hali hairidhishi, lazima tuendelee kushirikiana kati yetu,’’alifafanua.
Baadhi ya wazazi
wa wanafunzi hao, walisema mkazo uwekwe ili somo la kiingereza, kama msingi wa
masomo mingine lifahamike kwa upana.
Mzazi Nassor
Kai, aliwashauri waalimu kuendelea kubuni mbinu na mikakati endelevu, ili
kukabiliana na wanafunzi wavivu na wasiopenda kazi.
Subira Suleiman,
aliwataka wazazi wenzake, kupunguza mapenzi ya kupitiliza kwa watoto wao, na
kuwasimamia kwa dhati, ili kuhakikishan wanatimiza malengo yao.
Ali Salim
Ali, aliwashauri waaalimu, kuweka majaribio kila kipindi, ili wanafunzi hao kupima
uwezo wao pamoja na kutoka woga mitihani, jambo ambalo huchukua nafasi kubwa ya
kufeli.
Wanafunzi 82
wakiwemo wanawake 52 na wanaume 30 wanataeajiwa kufanya mitihani yao ya taifa
ya kidato cha nne mwaka huu skulini hapo.
Mwisho
Comments
Post a Comment