NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
“Waswahili
wanasema… ‘Pemba Peremba, ukienda na joho utarudi na kilemba’,.
Wengine wakasema kuwa, “waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba”.
Haya ni baadhi ya
misemo na misimu, ambayo wananchi wa kisiwa cha Pemba hupenda kuyatumia,
kulingana na wakati na kwenye kitu kinachohimiza maendeleo.
Karne zimepita, tangu misemo hiyo kutumika, licha ya kuendelea kutumiwa vijijini, kulingana na mazingira au kitu kilichopo.
Katika miaka
iliyopita, kulikuwa na baadhi ya watu waliweza kudiriki kusema kuwa, hakuna
uwezekano wa Pemba, kuwa ya viwanda, licha ya maeneo huru ya uwekezaji kutengwa
kwa miaka zaidi ya 20.
Sasa ni miaka
minne ya uongozi wa Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi, wananchi wa kisiwa
cha Pemba wameanza kujivunia maajabu ya kimaendeleo.
Tayari miradi ya kimkakati imeanza kuonekana ndani ya Kisiwa cha Pemba, kwa mabadiliko makubwa ya maendeleo, ndani ya kisiwa hicho.
Ilikua ni Julai 27 mwaka 2022, jua tayari linaelelekea kuzama, Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi alipowasilia katika eneo la Chamanangwe wilaya ya Wete na kudhihirisha kwa vitendo, msemo wake kuwa “Yajayo Yanafurahisha,”.
Hadithi hii inoga zaidi pale alipokunjua kitambaa na kukata utepe, kuashiria uzinduzi wa kiwanda cha Maji cha AMOS INDUSTRES LTD.
Mwaka jana, tena eneo la Kinyikani Wilaya ya Wete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, nae alikata utepe na kufungua kiwanda cha WATERCOM LTD kinachozalisha maji Pemba.
Kwa sasa tayari viwanda vitatu vikubwa vimejengwa, huku viwili vikifanya kazi ya uzalishaji, ikiwemo kiwanda cha Maji cha LULU kilichopo Chamanangwe na kiwanda kama kilichpo Kinyikani.
Kiwanda cha
kusarifia mwani nacho tayari bado kuanza kazi, huku viwanda vyengine, kama vile cha kuchakatia sembe na chakula cha kukua, kiwanda cha bati na Nondo vikiendelea na ujenzi.
Ndani ya miaka minne hii ya uongozi wa Rais Dk. Mwinyi, maeneo huru ya uwekezaji Micheweni sasa yameanza kung’ara, kufuatia uwepo wa barabara ya kisasa.
WANANCHI WANASEMAJE
Habiu Omar Haji, mkaazi wa Kiuyu wilaya ya Wete, anamshukuru Rais kwa kuona eneo la Chamanangwe,
ndani ya miaka minne kuwa ni eneo la uwekezaji kwa vitendo.
Anasema kuekezwa
miradi hiyo ni ishara nzuri ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wake, tayari
ishara ya kisiwa cha Pemba kufunguki kiuwekezaji yameanza kuonekana.
“Kwa sasa ni
faraja kubwa kwa vijana wetu, kupata ajira moja kwa moja, kupitia viwanda hivi,
wapo wanaingia moja kwa moja, wapo watakao jiajiri wenyewe kwa kuuza maji tu,”anasema.
Zuhura Juma Kombo anasema sasa wananchi wa Kisiwa cha Pemba, wanakunywa maji yanayozalishwa ndani
ya viwanda vilivyoipo Pemba na kuliuwa soko la maji kutoka maeneo mingine.
Anasema sasa ni
wakati kwa wananchi kuitunza hazina hii adimu, ambayo muda mrefu walikua
wakiisubiria ila ndani ya miaka minne ya Rais Dk. Mwinyi, kila kitu kimetimia.
“Inawezekana kila
wilaya inafurahia miaka minne ya Dk. Mwinyi akiwa Ikulu, lakini sisi wa wilaya
ya Wete, ndio zaidi tukofurani kwa kuwepo kwa viwanda hivi viwili,''anafafanua.
Said Omar Juma, anasema uwepo wa viwanda vya maji, ni kitu cha kihistoria, kitakachoweza kuinua
ajira kwa wananchi wa eneo hilo, na kisiwa kizima cha Pemba.
Anaona kama Dk.
Mwinyi, ameweka mazingira rafiki na kuwavuta wawekezaji,
ishara ya kuwa ni kiongozi imara inaonekana,’’anaeleza.
WAFANYA BIASHARA
Mfanyabiashara Ali Juma Ali, w Chake Chake, anasema biashara ya maji ndani ya kisiwa
cha Pemba, sasa imezidi kukua, kufuatia uwepo wa viwanda viwili, ambavyo
vinashindana kiuzalishaji.
“Tulikua
tukiagizishia maji kutoka Unguja, kama vile Drop, Uhai na maji mengine lakini
kwa sasa, tunamshukuru Dk. Mwimyi kwa kuweka mazingira na kupata wawekezaji,’’anasema.
Anaona ni muda
mchache tokea Rais wa awamu ya nane kuingia madarakani, lakini ahadi zake zimeanza
kuonekana tena kwa vitendo, katika kukibadilisha kisiwa cha Pemba.
Nae Othman Maulif Nassor wa Mkoani anasema, licha ya maji hata juisi za kitoto zimeanza
kuzalishwa ndani ya kisiwa cha Pemba, kupitia kiwanda cha maji cha Kinyikani.
Hapa anasema, kama kuna utekelezaji wa Ilani
ya CCM, kama ni mpango kazi wa Ikulu ya Zanzibar au maono yake, basi ndani ya
miaka hii mitatu amefanikiwa mno.
SEKTA YA UWEKEZAJI
Sekta ya
Uwekezeji Pemba imesajili miradi 12 mipya kipindi cha miaka miwili, miradi
yenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 183.324 sawa na zaidi ya
shilingi bilioni 419.553.
Kiujumla Pemba
nzima ina miradi 57 ya uwekezaji, yote ni matunda ya ya ndani ya miaka hii
mitatu ya Dk. Mwinyi.
Tayari visiwa
vitano vimepatiwa uwekezaji wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 136,
hiyo ni zaidi ya shilingi bilioni 304.367 za kitanzania.
ZIPA
Aliyekuwa Mkurugenzi wa 'ZIPA' Shariff Ali Sharif anasema, kiwanda hicho ni cha aina yake, wawekezaji wametumia
shilingi bilioni 1.8 na ajira zitakazo toka hapo ni 50 na kiwanda kitafanya
kazi masaa 24.
Anasema, Pemba
kuna miradi 57 na wametengeneza ajira za watu 2,889, Pemba imewekeza kupitia
ZIPA ambapo jumla ya dola za Kimarekani milioni 413.13, baada ya kuitangaza Pemba
eneo la kimkakati la uwekezaji.
Tayari visiwa
vitano vidogo vidogo ikiwemo Njau dola milioni 15, Kashani dola milioni 8,
Misali dola milioni 83, Kwata dola milioni 15 na Kisiwa cha Mtangano dola milioni
15, ambapo jumla ya dola za Kimarekani milioni 136.
Kwani anasema, ni hatua kubwa katika miaka tatu ya Rais Dk. Mwinyi kuwepo kwa kiwanda hicho na hayo yakidhihirisha upeo alionayo.
Amemshukuru Rais
kwa muono wake wa kukifungua kisiwa cha Pemba kiuwekezaji, hiyo ni hatua kubwa
ndani ya miaka mitatu.
Anasema kwani ni zaidi
ya dola bilioni 1 imekezwa katika kisiwa cha Pemba, kwa kipindi cha miaka
mitatu, jambo ambalo limevunja rekodi.
“Kisiwa cha Pemba
kimetangazwa kama kisiwa mkakati cha uwekezeji, ni kisiwa ambacho kina ‘brandi’
ya uhifadhi wa mazingira hata aina ya viwanda, vinazingatia uhifadhi wa
mazingira,’’anasema.
Waziri wa Biashara
na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban, anasema kinachoonekana, ni
matunda ya maelekezo ya Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, juu ya maagizo
anayoyataka Zanzibar iwe na viwanda vya kila saizi, kati, kikubwa na kidogo.
Anasema ekari 136
ambazo zimetengwa kwa ajili ya viwanda, tayari maombi mbali mbali, wameshaanza
kupokewa,
‘’Kwa kule ndani
ya miaka mitatu ya Dk. Mwinyi kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji,
tumeshapokea maombi ya kampuni ya ‘Group’ wanataka kujenga kiwanda cha
Mabati na Ahmed Said anataka kujenga kiwanda cha kuzalisha bomba za plastiki,’’anasema
Waziri.
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, anasema AMOS ni Mwekezaji
wa kwanza, kuekeza kiwanda cha maji Pemba.
Anasema pia
anakusudia kuekeza mitambo ya uzalishaji wa Juice na askrim, tayari ametimiza
dhamira yake kwa vitendo, na sio maneneo kwa kuekeza bilioni 1.8.
Anasema, viwanda
vinatoa faida ya moja kwa moja, ikiwemo ajira kwa wananchi, watakao ajiriwa
kiwandani na hata wafanyabiashara nje ya kiwanda, ikiwemo kuwepo na soko kubwa
la matunda ikiwemo embe, pesheni na mabungo.
“Kuwepo kwa kiwanda
hicho, kitarahisisha maendeleo ya vijana wa kisiwa cha Pemba, hata kitakuza
uchumi wa mtu mmoja mmoja,”anasema.
Sote tunakila
sababu ya kufurahia kwa vitendo kauli ya “Yjayoi
yanafurahisha” “Yajayo ni neema Tupu” tayari neema wenyewe tumeshaanza
kuziona, ikiwemo kuanza kufungua kisiwa cha Pemba kiuwekezaji.
MWISHO
Comments
Post a Comment