SALIM HAMAD, PEMBA@@@@
HAKIMU wa Mahkama ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, Zuwena Mohamed Abdul-kadir amewataka wadau wa mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji, kuongeza kasi katika mapambano hayo, ili kuwakinga watoto wasiharibiwe, ambao ndio kundi kubwa linalokabiliwa na shida hizo.
Kauli hiyo ya Hakim wa Mkoa, imetolewa kwaniaba yake na Hakimu wa Mahkama ya Mwanzo Wete Adam Abdalla Faki wakati akizungumza na Wadau wa Mambano ya Udhalilishaji, katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa uwezeshaji wa Kisheria na upatikanaji wa haki unaofadhiliwa na UNDP uliofanyika Baraza la Mji Wete.
Alisema katika kumaliza shidha hizo, wadau kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kusimama imara na kutoa ushirikiano katika kupiga vita vitendo hivyo visiendelee.
‘’Bado vitendo hivi vinaendelea kujitokeza pamoja na juhudi zote zinazochukulia lakini tunatakiwa kuwa wamoja na mashiriano kupiga vita vitendo hivyo,’’alisema .
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo kutoka Jumuia ya wasaidizi wa sheria Wete WEPO, Rashid Hassan Mshamata alisema mradi huo utajikita katika kuanizsha vilabu tofuti kwenye shehia ikiwemo katika Madrasa, ikiwa lengo ni kuona juhudi za mambano hayo zinaimarika.
Alisema hatua hii ya unzishwaji wa Vilabu kwenye maeno mbali mbali kwenye shehia kwa kiasi kikubwa, yanaweza kusaidia baada ya kupewa elimu juu athari za majanga hayo.
‘’Lengo kuu ya mradi huu ni kuona zile haki anazipata yule mtu atakaekabiliwa na shida hizo tunataka kunzisha vilabu katika maeneo mbali mbali kwenye Shehia, ikiwemo pia Madrsa tutawapa elimu naamini mpango huo utasaidia katika kuongeza kasi ya mapambano juu ya vitendo hivyo,’’alisema Rashid.
Naye Mkurugezni wa Jumuiya ya Wasaidizi wa Sheria Wilaya ya Wete (WEPO) Hemed Ali Hemed alisema miongoni mwa kazi za wasaidizi wa Sheria ni kutoa elimu ya kisheria katika maeneo tofauti ili jamii iweze kutambua haki zao.
Sheha wa Shehia ya Kiungoni Omar Khamis Othaman, alisema miongoni mwa sababu zinaochangia kutokumalizika kwa kesi hizo ni kuwepo kwa rushwa muhali.
Alisema mtu anakwenda kuripoti Polisi, lakini baadae anafuatwa na wanafamilia kupewa chochote na badala yake hafiki tena mahakamani kwenda kutoa ushahidi jambo hili linarudisha nyuma.
‘’Tatizo kubwa linalosumbua ni kuwepo kwa rushwa muhali, mtu anakwenda kuripoti vizuri kesi yake lakini baadae anafuatwa na wanafamilia kupewa chochote na hatmae kushindwa kwenda kutoa ushahidi na kesi kupotea,’’alisema.
Mkutano huo uliwakutanisha wadau tofauti ikiwemo Masheha, Polisi, Wasaidizi wa Sheria, walimu na Madaktari ambapo mada mbali mbali ziliwasilishwa ikiwemo haki za Binadamu na makosa ya udhalilishaji.
MWISHO.
Comments
Post a Comment