Skip to main content

MCHAKATO UKUSANYAJI MAONI MAREKEBISHO SHERIA YA MTOTO WAANZA

 








Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Siti Abass Ali amesema Idara hiyo ipo katika mchakato wa kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbali kwa ajili ya kuifanyia maboresho sheria ya Mtoto namba sita (6) ya mwaka 2011 ili iendane na wakati uliyopo.

 

Akizungumza katika kikao cha ukusanyaji wa maoni kilichowashirikisha  wadau mbali mbali wakiwemo viongozi wa dini, wanasheria, Jeshi la Polisi, n.k  katika ukumbi wa Skuli ya Kidonge Chekundu Unguja, jana alisema kutokana na vitendo vinavyojitokeza katika jamii,ikiwemo ajira za utotoni hivyo, idara hiyo imelazimika kuipitia sheria hiyo nakuja na maamuzi ya kuifanyia maboresha ili iendane na wakati .

“Kwa kweli Sheria hiyo  imetusaidia sana na inaenaendelea kutusaidia, imezungumza umuhimu wa mtoto kupata haki zake za msingi ikiwemo haki ya kupata elimu, matibabu, chakula, malazi, malezi, pia imezungumzia jinsi gani mtoto ataepukana na masauali ya udhalilishaji lakini baada ya kuipitia sheria hiyo tumeona bora tuifanyie maboreshao ili iwe nzuri zaidi, pia tumeona  ni ya muda kidogo, tangu ilipotungwa hadi leo ni miaka kumi na mbili na  vitendo vinaendelea kujitokeza kama hili suali la ajira za utotoni ni changamoto kubwa” Alisema Siti.




Alisema katika ukusanyajji wa maoni wameanza na makundi ya watoto kupitia mabaraza ya watoto, viongozi wa dini, waandishi wa Habari, waratibu wa kupinga vitendo vya ukatili na udhalilishaji, Wizara na Taasisi mbali mbali za Umma na Binafsi, wakiwemo Wizara ya elimu, Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar (TAMWA-ZNZ), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), n.k.

Aidha Mkurugenzi Siti alifafanua kwamba umuhimu wa marekebisho ya Sheria ya  mtoto ni pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia  ambayo kimsingi yameongeza haja ya kuimarisha baadhi ya vipengele katika sheria hiyo.

Naye Mkuu wa Divisheni ya Watoto wa Idara hiyo Mohammed Jabir alisema kipengele namba 18 cha uanzishaji na uendeshaji wa mahakama ya Watoto kimeeka wazi aina ya makosa na muda ambao mshatakiwa atapaswa kutumikia adhabu au kifungo lakini adhabu hiyo sio kali hivyo ni wazi kwamba marekebisho  yanahitajika katika kupengele hicho.




Pia alisema kipengeleza namba 12 kimezingatia majukumu ya wazazi katika kuwasiamia Watoto ila bado wazazi hawakielewa na kukitumia kinavyotakiwa katika kuleta mageuzi ya malezi bora kwa Watoto, hivyo kanuni inahitajika ili iweze kutoa miongozo.

Kwa upande wa washiriki wa mkutano ambao ni wadau wa kupinga Vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji wa kijinsia wamesema Sheria ya Mtoto namba 6 ya mwaka 2011 ni vyema ikatambua mgawanyo  wa haki za watoto kwa kuzingatia umri ili kulinda maslahi na ustawi wa mtoto.

 



Akizungumza  Hakimu dhamana Mkoa wa Kusini Unguja  Khamis Rashid Khamis  amesema ni wakati sahihi  wa kueka sheria ambayo Itatoa muongozo wa kushughulikia watoto wenye umri wa chini ya miaka 14  na 16 na kuweka utaratibu wa kusikiliza kesi zao.

 


Idara ya Maeleleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inaendelea na ukusanyaji wa maoni kwa kukutana na makundi mbali mbali katika jamii  kwa lengo la kuipata maomi ili sheria mpya iwe   nzuri kwa na yenye maslah kwa mtoto.

 

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...

…….SUZA WATOA USHAURI WA ADHABU YA KUNYONGWA

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ WANAFUNZI wanaosomea uwalimu Chuo cha taifa cha Zanzibar ‘SUZA’ kampasi ya Benjamin Wiliam Mkapa Wete Pemba, wamependekeza adhabu ya kunyongwa hadi kufa, kwa mtu atakaetiwa hatiani, kwa kosa la dawa za kulevya. Walisema, haiingii akili kuona, mahkama imeshamtia hatiani mtu kwa kukutwa na dawa za kulevya, ambazo huathiri nguvu kazi ya taifa na kisha, kupewa hukumu ya kifungo pekee. Wakizungumza leo Juni 26, 2024 kwenye kongamano la vyuo vikuu, juu ya masuala ya msaada wa kisheria, kuelekea wiki ya msaada wa kisheria Zanzibar, lililofanyika Chuoni hapo, walisema wakati umefika sasa kutolewa kwa hukumu hiyo. Walipendekeza kuwa, ni vyema kwa mtu anayetiwa hatiani asibakie chuo cha Mafunzo pekee kuitia tena hasara serikali kwa chakula na wakati mwingine matibabu, wakati tayari ameshasababisha madhara, kwa vijana. Mshiriki Juma Nafasi Juma, alifafanua kuwa kama mtu ameamua kuliumiza taifa kwa kuingiza, kusafirisha, kusambaaza dawa za kulevya, hivyo n...