NA HAJI
NASSOR, PEMBA@@@@
WAKALA wa
usajili na matukio ya kijamii Zanzibar, wilaya ya Chake chake, imekumbushwa kuwatumia
waandishi wa habari na wadau wengine wa haki za binaadamu, ili kufikia jamii kwa
lengo la kuielimisha na kuepukana na vyeti na vitambulisho vyenye mgogoro
miongoni mwao.
Wito huo
ulitolewa leo Oktoba 17, 2023 na Mkurugenzi wa mradi wa kuihamasisha jamii
kudai haki zao za uongozi, siasa na demokrasia ‘SWIL’ kutoka Jumuiaya ya
Utetezi wa Mazingira na Jinsia ‘PEGAO’ Hafidh Abdi Said, kwenye mkutano wa
kuwasilisha kero, zilizoibuliwa na wahamasishaji, uliofanyika ofisi ya TAMWA Mkanjuni
Chake chake.
Alisema kuwa,
kutokana na jamii kutokuwa na ufahamu wa kutosha juu ya vielelezo hivyo,
kumepelekea kuwepo kwa tatizo kubwa ambalo linahitaji kufanyiwa kazi, ili
liweze kuondokana nav yeti bandia na vitambulisho vye mgogoro.
Alieleza
kuwa, tatizo hilo limekuwa ni la muda mrefu katika jamii, hivyo ni wakati sasa
Wakala wa usahili na matukio ya kijamii kufanyaka kazi zao kwa karibu na vyombo
vya Habari, ili jamii itambue kasoro zao.
Mkurugenzi
huyo alieleza kuwam jambo hilo sasa limekuwa kubwa na kwamba ni kosa linalosababisha
athari kubwa, ikiwemo watu kucheleweshewa kupata haki zao, kukosa mikopo,
safari za kimatibabu kutokana na kasoro iliyomo kwenye nyaraka hizo.
‘’Niwaombe
sana wenzetu wanaoshughulikia vitambulisho, vyeti vya kuzaliwa, takala, ndoa na
nyaraka nyingine za serikali, kuanzisha mpango maalum na endelevu ili
kuhakikisha jamii inapata uwelewa wa kutosha,’’alishauri Mkurugenzi huyo.
Katika hatua
nyingine Mkurugenzi wa mradi huo Hafidh Abdi Said, alieleza kuwa ujio wa mradi
huo umekuwa ukisaidia kuibua changamoto nyingi kwa jamii, ikiwemo vyeti na
vitambulisho vyenya kasoro, ukosefu wa huduma za kijamii Pamoja na jamii
kulalamikia utaratibu mbovu kwa vaadhi ya tasisi za serikali.
Mratibu wa
Chama cha waandishi wa Habari Tanzania TAMWA-Zanzibar ofisi ya Pemba Fat-hiya
Mussa Said, alisema kuwa mradi huo wa SWILL unahamasisha na kuwawezesha jamii,
katika kupata haki zao stahiki, bila pingamizi zozote na sio kwenye nafasi za
uongozi pekee, kama ilivyozoeleka kwa baadhi ya watu.
Hivyo
waandishi wa habari na wadau wengine kuona kwamba kuna umuhimu mkubwa kwao,
kuifikia jamii kuwapa elimu juu ya haki mbali mbali za jamii.
‘’Mradi huu
umekuja kuibua changamoto ambazo kwa njia moja ama nyingine zinamsahaulisha
mwanamke kugombea, kudai haki zake za kisiasa na kijamii,’’alifafanua.
Mapema akiwasilisha
changamoto zilizoibuliwa na wahamasishaji jamii, juu ya kudai haki zao za
uongozi demokrasia na siasa, mtoa mada Khalfan Amour Mohamed alieleza kuwa,
bado jamii inatatizo la uelewa mdogo juu ya haki yao ya vyeti vya kuzaliwa na
vitambulisho vya mzanzibari mkaazi.
‘’Imebainika
kuwa, kuna utamaduni kwa baadhi ya watu kuwatuma wengine kuwafuatilia zao,
hivyo kama kuna kasoro inakuwa vigumu kubaini na kisha kurudi kwenye mamlaka
husika,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine, amewakumbusha wazazi na walezi, kuwa makini wakati wanapowasilisha
taarifa za watoto wakati wa kuandikishwa skuli, kwani taarifa hizo hutumika
hata baada ya kumalizika kwa masomo.
Hata hivyo aliwataka
wananchi wasikubali kuwatumia wasiokuwa wafanyakazi wa mamlaka husika, katika
maeneo mbali mbali wanayokwenda kutaka huduma za umma.
Nae Afisa
Elimu na Mafunzo ya Amali mkoa wa kusini Pemba, Mohamed Shamte Omar, amezitaka
taasisi husika zinazosajili matukio ya kijamii, kuondosha vikwazo pale
inapotokezea changamoto mbali mbali, ili jamii isikate tamaa na ofisi hiyo.
Mapema Afisa
kutoka Wakala wa Usajili na Matukio ya Kijamii wilaya ya Chake chake Yussuf Iddi
Faki, alisema lawama zinazoelekezwa kwao sio sahihi, kwani wao wamekuwa
wakiandika taarifa wanazopewa na mlengwa.
‘’Sisi
taarifa ambazo zimo kwenye vitambulisho, vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya kifo, ndoa
na talak azote hupewa na jamii husika na uthibitisho wake wa kina, sasa ikitokezea
kuna shida ya jina ni mwananchi mwenyewe ndio muhisika,’’alieleza.
Nao
waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti Salimu Ali Mselem na Essau Saimon
Kalukubila, walieleza kuwa, watakuwa wajumbe kwa jamii, kuona wanaelimisha juu
ya madhara ya kuwa na vielelezo visivyorasmi wakati wa kutengeneza nyaraka za
serikali.
Mwisho
Comments
Post a Comment