Na Nafda Hindi@@@@
Wizara ya Afya imeombwa kutoa mashirikiano
mazuri kwa waandishi wa habari kwa lengo la kuleta mabadiliko katika jamii.
Akizungumza wakati wa uwasilishaji
ripoti ya elimu ya Afya ya Uzazi kwa wasichana na wanawake wa mjini na
vijijini katika ukumbi wa Kificho Mwanakwerekwe Mkurugenzi wa chama cha
waandishi wahabari wanawake Tanzania Zanzibar Dk. Mzuri Issa amesema watendaji wa
Wizara husika kuepuka tabia ya usiri wa kutotoa taarifa muhimu zinazogusa
maisha ya watu.
“ Kuna usiri wa taarifa kwa baadhi ya
watendaji hivyo tunaiomba Wizara ya Afya iendelee kutoa mashirikiano mazuri kwa
waandhishi wahabari kwa sababu masuala ya kinchi nay a kijamii ni lazima
yasikike kupitia vyombo vya habari,’ Dk Mzuri Issa, Mkurugenzi TAMWA,ZNZ.
Dk Mzuri amesema masuàla yànayohusu nchi
pàmoja na jamii lazima yasikike kupitia vyombo vya habari kwa wananchi kupaza
sauti zao
“ Ni haki ya kila mtu kupata taarifa na uhuru
wa kujieleza na katiba zote mbili zimeeleza ile ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na ya Zanzibar na hata kidunia tumesaini mikataba mbali mbali ya Kimataifa ikiwemo Africa
Charter, Dk Mzuri Issa.
Mapema akiwasilisha ripoti hiyo Afisa Tathmini
na Ufatiliaji Abdul Mohamed kutoka TAMWA ZNZ amesema ripoti hiyo imengunduwa
mapungufu kadhaa kama vile ukusanyi wa takwimu zà uhakika pamoja na umri
zinazohusu wanawake na wasichana zinazoonesha vifo wakati wa kujifunguwa.
“Baadhi ya mafungufu ni kutokuwepo takwimu
sahihi za vifo na umri kwa wanawake na wasichana, tunaomba Wizara ya husika
lifanyie kazi”, Abdul Mohamed.
Nae Afisa mradi wa kuendeleza utetezi kwa
vyombo vya habari kwa wasichana na wanawake kutoka TÀMWA ZNZ Zaina Abdalla Mzee
amesema lengo la mradi huo ni kuibuwa changamoto zinazowakuta kundi hilo pamoja
na vituo vya Afya na kuzitafutia ufumbuzi kwa wahusika.
“Tulianza kwa kufanya utafiti na kugunduwa waandishi
wengi hawana uelewa juu ya masuala ya Afya ya uzazi hivyo tuliandaa mafunzo ya
kuwajengea uwezo na sasa wanaripoti vyema habari hizi na wanasaidia jamii
kupata huduma stahiki,” Zaina Mzee.
Nao watendaji kutoka Wizara yà Afya Zanzibàr
wamekiri kuwepo kwa baadhi ta changamoto katika sekta hiyo ikiwemo bajeti ndogo
ukilinganisha na mahitaji ya wananchi.
Hata hivyo wàndishi wahabari waliopatiwa
mafunzo kupitia mradi huo wamesema wanakabiliwa na changamoto wakati wa kuandaa
habari pamoja na vipindi kwa bàadhi ya wandendaji wa Wizara hiyo kutotoa
mashirikiano.
“ Changamoto zinakuja kwa baadhi ya watendaji
kutupiga danadana wakati wa kukusanya hizi taarifa kwa hivyo inatuwia vigumu kuzipata
kwa muda sahihi na nyengine hazipatikani kabisa,” Waandishi wa habari.
Mradi wa kuendeleza utetezi wa haki ya elimu
ya Afya ya uzazi kwa vyombo vya habari kwa wasichana na wanawake
unaotekelezwa na TAMWA ZNZ ulitowa mafunzo kwa waandishi wa habari 71 na
wahariri 23 kwa Unguja na Pemba ambapo ulioanza Octobet 2022 na kumalizika
October 2023 ulitekelezwa kwa Wilaya ya Magharibi "B" na Kati kwa
Unguja na Wilaya ya Chake Chake kwa Pemba.
Comments
Post a Comment