NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MAOFISA wa wizara ya Afya Pemba,
wamesema sasa wako tayari kuzidisha ushirikiano kati yao na vyombo vya habari,
kwa ajili ya kuwapa taarifa wananchi, juu ya shughuli mbali mbali zikiwemo za
haki ya afya ya uzazi.
Walisema, waandishi wa habari, ndio
wasemaji wa wasio kuwa na suati, hivyo suala la kuongeza ushirikiano, kwa hilo
wako tayari wakati wowote na kwa jambo lolote.
Wakizungumza kwenye mkutano wa
ufungaji wa mradi wa Haki ya afya ya uzazi, uliofanyikwa ofisi ya Chama cha
waandishi wa Habari wanawake Tanzania TAMWA-Zanzibar ofisi ya Pemba, walisema
ni vyema, waandishi wakawafika wanapowahitaji kwa kutengena Habari mbali mbali.
Walisema kupitia mradi huo, waandishi
wa Habari walisaidia mno kuharakisha upatikanaji huduma, kama za afya ya mama
na mtoto, huduma za kuchuunguza afya hasa
kwa virusi vya Ukimwi, jambo ambalo limewasaidia wananchi
Daktari wa wilaya ya Chake chake ‘DMO’
Sharif Hamad Khatib, alisema kwa mfano suala la kukatika kwa huduma ya maji safi
na salama kituo cha Afya Wesha, ambalo liliibuliwa na waandishi wa Habari, limesaidia
mno.
‘’Kwa huduma ya maji safi na salama
sasa imerejea, na wanaokwenda kujifungua, ingawa hakutakiwa kupeleka maji, lakini
kwa ujumla huduma imerejea, baada ya timu ya Waandishi wa Habari, iliyoratibiwa
na TAMWA, kwenda kuibua changamoto hiyo,’’alisifia.
Aidha Daktari huyo alisema, kimsingi
na kiafya hata hospitali ikose huduma ya maji safi na salama, hatakiwi mzazi
ama mgonjwa mwengine, kupeleka huduma ya maji, na badala yake wizara ndio yenye
jukumu hilo.
Mratibu wa Kitengo Shirikishi cha Afya
ya Mama, mtoto na Lishe Pemba Mkasha Hija Mkasha, alisema waandishi wamekuwa
wakisaidia mno, ili kuhakikisha hakuna anayejifungulia nyumbani.
‘’Waandishi wa Habari karibuni ofisini kwetu, kufanya makala, vipindi na habari nyingine, juu ya haki ya afya ya uzazi kwa mama na mtoto, kwani haya ndio ambayo jamii, wanapaswa kuyajua,’’alieleza.
Kwa upande wake, Mratibu kitengo Shirikishi Ukimwi, Kifua kikuu, Homa ya Ini na Ukoma Pemba Dk. Khamis Hamad, alisema
kupitia mradi huo kwa upande wa Unguja, kuliibuliwa uhaba wa vifaa vya
kuchunguuzia virusi vya Ukimwi, jambo ambalo liliwasaidia kupatikana kwake.
‘’Sisi ilikuwa tunajua kuwa baadhi ya
vituo vya afya vifaa hivyo ‘HIV kits’ havipo, lakini ile habari ilipotoka,
hakuna aliyelala ofisini, kwa sasa vifaa hivyo vimesharejea, hivyo mliwasaidia
wahitaji,’’alieleza.
Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano
huo, Mratibu wa TAMWA ofisi ya Pemba Fat-hya Mussa Said, alisema mradi huo
umekuja, baada ya jamii na waandishi wa habari kutokuwa na uwelewa mpana wa haki
ya afya ya uzazi.
''Kuanzia mwezi Aprili hadi Juni mwaka huu, TAMWA ilifanya utafiti katika vyombo vya habari, na kugundulika kuwa, waandishi hawana uwelewa wa kutosha, juu ya haki ya afya ya uzazi,’’alifafanua.
Mratibu wa mradi wa haki ya afya ya
uzazi kutoka TAMWA-Zanzibar Zaina Abdalla Mzee, alisema mradi huo wa majaribio,
kwa sasa unaelekea kufikia ukingoni, kwa vile ulikuwa ukitekelezwa kwa mwaka
mmoja.
‘’Mradi huu, ulikuwa unatekelezwa katika wilaya ya Chake chake kwa Pemba na wilaya ya Magharibi ‘B’ na Kati kwa Unguja, na jamii imefikiwa, maana vipo vipindi 24 vya redio makala zaidi ya 35 pamoja na zaidi ya habari mchanganyiko 50 kwenye mitandao ya kijamii zilizoandikwa,’’alifafanua.
Hata hivyo Mratibu huyo, alisifia wazo
la maofisi hao wa wizara ya Afya la kuwakaribisha waandishi wa habari katika
ofisi zao, kwani moja ya changamoto zilizoonekana katika utafiti mdogo, ni
ushirikiano unaolega lega baina ya pande hizo.
Akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa mradi huo, Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka TAMWA Zanzibar Abdull-rahman Mohamed, alisema inaonesha uwepo wa mafanikio kwa jamii, baada ya waandishi wa habari kuandaa vipindi na makala.
Alieleza kuwa, lengo hasa la mradi huo,
ilikuwa ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari, ili waandike kwa uweledi juu
ya haki ya afya ya uzazi, ambao walengwa wakuu ni wasichana na wanawake.
Waandishi wa Habari akiwemo Essau Saimon
Kalukubila wa redio jamii Micheweni na Sheikh Rashid Seif wa Shirika la
Utangaazaji Zanzibar ZBC, waliahidi kuendelea kuwaelimisha wananchi.
Maradi huo wa majaribio wa mwaka mmoja, uliendeshwa
katika wilaya za Magharibi ‘B’ na Kati kwa Unguja na wilaya ya Chake chake kwa
Pemba.
Ambapo mradi unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya TAMWA-Zanzibar na wenzao wa Tanzania bara, unafadhiliwa na Shirika la Wellspring Philonthropic fund la Marekani
Shabaha kuu ya mradi huo ni kuwajengea uwezo waandishi
wa habari, ili kuripoti kwa ufanisi, juu ya haki ya afya ya uzazi kwa wanawake
na wasichana walioko mjini na vijijini.
Mwisho
Comments
Post a Comment