NA
HAJI NASSOR, PEMBA:::
MAHAKAMA
ya maalum ya makosa ya udhalilishaji ya Mkoa kusini Pemba, iliyopo Chake chake,
asubuhi ya leo Oktoba 31, inatarajia kusoma hukumu ya mwalimu skuli ya Madungu
msingi Ali Makame Khatib, anayetuhumiwa kumbaka mwanafunzi wake.
Mahakama hiyo, chini ya
hakimu wake Muumini Ali Juma, imefikia uamuzi huo, baada ya pande zote mbili
mahakamani hapo, kufunga ushahidi wao.
Ambapo kwa upande wa
utetezi, ulifunga ushahidi wake tokea Oktoba 19, mwaka huu baada ya mtuhumiwa
huyo kuwasilisha mashahidi wanne, wakiwemo waalimu wa skuli ya Madungu msingi.
Ambapo katika utetezi huo,
walidai kuwa mtuhumiwa hawajahi kuripotiwa skulini hapo, kuwa amekuwa na vitendo
viovu, hivyo wana hakika mwalimu huyo (mtuhumiwa) hajambaka mwanafunzi wake,
kama ilivyodaiwa.
Kwa upande wa mashtaka
ukiongozwa wakili wa serikali Ali Amour Makame, ulifunga ushahidi wake tokea
Oktoba 11, mwaka huu na Oktoba 12, mahakama hiyo ikatoa uamuzi, kuwa mtuhumiwa anyo
kesi ya kujibu.
Hivyo kutoka Oktoba 19, mara
baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wao, mahakama hiyo maalum ya makosa
ya udhalilishaji, imepanga leo Oktoba 31 iwe ni siku ya kusoma hukumu kwa
mtuhumiwa.
‘’Kama upande wa utetezi na
mashataka mmeshafunga ushahidi wenu, mahakama inapanga Jumatatu ya Oktoba 31,
mwaka huu, iwe ni siku ya kusoma huku, hivyo mtuhumiwa arejeshwe tena rumande
hdi siku hiyo,’’alisema Hakimu Muumini.
Hata hivyo wakili wa upande
wa utetezi Suleiman Omar, alikubaliana na uamuzi wa mahakama hiyo, kulipanga
shauri hilo leo hii Oktoba 31 kwa ajili ya hukumu.
Awali ilidaiwa mahakamani
hapo kuwa, mtuhumiwa huyo Ali Makame Khatib (mwalimu wa skuli), mkaazi wa
Matuleni wilaya ya Chake chake, alidaiwa kumbaka mtoto (mwanafunzi wake) mwenye
miaka 11.
Aambapo kufanya hivyo ni
kinyume na kifungu 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya Adhabu
nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment