NA
HAJI NASSOR, PEMBA::::
MAHAKAMA
ya maalum ya makosa ya udhalilishaji ya Mkoa kusini Pemba, iliyopo Chake chake,
imelazimika kumrejesha tena rumande, mwalimu wa skuli ya Madungu msingi Chake
chake Ali Khatib Makame, baada ya kushindwa kumsomea hukumu yake.
Mahakama hiyo chini ya
hakimu wake Muumini Ali Juma, juzi Oktoba 31, mwaka huu ilitarajia kusomea
hukumu ya mwalimu huyo, anayedaiwa kumbaka mwanafunzi wake, ingawa hakusomewa,
kutokana na kutokamilika.
‘’Ni kweli leo (juzi Oktoba
31), tulitarajia kukusomea hukumu yake, ingawa kutokana na kuwepo kwa hukumu
nyingi ya kwako, bado haijamalizika kuandaliwa, hivyo utarudi tena
rumande,’’alisema Hakimu.
Hakimu huyo, baada ya
kushauriana na upande wa mashataka na utetezi, aliamua kulirejesha tena shauri hilo
Novemba 14, mwaka huu na kusema siku hiyo itakuwa na ya kusomea hukumu.
Awali Mwendesha Mashataka
kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka, Ali Amour Makame, alidai kuwa shauri
hilo lipo mahakamani hapo, kwa ajili ya hukumu na hasa baada ya wiki mbili
zilizopita, pande zote mbili kufunga ushahidi wao.
Wakili wa mtuhumiwa huyo
Suleiman Omar Suleiman, alipoulizwa na Hakimu Muumini, alidai hana pingamizi
yoyote juu ya uamuzi uliotolewa mahakamani hapo.
Ambapo kwa upande wa
utetezi, ulifunga ushahidi wake tokea Oktoba 19, mwaka huu baada ya mtuhumiwa
huyo kuwasilisha mashahidi wanne, wakiwemo waalimu wa skuli ya Madungu msingi.
Kwa upande wa mashtaka,
ukiongozwa wakili wa serikali Ali Amour Makame, ulifunga ushahidi wake tokea
Oktoba 11, mwaka huu na Oktoba 12, mahakama hiyo ikatoa uamuzi, kuwa mtuhumiwa anyo
kesi ya kujibu.
Hivyo kutoka Oktoba 19, mara
baada ya upande wa utetezi kufunga ushahidi wao, mahakama hiyo maalum ya makosa
ya udhalilishaji, imepanga leo Oktoba 31 iwe ni siku ya kusoma hukumu, ingawa
pia imeghairishwa tena hadi Novemba 14, mwaka huu.
Awali ilidaiwa mahakamani
hapo kuwa, mtuhumiwa huyo Ali Makame Khatib (mwalimu wa skuli), mkaazi wa
Matuleni wilaya ya Chake chake, alidaiwa kumbaka mtoto (mwanafunzi wake) mwenye
miaka 11.
Ambapo kufanya hivyo ni
kinyume na kifungu 108 (1), (2) (e) na kifungu cha 109 (1) cha sheria ya Adhabu
nambari 6 ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment