NA
HAJI NASSOR, PEMBA::
WIZARA
ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Pemba, imesema imejipanga kikamilifu, ili
kuhakikisha barabara ya Kipapo- Mgemelea hadi Wambaa yenye urefu wa kilomita
9.3 inamalizika kwa kiwango cha lami, katika bajeti kuu ya mwaka 2022/2023.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mdhamini wa wizara hiyo
Pemba Ibrahim Saleh Juma, wakati akizungumza na mwandishi w ahabari hizi, juu
ya maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo.
Alisema, wizara imeshajipaga kikamilifu ili kuona ndani
ya bajeti yake kuu ya mwaka 2022/2023, fedha zilizotengwa zinatumika na
kukamilika kwa kiwango cha lami.
Alieleza kuwa, kwa sasa tayari jumla ya kilomita 5.5 za
barabara hiyo imeshawekea lami nyepesi ‘primer’
yenye leya tatu, ambayo ni kutoka Kipapo hadi Mgelema.
‘’Kutoka ilipoanzia
eneo la Kipapo hadi kijiji cha Mgelema, yari kumeshawekewa lami nyepsi na
ambapo sasa iko tayari kuwekewa lami moto na kikokoto zake
nyembamba,’’alieleza.
Hata hivyo Afisa Mdhamini huyo alisema, katika barabara
hivyo zipo daraja nne, ambapo mbili ni kubwa na moja imeshakamilika ujenzi wake
na nyingine ikiendelea.
Kuhusu kilimita zilizobakia, alisema kilomita 1,
imeshasafishwa kutoka eneo la kijiji cha Mgelema hadi Wambaa, ambapo kazi hiyo
kwa sasa imesimama kutokana na ujenzi unaoendelea wa daraja.
Hata hivyo amesema
kwa sasa wanaendelea na matengenezo ya mtambo wa kusagia kokoto, ambao
uliharibika hivi karibuni, na mara utakapotengenea wataanza kazi ya uwekaji
kokoto nyepesi kwenye barabara hiyo.
‘’Lakini pia kazi nyingine ambayo tunaweza kuirudia ni
uwekaji wa lami nyepesi ‘primer’ kwa yale maeneo ambayo
yamesharibika kutokana na kukaa kwa muda mrefu,’’alifafanua.
Baadhi ya wannachi wanaoitumi barabara hiyo, wameiomba
wizara kuharakisha ujenzi wake, ili waitumie kwa uhakika kuanzia Kipapo,
Mgelema hadi Wambaa.
Othman Mjaka Nassro wa Mgelema walisema, bado changamoto
ni kutomalizika kwa wakati, hali ambayo inampa hofu wa kusimama kwa ujenzi wake
na kurudi tena kwenye shida.
Kaije Ali Said na Mwanahama Amour Ali walisema ni vyema
ujenzi ukaharakishwa, ili waweze kuitumia hadi Wambaa hata kipindi cha mvua.
Akiwasilisha
malengo ya bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022, waziri wa wizara hiyo Khalid
Salum Mohamed, alisema mradi
huo ulipangiwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni 2.203, ambapo hadi kufikia mwezi
Machi, 2022 kulikuwa na shilingi bilioni 1118 sawa na asilimia 50.
Hata
hivyo alisema, mwaka huu wa fedha wa 2022/2023, alisema Wakala wa barabara
Zanzibar, imepanga kuzijenga na kuzifanyia matengenezo barabara mbalimbali kwa
kiwango cha lami za Unguja na Pemba.
Alieleza
kuwa barabara hizo, zitakazogharamiwa na Mfuko wa barabara Zanzibar ni ujenzi
wa barabara ya Tumbatu yenye urefu wa kilomita 9, kuendelea na ujenzi wa
barabara ya Kipapo – Mgelema – Wambaa yenye urefu wa kilomita 9.3 pamoja na
uwekaji wa lami katika barabara ya Kijangwani – Birikau Pemba yenye urefu wa
kilomita 4.2.
Mwisho
Comments
Post a Comment