NA HAJI NASSOR, PEMBA:::::
MAHAKAMA ya Mkoa Wete, leo itaendelea
tena na shauri la ubakaji linalomkabili, daktari Is-haka Rashid Hadid, wa Kituo
cha Afya Gombani, baada ya wiki iliyopita kupelekwa rumande.
Leo,
Mahakama hiyo maalum ya makossa ya udhalilishaji, chini ya Hakimu Ali
Abdur-haman Ali,inatarajia kuwasikiliza mashahidi wa upande wa mashtaka, ambapo
awali ilidaiwa upelelezi umeshakamilika.
Mtuhumiwa
huyo ambae ana makosa manne, matatu ni kudaiwa kumbaka mtoto mwenye 16 na la
pili ni kumtorosha kutoka kwenye himaya ya wazazi wake.
Awali akisoma
hati ya mashtaka, Mwendesha Mashtaka kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Juma
Mussa, alidai kuwa, mtuhumiwa huyo
alimbaka mtoto huyo, ambae yuko chini ya uangalizi wa wazazi wake.
Alidai kuwa,
baina ya Aprili 21, mwaka huu mtuhumiwa huyo alimtorosha mtoto huyo, kutoka
nyumbani kwao Gombani wilaya ya Chake chake mkoa wa kusini na kumpeleka nyumbani
kwake Kangagani wilaya ya Wete.
Ambapo baada
baada ya kumtorosha, usiku wake alianza kumbaka na kuendelea kumfanyia kitendo
hicho kwa siku tatu tofauti.
‘’Mtuhumiwa
umetenda makosa manne, kwa mtoto mwenye miaka 16, moja ni kumtorosha na pili
ulimbaka mara tatu, wakati akiwa nyumbani kwako, eneo la Kangagani wilaya ya
Wete mkoa wa kaskazini Pemba,’’alidai.
Mara baada
ya kusomewa mashtaka yake, mtuhumiwa huyo chini ya wakili wake Abeid Mussa, aliulizwa
na Hakimu wa makosa ya udhalilishaji Ali Abdur-haman Ali, ikiwa anakubali ama
laa.
‘’Umeyaskia
makossa yako vyema, kama yalivyosomwa na Mwendesha mashtaka, kama jawabu ndio unakubali
ama unakataa,’’alimuuliza mtuhumiwa Hakimu huyo.
Mtuhumiwa
huyo alikana tuhuma hizo, na kuiomba mahkama hiyo kumpa dhama kwa masharti
nafuu, ombi ambalo halikuzingatiwa mahakamani hapo.
Ndipo Hakimu
wa mahkama hiyo, alipoliahirisha shauri hilo hadi leo Juni 1, mwaka huu, na
mtuhumiwa alipelekwa rumande.
Kufanya
hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 113 (1) (a) cha sheria ya Adhabu nambari 6
ya mwaka 2018, sheria ya Zanzibar.
Kosa la pili
kwa mtuhumiwa huyo baada ya kumtorosha mtoto huyo, siku hiyo hiyo majira ya saa
3:00 usiku alimbaka, ambapo ni kinyume na kifungu cha 108 (1), (2), (e) na 109
(1) cha sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018.
Kosa la tatu
ambalo lilitokea Aprili 22 na la nne ambalo lilitokea Aprili 23, mwaka huu pie,
alilitenda kwa nyakati tofauti za usiku, ambapo alidaiwa kumbaka mtoto huyo.
Ambapo pia
kufanya hivyo, ni kinyume na kifungu cha 108 (1), (2), (e) na 109 (1) cha
sheria ya Adhabu nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.
Mwisho
Comments
Post a Comment