NA MWANDISHI WETU, PEMBA::____------
JANA Mei 26, 2022, wasaidizi wa
sheria kutoka majimbo 18 ya uchaguzi kisiwani Pemba, wamemaliza na kisha
kutunukiwa vyeti vyao, baada ya kumaliza mafunzo ya siku 15 ya wasaidizi wa
sheria.
Aliyekabidhi
vyeti hivyo, kwenye hafla iliyofanyika Gombani Chake chake, alikuwa Afisa Mdhamini
Afiri ya Rais, Katiba, Sheria, Utamishi na Utawala Bora Pemba, Hali Ali Khamis.
Kwenye
hutuba yake, aliwataka wasaidizi hao wa sheria, kwenda kuisadiai jamii, ili
kupunguza majanga kama ya udhalilishaji, dawa za kulevya, migogoro ya ardhi na
ndoa.
Hata hivyo
aliwataka wasibweteke na elimu ya awali ya sheria walioipata, na badala yake,
wabuni mbinu za kujiendeleza ili kupanua wigo, wa utoaji msaada wa kisheria.
Aidha
aliipongeza Idara ya Katiba na Msaada wa Kisheria Zanzibar, kwa kuendelea
kuijengea uwezo wa kisheria jamii ya Zanzibar.
Mkurugenzi
wa Idara hiyo Zanzibar Hanifa Ramadhan Said, alisema pamoja na kumalizika kwa
mafunzo hayo ya awali, Idara itaendelea kuwajengea uwezo, wasaidizi hao wa
sheria.
Alisema,
waliharakisha kuwapa elimu wasaidizi hao wa sheria wapya, ili wende vijijini
kuisaidia jamii, na kisha mafunzo mengine yatafuata.
Hata hivyo,
aliipongeza tasisi ya LFS, kwa kuendelea kuwaunga mkono katika mradi wa
Kuimarisha upatikanaji haki Zanzibar, ambapo mafunzo, hayo ni sehemu ya
utelezaji wa mradi huo.
Kwa upande Afisa
sheria wa Idara ya Sheria Zanzibar Ali Haji Hassan, alisema wasaidizi hao wa
sheria, walikuwa jasiri na anaamini, wamepata elimu waliyopewa.
‘’Jamii
inawasubiri kwenda kuwapa elimu ya kisheria, ushauri na hata msaada wa
kisheria, lakini silaha pekee ni kujisomea zaidi,’’alisema.
Naibu Mkuu
skuli ya sheria Zanzibar -Utawala Khamis Juma Mwalimu, alisema wataendelea
kushirikiana na Idara ya Katiba na Massada wa Kisheria Zanzibar, katika kutoa
utaalamu.
Mapema
wakisoma risala yao, wahitimu hao waliiomba Idara kuharakisha kupatiwa mafunzo
nyongeza, ili kuongeza uwelewa wao wa siku 15.
Walisema, ni
vyema kukaandaliwa kwa sheria nyingine kama ZSSF, mabaraza ya miji na hifadhi
ya wazee, ili kuzifahamu kwa kina, wakati wanapotoa msaada wa kisheria.
Hata hivyo,
aliiomba kutengenezewa vitambulisho maaluma, na kuandaliwa zira za kimafunzo,
kisiwani Unguja ili kbadilishana uzoefu na wenzao.
Mahafali
hayo ya wasaidizi wa sheria ni ya kwanza, yakisimamiwa na Idara ya Katiba na
Msaada wa Kisheria Zanzibar.
Mradi wa
wasaidizi wa sheria, ulianzishwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, mwaka
2007, ambapo kwa sasa wapo wasaidizi wa sheria zaidi ya 290 kwa Unguja na
Pemba.
Mwisho
Comments
Post a Comment