NA HAJI NASSOR, PEMBA
NAIBU Mkuu wa skuli ya sheria
Zanzibar ‘Zanzibar school of law’ kitengo cha taaluma, Msemo Mavare amewataka
wasaidizi wa sheria kisiwani Pemba, kujiendeleza na kuwa wanasheria kamili,
mara watakapomaliza mafunzo yao ya awali.
Alisema,
bahati ya kuingia kwenye usaidizi wa sheria ni mwanzo, hivyo ili isiwe mwisho,
lazima wajiewekee mpango wa kujisomea sheria zaidi hapo baadae.
Naibu huyo
aliyasema hayo Gombani Chake chake Pemba, wakati akizungumza na wasaidizi wa
sheria tarajali, kwenye mafunzo ya siku 15 yanayoendelea, ambayo yameandaliwa
na Idara ya Katiba na Msaada wa kisheria Zanzibar.
Alisema,
wapo wanasheria na mawakili hapa Zanzibar, ambao mwanzo wao, walianzia kuwa
wasaidizi wa sheria, na wamepanua wigo wa kutoa huduma zaidi kwa jamii.
Alieleza
kuwa, kada ya sheria, imekuwa tegemeo kubwa jamii ya watu maskini na wale
wasiokuwa na uwelewa wa kujua misingi ya haki zao kisheria.
‘’Nyinyi
wasaidizi wa sheria, mhakikishe mnajiendeleza kielimu hapo baada ya kumaliza
mafunzo haya, maana elimu na hasa ya sheria ina uwanja mpana,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine, Naibu huyo mkuu wa skuli ya sheria Zanzibar kada ya taaluma, alisema
jambo jengine muhimu la kuzingatia, ni kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi.
Hata hivyo,
amewataka wasaidizi hao wa sheria tarajali, kuthamini nafasi hizo, kwani
walioomba kwa Pemba pekee, walikuwa zaidi ya 200 na kupatika 18 kutoka kila
jimbo la uchaguzi.
Kwa upande
wake Afisa sheria kutoka Idara ya Katiba na msaada wa sheria Zanzibar, kisiwani
Pemba, Bakari Omar Ali, alisema kazi ambayo iko mbele yao, wasaidizi hao wa
sheria, ni kujitolea zaidi.
‘’Muelewe
kuwa, mnakwenda kuisaidia jamii, ambayo wakati mwengine imeshakata tamaa, hivyo
hakuna malipo ambayo unaruhusika kumdai, hata kama atapa mabilioni ya
fedha,’’alieleza.
Akiwasilisha
mada ya sheria nambari 7 ya mwaka 2018 ya Mwenendo wa Makosa ya Madai Zanzibar,
wakili wa kujitegemea, Zahran Mohamed Yussuf, alisema huo ndio msingi mkuu wa
kesi za madai.
Alieleza
kuwa, msingi mkuu wa kudai haki kupitia hati ya madai, inajumuisha, jina kamili
la mdai ‘Plaintiff’, anuwani kamili, kinacholalamikiwa.
‘’Lakini
hata kwa anayedaiwa ‘defendant’ nae baada ya kupokea
wito, atakakiwa kujibu kipengele kimoja baada ya chengine kwa nambari, na kisha
atatakiwa kuwasilisha mashahidi,’’alieleza.
Nae wakili
wa sherikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka Juma Ali Juma, aliwataka
wasaidizi hao wa sheria, kuwa makini kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya
wasaidizi hao tarajali, walisema mafunzo hayo watayafanyia kazi ipasavyo, ili
kuona jamii iliyowazunguruka inanufaika na mafunzo hayo kwa kina.
Juma Seif
Juma wa jimbo la Chonga, Abdalla Saleh Issa Mkoani, Omar Abdalla Nassor wa
jimbo la Pandani na Habib Chapa Hamad wa Jimbo la Micheweni walisema, bado
jamii inahitajia elimu juu ya kujua haki zao za kisheria.
Mafunzo hayo
ya siku 15 yalioanza Mei 12, mwaka huu yameandaliwa na Idara ya Katiba na
Msaada wa kisheria Zanzibar, yalifadhiliwa na LSF na mada kadhaa zilijadiliwa
ikiwa ni pamoja na mirathi, jinai, sheria za ardhi, dhana ya wasaidizi wa sheria
na maadili.
Mwisho
Comments
Post a Comment