NAIBU Waziri wa Maendeleo wa Jamii Jinsia Wazee na Watoto Anna Athanas Paul amesema iwapo mtoto wa kike atasoma kwa bidii ataweza kuviepuka viashiria vya unyanyasaji ambavyo ndio vikwazo vikubwa vinavyowafanya kutokufikia malengo yao.
Ameeleza jayo katika maadhimisho ya siku ya
kimataifa ya mtoto wa kike huko katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar
(SUZA) Kampas ya Maruhubi Unguja.
Amesema watoto wa kike
wakisoma kwa bidii itasaidia kutimiza malengo yao ya baadae hali ambayo itasaidia
kujiepisha na vitendo viovu ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia.
“Iwapo mtoto wa kike atasoma kwa
bidii ataweza kuviepuka viashiria vya unyanyasaji ambavyo ndio vikwazo vikubwa
vinavyowafanya kutokufikia malengo yao” Amesema Waziri huyo.
Naibu Waziri huyo amefahamisha kuwa kwa mujibu takwimu kutoka Afisi ya Mtakwimu Mkuu mwaka 2023 matukio 1954 ya ukatili na
udhalilishaji yaliripotiwa kati ya matukio hayo wasichana walikuwa 1263 sawa na
aslimia 77.1 hiyo inaonesha bado watoto wa kike wanahitaji elimu kwa nguvu
zote.
Kwa upande wa watoto walioshiriki katika maadhimisho hayo akizungumza
Fatma Salum (16) kutoka Skuli ya Msingi ya Tumekuja amesema ni vyema wazazi na walezi wakatenga muda maalum wa
kuzungumza na watoto ili kuyajua mambo wanawakwaza katika mazingira
yaliyozunguuka.
Naye Mtaalam wa elimu kutoka Shirika la Kusaidia Watoto Duniani
kanda ya Tanzania Henry Tindwa amesema Save the Children itaendelea
kusaidia watoto kujielewa ili kupunguza wimbi la udhalilishaji na watoto
kujielewa.
Siku ya mtoto wa kike huadhimishwa kila mwaka ifikapo Oktoba
11 na Kauli mbiu ya mwaka huu: Muezeshe mtoto wa kike,apaze sauti yake.
mwisho.
Comments
Post a Comment