Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Abeida
Rashid Abdallah amesema Wizara hiyo itaendelea kusimamia maendeleo ya jamii
ikiwemo kundi la watu wenye ulemavu ili kuona wanaishi katika mazingira mazuri
na salama.
Akizungumza kwa niaba ya katibu mkuu huyo Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji
na Utumishi Dkt. Salum Khamis Rashid wakati akikabidhi visaidizi vya watu
wenye Ulemavu kwa Taasisi ya Maisha Bora Fondation, katika ukumbi wa Wazee
Sebleni.
Dkt Salum alivitaja visaidizi hiyo ikiwemo na lotion 72 kwa ajili ya watu wenye
ulemavu wa ngozi ALBINO, fimbo nyeupe 20 kwa ajili ya watu wenye ulemavu
wa uoni, pamoja na viti vya magurudumu mawili 30 (Wheel chair) kwa ajili ya
watu wenye ulemavu wa viungo
Alisema Wizara itaendelea kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili
wananchi kadiri hali itakavyoruhusu ili kuhakikisha hakuna kundi ambalo
limeachwa nyuma.
Alieza kwamba moja kati ya jukumbu la Wizara hiyo ni kujenga ustawi mzuri
kwa jamii hivyo Wizara hiyo itaendeleo kutatua changamoto za watu wenye
ulimavu na makundi mengine iliwaondokane na changamoto hizo.
“Wizara inaelewa changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu na makundi
mengine katika jamii lakini hali itakavyokuwa inaruhusu, Wizara itaendelea
kutatua changamoto hizo” alisema Dkt Salum
Naye mwakilishi kutoka Maisha Bora Foundation Mohammed Nyahega amesema
watu wenye ulemavu bado wanahitaji vitu vingi ili waweze kuishi vizuri. Hivyo
msaada uliyotolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto
utasaidia kutatua baadhi ya changamoto zao.
Aidha ameishukuru Wizara hiyo pamoja na kuahidi kwamba visaidizi
alivyokabidhiwa atavifikisha kama alivyopewa bila ya kwenda kinyume na
hatimae vitawafikia walengwa kama Wizara ilivyokusudia kuendeleza kujenga
Ustawi wa Jamii.
Visaidizi hivyo vimetolewa na Ubalozi wa Kuwait kwaajili ya kuendeleza
mashirikiano mazuri na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Comments
Post a Comment