NA
HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
NOVEMBA
3 ya miaka mitatu iliyopita, ilikuwa ndio siku ya kwanza ya Rais mpendwa wa
Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuwasili ndani ya Ikuklu ya Zanzibar.
Kwa
wakati huo, hakuwasili akitokea nchi jirani..laaahasha alitokea kwenye viwanja
alivyokula kiapo, kushika hatamu ya uongozi.
Maana Dk. Mwinyi, baada ya kumalizika kwa kampeni za
zaina yake, zilizotajwa kama za kisayansi kwa kule kukutana na makundi mbali
mbali, kisha wananchi walimpigia kura.
Baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa vyama vingi,
Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC, ilimtangaaza Dk. Mwinyi kuwa rais wa Zanzibar
kwa kupata asilimia 76.27 na kuwaacha mbali wagombea wenzake.
‘’Nimepokea ushindi kwa mikono miwili na nawashukuru
wananchi wa Zanzibar kwa kunichagua mimi na chama changu, kwa miaka mitano
ijayo,’’alisema wakati huo.
Kwa wananchi Zanzibar, kama alivyosema Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa kaskazini Pemba Mberwa Hamad Mberwa, kuwa duniani viongozi kama
aina ya Dk. Mwinyi ni wachache.
Maneno kama haya, yaliwahi kusemwa pia na Mbunge
viti Maalum mkoani humo, Asya Sharif Omar, kuwa Zanzibar mwaka wake wa kuneemeka
ni awamu ya Dk. Mwinyi.
Haya, yanakuja kudhihirishwa leo akiwa ndani ya
miaka mitatu ya uongozi wake, maana baada ya kuwaahidi wananchi, juu ya
utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.
KULIINUA ZAO LA MWANI
Alikuwa, akinukuu mara kwa mara juu ya kuliimarisha
na kilipima eneo la Chamanangwe kwa Pemba, pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kusarifiwa
mwani
Na haya pamoja na mengine, kumbe yamo ndani ya Ilani
ya CCM ya mwaka 2020/2025, kwenye Ibara ya 156 (e) na (m), ambayo imeelekeza
kuanzishwa viwanda vya kusarifia biadhaa ikiwemo za mwani.
Kwenye hili Dk. Mwinyi hakuwa tu akisema kwa matakwa
yake, kumbe hata lile la uchumi wa buluu lipo kwenye Ibara ya 162 kwenye
vifungu vidogo vya (c) na (e) ilielezea namna bora ya kuyatumia mazao ya
baharini kama mwani, kuwa chachu ya maendeleo.
Haya wakati anayanadi, wapo wasiomfahamu Dk. Mwinyi
kuwa wala asingeweza kulipandisha hadhi zao la mwani, kama vile alivyoahidi
wakati wa kampeni.
LEO NDANI YA MIAKA MITATU
Mkurugenzi mkuu Kampuni ya mwani Zanzibar Massoud
Mohamed Rashid, anasema ujenzi wa kiwanda hicho, umekamilika.
Ujenzi huo ambao ulikuwa unajengwa na Kikosi Maalum
cha Kuzuia Magendo Zanzibar ‘KMKM’ kwa awamu ya kwanza, kati ya zile tatu,
umeshakamilika wote.
Zuri ni kuwa, ujenzi huo wa kiwanda cha kusafiria
mazao yatokanayo na mwani, unasimamiwa na Mshauri elekezi, kutoka Wakala wa
Majengo Zanzibar.
Mkurugenzi anasema kuwa, awamu ya kwanza ilijumuisha
ujenzi wa jengo kuu la kiwanda, ujenzi wa ghala pamoja na uzio maalum, kwa
ajili ya kulihifadhi eneo hilo.
Na awamu hii ya kwanza, kumbe imepangwa kukamilika
ndani ya mwaka huu, kabla ya kuanza kwa awamu ya pili, ya ujenzi wa kiwanda
hicho.
Maana awamu hii ya kwanza, ilishaanza tokea mwezi
Julai mwaka 2022, ambapo kwa sasa umefikia asilimia 100.
‘’Awamu pili ulijumuisha ujenzi wa maeneo ya
bustani, ufungaji wa mitambo husika na awamu ya tatu ni kuanza uzalishaji
bidhaa, zitokanazo na zao la mwani,’’anafafanua.
Yeye anasema, ndani ya miaka mitatu ya Dk. Mwinyi,
wakulima wa zao la mwani kisiwani Pemba, waanze kukaa mkao wa kula, kwani sasa
mwani utaongezeka thamani.
‘’Kwa hakika aliyofanya Dk. Mwinyi hapa Chamanangwe
ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 kwa vitendo, sasa huku ndio
kuwainua wananchi kiuchumi kwa vitendo,’’anasema.
Baada ya kukamilika kwa ujenzi huo, shughuli za
kutafuta na kufunga mashine zinatarajiwa kuanza, na kukamilika kwa kazi hiyo,
kutawezesha kazi za kusarifu mwani, kuanza.
Kwa wakati huo ujenzi huo wa awamu ya kwanza, ukitarajiwa
kutumia shilingi bilioni 8.2 ingawa wakati ulipotembelewa na mwenge wa uhuru,
ulishatumia shilingi bilioni 4.024 na utakapomalizika wote, utagharimu shilingi
bilioni 13.
‘’Mradi huu wa kiwanda, utakapomalizika utakuwa na
uwezo wa kusarifu mwani tani 30,000 kwa mwaka, ambapo umiliki wake kwa asilimia
55 utakuwa serikalini na asilimi 45 utakuwa wa kampuni ya Nutri-san,’’anasema
Mkurugenzi.
Hapa Mkuu wa wilaya ya Wete Dk. Hamad Bakar Omar,
anaamini kuwam, mradi huo mkubwa na wa aina yake, utakuwa na tija mara mbili.
Moja ni ajira za muda na kudumu, sambamba na zao la
mwani, sasa kupata hadhi, kwa kule kuongezeka bei, ikilinganishwa na iliyopo
sasa.
‘’Naamini, kiwanda hichi kinakuja kuwa mkombozi kwa
wakulima wa mwani, ambao wengi wao ni wanawake, hivyo ni wajibu kukitunza,’’anasema.
Anasema ambae haoni aliyoyafanya Dk. Mwinyi ndani ya
miaka mitatu, afike ndani ya wilaya yake na hasa eneo la Chamanagwe, ataona
kazi iliyofanywa kwa vitendo.
Mkuu huyo wa wilaya anasema, kasi aliyokuja nayo Dk.
Mwinyi na akimaliza kipindi cha miaka yake mitano, hakutakuwa na eneo, ambalo
hajaligusa kwa uwekezaji mkubwa.
‘’Sisi wananchi wa wilaya ya Wete, na hasa wakulima
wa mwani, sasa tumefarajika mno, maana yale aliayoaahidi Dk. Mwinhyi, sasa
yanaonekana kwa vitendo, hongera miaka mitatu,’’anasifia.
Hivi karibuni, Mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba
Salama Mbarouk Khatib, akizungumza na vyombo vya habari, alisema mradi huo,
haujawahi kutokea hasa kwa ukubwa na umuhimu wake.
‘’Kila mmoja ni shahidi kuwa, wakati rais wa sasa wa
Zanzibar Dk. Hussein Ali Mwinyi akipeperusha bendera ya chama chake, aliahidi
ujenzi wa kiwanda hicho, leo upo,’’anafafanua.
WAKULIMA WA ZAO MWANI
Salama Makame Mchakwe wa Tumbe, anasema sasa ni
jambo la kujivunia, kwa mradi huo mkubwa ndani ya mkoa wa kaskazini Pemba, kwa miaka
hii mitatu ya Dk. Mwinyi.
Anasema, wapo baadhi yao na kwa wakati huo, walishindwa
kuamini, juu ya ujenzi wa kiwanda hicho, kwani walishazoea kuelezwa, ahadi kama
hizo.
‘’Leo tukiwa ndani ya shamra shamra za kutimia miaka
mitatu ya uongozi wa Dk. Mwinyi, nasisi wakulima wa zao la mwani, tunalo tena kubwa
la kujivunia,’’anasema.
Hata Maryam Haji Bakari na mwenzake Aisha Issa Ali
wanaolima mwani Tumbe, wanaona kama vile sasa, wamepata mkombozi, pindi kiwanda
hicho kitakapomalizika kufungwa mashine.
‘’Kwa hakika, kiongozi
mkweli hupimwa kwa kauli zake na vitendo, leo ndani ya miaka mitatu, tokea Dk.
Mwinyi aingie ikulu, sasa Chamanagwe panan’gaa maana kiwanda kinasubiri
ufungaji wa mashine tu,’’wanasema.
Afisa Uvuvi Wilaya ya Micheweni Abdalla Issa Nassor, anakiri kuwa wakulima
zile changamoto kadhaa na nyingine zilizokuwa zikiwakabili wakulima hao, sasa
watafutwa jasho ndani ya miaka hii mitatu ya Dk. Mwinyi.
‘’Walishapita viongozi
wengine, lakini hawakuumwa na zao la mwani, lakini Dk. Mwinyi ndani ya miaka
mtatu, mambo yanang’aaa,’’anasema.
Eneo jingine imeelezwa
na Kaimu Mratibu wa kampuni ya mwani ya Serikali Zanzibar (ZSCO)Pemba Khadija
Zahran Mohamed kuwa, kampuni ya mwani ya serikali, imekuja kuondosha manyanyaso
wanayoyapata wakulima wa zao hilo.
Anasema wapo wakulima
walifika kuambiwa mwani wao ni mpeta, sababu sio wakulima wanaosaidiwa vifaa na
kampuni hiyo, hali iliyopeleka kushindwa kununuliwa.
“Wapo waliopatiwa vifaa
vya kulimia na kubeba mwani, hawa sasa wanapaswa kulima kwa wingi, wale ambao
bado tutahakikisha kupitia kampuni hii, nao wanapatiwa,’’anaeleza.
Aliwataka wakulima hao
kuhakikisha wanashirikiana na serikali, pale itakapoanza kunua mwani, huku suala
la bei linaweza kubadilika, kama ilivobadilika awali kutoka shilingi 700 hadi
shilingi 1000 na inaweza kufikia hata shilingi 2000 kwa kilo moja
Wakati huu kiwanda
kikiwa hakijaanza kusarifu bidhaa za mwani, usafirishaji wa zao la hilo,
nje ya nchi umeongezeka, kutoka tani 11,383 mwaka 2020 hadi tani 12,124 mwaka
2021 sawa na ongezeko la asilimia 6.1.
Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, imeanisha kuwa, uzalishaji
wa zao la mwani, umeongezeka kutoka, tani 10,531 kwa mwaka 2021, hadi tani
12,594 kwa mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 20.
Taarifa ikafafanua kuwa, usafirishaji wa mwani nje ya nchi umeongezeka
kutoka tani 12,124 kwa mwaka 2021 hadi tani 13,972 mwaka 2022, sawa na ongezeko
la asilimia 15.
Kama hivyo ndivyo, hongera Dk. Mwinyi, hongera miaka mitatu ukiwa ikulu
na hongera CCM kumpa kijiti Dk. Mwinyi.
Mwisho
Comments
Post a Comment