NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
MBUNGE wa Viti maalum mkoa wa kaskazini Pemba Alhajjat
Asiya Sharif Omar, amewakumbusha wazazi na walezi, wenye watoto wao Almadrassatul-Qamariyya
ya Wete, kulipa ada za watoto wao kwa wakati, ili kuwapa uhakika waalim
kufundisha kwa ufanisi.
Alisema,
maendeleo yaliopo katika madarassa hiyo, hayakuja bure, hivyo ili yawe endelevu,
hakuna budi kwa wazazi na walezi kujikumbusha namna ya ulipa ada.
Mbunge
huyo aliyasema hayo, ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi Wete, kwenye
mahafali yalioambatana na siku ya wazazi kwa madrassa hiyo.
Alisema,
maendeleo endelevu katika madrassa hiyo, hayatokuja kwa haraka na kudumu, ikiwa
wazazi watapuuzia suala la ulipa ada kwa watoto wao.
Alieleza
kuwa, madarassa hiyo haina mfadhili wala ruzuku kutoka serikalini, hivyo na
inategemea moja kwa moja ada kutoka kwa wazazi na walezi, wenye watoto wao
katika madrassa hiyo.
“Nichukuwe
nafasi hii, kuwasisitiza wazazi na walezi kuhakikisha wanalipa ada zao kwa
wakati, kwani hizo ndio zinazotegemewa na waalimu, kuendesha madrassa hiyo, na
kinyume chake, ni kudhoofisha malengo husika,’’alieleza.
Katika
hatua nyingine Mbunge huyo, amewataka wazazi na walezi, kufuatilia kwa karibu maendeleo
ya elimu kwa watoto wao, ikiwemo kujenga ushirkiano endelevu kati yao na waalimu
na kamati husika.
Aidha
Mbunge huyo wa viti maalum, ameikumbusha jamii, kuwa watoto wana haki mbali
mbali, ikiwemo kusikilizwa, kupatiwa elimu bora, kucheza pamoja na kulindwa na
majanga.
Wakati
huo huo Mbunge huyo, aliongoza harambee, kwa ajili ya ununuzi wa bati ya kuezekea
madraasa hiyo, na kupatikana shilingi 300,000 nae kisha kuchangia shilingi
500,000 katika hafla hiyo.
Hata
hivyo alisema, atachangia bati kadhaa kwa ajili ya kazi hiyo, mara baada ya
kamati ya madrassa hiyo, kumpa taarifa rasmi.
Awali
alikabidha zawadi mbali mbali kwa washindi wa masomo mbali mbali katika madarassa
hiyo, samba mba nae kukabidhi vinywaji aina soda na biskuti kwa ajili ya wanafunzi
hao, vilivyogharimu wastani wa shilingi 650,000.
Mapema
Mwalimu mkuu wa Madrasaa hiyo ya Qamariyya Fadhila Awadhi Salimu, alimpongeza
Mbunge huyo, kwa moyo wake, wa kuwa karibu na mdau mkuu wa maendeleo ya elimu.
Alisema, Mbunge huyo amewakua akishirikiana na jamii kila wakati, bila ya kujali nafasi yake, jambo ambalo linawapa wigo mpana wa kuendesha shughuli zao.
“Tunaomba viongozi wetu wote wawe mfano wa kama alionao Mbunge wetu huyu, kwanza hana majivuno, pili ni mpenda maendeleo ya watoto na amekuwa mdau mkuu wa elimu,’’alieleza.
Akisoma
risala ya wanafunzi katika madrassa hiyo, mwanafunzi Saleh Ibrahim, alisema kwa
sasa madrassa hiyo, inakabiliwa na uchakavu wa majengo.
Alisema
changamoto nyingine ni baadhi ya wazazi na walezi, kuwa wazito wa kulipa ada
zao, jambo linalochangia kuongeza uzito wa kuiendesha madrassa hiyo.
Katika
hafla hiyo, wanafunzi hao walionesha vipaji mbali mbali ikiwemo, sira, ngonjera,
wimbo wa ukaribisho, namna ya kufuata kwa vitendo hadithi za Mtume Muhammad (S.A.W)
pamoja na jukumu la wazazi katika malezi ya pamoja.
Mwisho
Comments
Post a Comment