KAMANDA
wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi kamishina
Msaidizi wa Polisi Richard (ACP),
Thadei
Mchomvu, amewataka wazazi na walezi
kushirikiana kwa pamoja katika kuwalea na kuwatunza watoto wao kwa ajili
ya kuwalinda na vitendo vya ukatili na udhalilishaji.
Akizungumza
na mwandishi wa gazeti hili ofisini kwake Muembe Madema Mjini
Zanzibar, amesema baadhi ya wazazi hushughulikia
shughuli zao zaidi na hawana utamaduni wa kuwa
karibu na watoto wao jambo ambalo hupelekea
kuendelea vitendo hivyo.
"Wapo
wazazi wakitoka asubuhi ndo wametoka kurudi kwao ni usiku watoto
wakiwa wamelala, mtindo ambao unachangia watoto kukosa elimu ya kujitambua iliyo muhimu katika kuwasaidia kuepuka
kufanyiwa vitendo viovu vya kudhalilishwa," alisema
Richard
"
Na baadhi ya kina mama wanawacha watoto kudhurura ovyo bila ya kuwavisha nguo
kamili na kupelekea mtoto kufanyiwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji."
Aliongezea Richard
Aidha
alisema kuna faida mbalimbali zinazopatikana wazazi wakishirikiana kwa pamoja
katika kumlea watoto wao.
"Ushirikiano
wa wazazi katika malezi ya mtoto huwezesha kugawana majukumu na mzigo wa kumlea
mtoto. Hii inamaanisha kuwa mzazi mmoja hatakuwa na jukumu kubwa la kumlea
mtoto peke yake, na hivyo kupunguza shinikizo na mafadhaiko ya mzazi mmoja,
ushirikiano wa wazazi unaweza kuongeza uhusiano mzuri na mawasiliano kati yao,
ambayo ni muhimu katika kujenga familia yenye furaha na imara".alisema
Richard
"Faida
nyingine ya wazazi kushirikiana katika malezi ni kwamba inawezesha mtoto kupata
upendo na huduma kutoka kwa wote wawili. Mtoto anapopata upendo na huduma
kutoka kwa wazazi wote, anajenga uhusiano wa karibu na wote wawili na hivyo
kuimarisha hisia za usalama na utulivu. "aliongezea Richard
Pia
alisema takriban asilimia
80% ya matukio ya ubakaji ambayo
yamehusisha mabinti chini ya miaka kumi
na mmoj 11 hadi kumi na saba 17.
“Jumla
ya matukio ya kubakaji 285,katika matukio hayo watoto wenye umri 0-10 walikuwa
30,mabinti kuanzia miaka 11hadi 17 walikuwa 232, na wasichana kuanzia miaka 18 na kuendelea
walikuwa ni 23." alisema Richard.
Comments
Post a Comment