NA HAJI NASSOR, ARUSHA@@@@
WANACHAMA wa Baraza la Habari
Tanzania MCT, wamemrejesha tena Rais wa Baraza hilo, Jaji Mstaafu: Juxon Isaac Mlay kwa miaka
mengine mitatu ijayo, kupitia mkutano mkuu wa 25, uliofanyika Septemba 28, 2023
mkoani Arusha.
Mkutano huo,
pia umemchagua Yussauf Khamis Yussuf kuwa Makamu wa rais na wingine waliochaguliwa katika mkutano huo
ni wawakilishi wa vyombo vya habari, akiwemo Tido Mhando.
Wawakilishi
wingine ni Rose Rouben, Ali Haji Mwadini samba mba na kupatikana kwa
wawakilishi watatu, kundi la umma wakiongozwa na CPA: Happiness Nkya, Jaji
Robert Makaramba na Mwajaa Said.
Akizungumza
mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo, rais aliyerejea tena madarakani
Juxon Isaac Mlay, alisema kasi na ari iliyokuwepo kwa miaka mitatu, ni vyema ikaongezeka.
Aliwataka
viongozi wenzake, waliorudi kutetea nafasi zao, kuhakikisha wanaendelea kufanya
makubwa, wakiwa ndani ya Baraza la Habari Tanzania, ili kuwalipa wanachama
waliowachagua.
‘’Niwaombe
wale viongozi wenzangu, tuliochaguliwa kuhakikisha tunafufua ari na kasi mpya,
ili kuendelea kulipatia maendeleo endelevu na wanachama wake Baraza letu,’’alieleza.
Katika hatua
nyingine, Rais huyo wa Baraza la Habari Tanzania alimtangaaza Ernest Sungura,
kuwa ndie anayetarajiwa kubeba mikoba ya nafasi ya Katibu Mtendaji mpya.
‘’Kwani
miezi mitatu ijayo, Katibu Mtendaji wa sasa
Kajubi Mukajanga, anatarajiwa kustaafu, hivyo tayari Bodi ya wadhamini
imeshamteua mtu, wa kushika nafasi hiyo,’’alieleza.
Katibu
Mtendaji wa MCT anayemaliza muda wake Kajubi Mukajanga, alisema anajivunia
umoja na mshikamano, aliyoupata kutoka kwa wafanyakazi wenzake, katika kipindi
cha utumishi wake.
Aidha
alisema, sasa anashukuru, wakati anamaliza muda wake, tayari MCT inayofisi, na
huku vyombo vya habari na waandishi wake, wakiwa wamepata uwelewa wa mambo
kadhaa.
‘’Lakini
kubwa zaidi, ni kuendelea kufanikisha uwepo wa utamaduni wa mashindano ya
umahiri wa waandishi wa habari, kwa miaka 14 mfululuzo sasa,’’alieleza.
Hata hivyo
Katibu huyo Mtendaji, alieleza kuwa, anaendelea kusononeshwa na wanachama wa
MCT, wasiolipa ada zao, akisema wanadhofisha baadhi ya harakati za kimaendeleo.
Akiwasilisha
ripoti ya utendaji ya MCT, Afisa kutoka baraza hilo Saumu Mwalimu, alisema
kwenye ufuatiliaji wao wa vyombo vya habari, wamegundua vyombo vya habari vya
magazeti, vimekuwa vikijibebesha kazi ya kutoa hukumu, kwenye vichwa vyao vya
habari.
‘’Kwa mfano,
vipo vichwa vya habari vinavyoandikwa na wahariri, hutoa jawabu au hukumu kwa
aina habari iliyoripotiwa, lakini na kuendesha mazungumzo yasio na tija kwa
watangaazaji wa redio,’’anaeleza.
Nae Afisa wa
MCT Paul Mallimbo, alisema wanachofanya baada ya kuona chombo cha habari,
kinakengeuka kanuni, sheria na sera za uandishi wa habari, ni kuviandikia
barua.
Wakichangia
ripoti za fedha na za utendaji, washiriki wa mkutano huo akiwemo Jabir Idrissa,
alilipongeza Baraza kwa kazi kubwa wanazozifanya, hasa za utatuzi wa migogoro.
Mwandishi
Nevile Meena, alisema kama waandishi wa habari hawafanyi habari za uchambuzi
wanaweza kuachwa nyuma na wasiosomea uandishi wa habari.
Wakati huo
huo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Kajubi Mukajanga, alisema, bado kuna
uminywaji wa habari, na kuwakosesha taarifa wananchi, kujua kinachoendelea
serikali.
Katib huyo
Mtendaji, alitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, ukumbi wa Kibo, jengo la
Mahkama ya Afrika, mkoani Arusha ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya kujua
duniani.
Alisema
ujumbe wa mwaka huu, wa unakwenda sambamba na kauli ya Waziri mkuu wa serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaaliwa Kassim Maajaliwa.
‘’Ujumbe wa
mwaka huu unaosema ‘umuhimu wa matumizi ya mitandao ya kijamii katika kupata
taarifa’ jambo ambalo linakwenda samba mba na sheria kadhaa za
habari,’’alieleza.
Kwa upande
wake Mhadhiri wa Chuo cha Kiislamu Murorogo, Rehema Twahiri, alisisitiza umoja
na mshikamano wa vitendo baina ya waandishi wa chombo kimoja na
chingine,’’alishauri.
Ne Mhadhiri
wa Chuo Kikuu Huria Tanzania ‘OUT’ Vicent Mpepo, alisema hata kama vyanzo watu
vya kutoa habari, ifikiriwe namna kwa MCT.Z2/
atika
mkutano huo mkuu wa 25 wa Baraza la Habari Tanzania MCT, ulihudhuria na
wanachama hai 54, kati ya 61 ambao hawana deniAAAA hadi mwaka 2023.
Mwisho
Comments
Post a Comment