NA HAJI NASSOR, ARUSHA
RAIS wa Mahkama ya Afrika ya haki za binaadamu na haki za watu Imani Daud Aboud, amesema kama waandishi wa habari wanafanyakazi zao chini ya vitisho kutoka kwa mamlaka kunahatarisha kudhoofisha uhuru wao na ule wa kujieleza na kutoa maoni.
Rais huyo aliyasema hayo jana ukumbi wa mahakama hiyo mkoani Arusha alipokuwa akifungua mkutano wa kikanda kwa waandishi wa habari juu ya ulinzi na usalama wao uliondaliwa na Baraza la habari Tanzania MCT.
Alisema vipo vyombo au mamlaka vimekuwa vikiingilia na kuwatisha waandishi wa habari wanpokuwa kazini jambo ambalo halisidii kuimarisha uhuru wa kujieleza na ule wa habari.
Alieleza kuwa, haki ya kupata na kusambaaza habari ni haki ya kikatiba hivyo ni kosa kwa mamlaka nyingine kuviingilia vyombo vya habari pasi na dai la haki.
'Waandishi wa habari ni sauti ya wsiokuwa na sauti na ni sauti kwa waliokata tamaa hivyo ni jukwaa muhimu na linapaswa lilindwe na sio kushambuliwa,'alieleza.
Katika hatua nyingine rais huyo wa mahakama ya Afrika ya haki za binaadamu na haki za watu Imani Daud Aboud amewakumbusha waandishi hao wa habari kufanya kazi zao kwa kufuata sheria za kihabari na misingi ya kazi zao.
Hata hivyo ameupongeza uongozi wa Baraza la habari Tanzania MCT kwa juhudi zao za kuendelea kuwaelimisha wandishi wa habari juu ya ulazima wa kuzijua sheria wanazozifanyia kazi.
Mapema Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Tanzania Kajibu Mukajanga alisema mkutano huo ni muendelezo wa mikutano yenye lengo la kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika kazi zao.
Alieleza kuwa mkutano ambao uliokusanya waandishi wahabari nguli kutoka mataifa ya ukanda wa Afrika mashariki yakiwemo ya Uganda, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan kusini na Tanzania ulilenga kubadilishana uzoefu juu ya ulinzi na usalama kwa wandishi hao.
'Kumekuwa na uminywaji wa habari, vitisho kwa waandishi wa habari paamoja wengine kutekwa na kish kupoteza maisha hivyo mkutano huu ni kuwakumbusha namna ya kujilinda,'alifafanua.
Akiwasilisha mada ya ulinzi na usalama kwa wandishi wa habari, mwandishi nguli kwa ssa anayefanyia kazi zake Somalia Valerie Msoka alisema waandishi anapaswa kujikinga wenyewe na wasisubiri kukundwa na sheria.
Alisema njia moja wapo ni umakini katika uandishi wao wa habari, kufanya uchambuzi wenye takwimu pamoja na kujenga ushirikiano..
Kwa upande wake mtaalamu wa takwimu kutoka shirika la Nukta Afrika Nuzulack Dausen alisema bado kuna muamko mdogo kwa waandishi wa wa habari kujikita katika uandishi wa habari za takwimu.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo waliziomba mamlaka husika kutotungwa kwa sheria ambazo zinazokinzana na uhuru wa maoni na kujieleza kwa waandishi wa habari.
Mwisho
Comments
Post a Comment