Skip to main content

UCHUMI WA BULUU YAJA NA MRADI WA AINA YAKE KWA UVUVI, UFUGAJI ENDELEVU WA MAZAO YA BAHARINI


 NA FATMA HAMAD,PEMBA @@@@

SEKTA ya uvuvi, ufugaji wa samaki na kilimo  cha mwani iznaendelea kuwa nguzo muhimu ya ajira na kipato kwa wananchi wa Zanzibar huku Serikali  na taasisi binafsi ikiweka mkazo katika matumizi ya rasilimali za baharini kama fursa ya biashara na uwekezaji. 

Hayo yalisemwa na  jana Septemba 1, 2026 na Ofisa Mdhamini wizara ya Uchumi wa Bulu DK Salim Mohamed Hamza wa kati akizungumza katika mkutano wa wadau wa Mradi wa Kuimarisha Usimamizi Endelevu wa Uvuvi na Ufugaji wa Mazao ya Baharini Tanzania, TASFAM,  huko katika ukumbi wa ZRA Gombani Chakechake Kusini Pemba. 

Alisemesema ushirikiano wa wadau ni muhimu katika kuongeza uzalishaji, ajira na kipato kwa wananchi. 

ALisema kwa Sasa serikali imeelekeza zaidi katika sekta ya Bahari, hivyo imeamua kuleta Mardi huo wa kuimarisha usimamizi endelevu wa uvuvi na ufugajibwa mazao baharini, ili wadau muunge mkono Mardi huo na lile lengo la serikali liweze kutimia la kujipatia kipato kupitia Bahari.  



"Nyinyi wadau mnamchango mnaoshughulika na masuala ya Bahari mnamchango makubwa, hivyo tumeamua kuwaita muweze kufanya kazi na sisi, ili Mardi muweze kufanikiwa na Kupatikana kwa maedeleo yanayohitajika,"alisema.  

Alisema lengo hasa la mkutano huo ni  kuutanbulisha Mardi huo, muweze kufahamika na kuiona Kila mdau anaelekeza nguvu zake, ili kuweza Kupatikana kwa matunda ambayo yataifadisha jamii na serikali kiujumla. 

Kwa upande wake Mratibu wa Mardi wa TASFAM, Mohammed Said Khamis, alisema  mradi huo utatowa fursa mbalimba zinazotokana na rasilimali za baharini ambazo  zitawanufaisha  wananchi ili kufikia maendeleo endelevu.  

"Niseme kwanba Mardi huu utakuza zaidi uchumi wa wananchi wanaoishi katika maeneo ya ukanda wa pembezoni mwa Bahari,"alieleza.  



Aidha alifahamisha kwamba Mardi huo pia utasaidia uimarishwaji wa kukabiliana na kupambana na masuala ya mabadilikotabia nchi, jambo ambalo kimekua liikiathiri jamii.  

 Akiwasilisha mada katika mkutano huo afisa tathmini kutoka mradi huo Daudi Haji Pandu   alisema TASFAM inalenga kuwasaidia wananchi kutumia rasilimali za baharini kama chanzo cha ajira, biashara na uwekezaji husasan kwa wakaazi wa maendeleo wa ukanda wa bahari. 

Kaimu Mkurugenzi wa Mardi huo Mussa Ramadhan Said alisema, Mardi huo utahakikisha unamnufaisha Kila mtu awe kijana, mzee,mwanamke ama mwanamke. 

"Kwakweli Mardi wetu huu utakuza ni chachu ya mabadiliko kwa watu wote, utahakikisha haumuachi mtu nyuma,'alieleza. Baad 

hi ya wadau walioshiriki mkutano huo walisema ni vyema jamii iendelee kupewa elimu zaidi juu ya dhana ya Uchumi wa buluu iweze kufahamu, na kuweza kuchangamkia fursa zitokanazo na sekta hiyo. 


Sambamba na hilo walisema ni vyema kuzingatia sera ya Jinsia katika utekelezaji wa Mardi huo, ili Kila mwananchi anufaike na fursa hiyo. 

Mradi huo ambayo  unatekelezwa na  Wizara ya Uchumi wa buluu Zanzibar, wizara yaMifugo na Uvuvi MLF Tanzania, na Dee Sea Fishing, Authority  DSFA Tanzani. 



Ambapo atatekeleswa kuanzia 2025 hadi 2030 kwa ufadhili wa benk ya dunia.

naolenga kuongeza uzalishaji wa thamani ya mazao ya baharini pamoja na kuimarisha upatikanaji wa masoko na uhifadhi wa rasilimali hizokwa manufaa wa kizazi cha sasa na kijacho.

 …MWISHO..


Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...