Skip to main content

SITI FAKI ALI WA WETE: Ndie Mwalimu Mkuu alieondosha ‘sifuri’ skuli ya Utaani

 

                


               

‘Aweka mikakati wanabaki daraja la kwanza na la pili tu.

IMEANDIKWA NA ZUHURA JUMA, PEMBA

"Nilipoteuliwa kuwa Mwalimu Mkuu, mwanzo nilipata hofu hasa pale nilipojiona, naenda kuongoza watu wenye kiwango cha elimu sawa na mimi,’’anasema. 

 

Ni maneno ya Mwalimu Mkuu skuli ya Sekondari ya Wanawake Utaani Wete, Siti Faki Ali mkaazi wa Chasasa Wete.

 

Mwalimu huyo ambae alitokea skuli ya Chasasa akiwa Msaidizi Mwalimu Mkuu, alipata hofu mara ya kupokea barua ya kwenda kuiongoza skuli hiyo.

 

Anasema, kwa vile ameshakaa uongozi katika mambo mbalimbali ya kijamii na Serikali kwenye nafasi ndogo ndogo, ndipo alipoona kwamba na nafasi hiyo anaweza kuiongoza.

 

Mara baada ya kukabidhiwa madaraka, alianza kuweka mikakati, ikiwemo kuondosha zero kwa wanafunzi kuanzia kidato cha pili hadi cha sita.

 

"Nilipofika nilianza kuangalia kitu gani nifanye, ili kuifanya skuli hii, iwe nzuri na ya mfano wa kuigwa, nikaamua kwanza niwaandae walimu wangu vizuri, ili wapate nguvu ya kufundisha,’’anabainisha.

 

Anasema, hilo limeanza kufanikiwa, maana mwaka jana, kidato cha nne na mwaka huu cha sita hakuna mwanafunzi alietoka na zero, hali ambayo haijawahi kutokea kwa kidato cha nne.

 

Atajipanga zaidi kuimarisha mipango yake na mikakati, kuhakikisha wanafunzi wa skuli ya Utaani, wanakuja na daraja la kwanza na la pili tu.

 

Matokeo ya Kidato cha nne

 

Mwaka 2023 wanafunzi waliofanya mitihani ni 159, ambapo daraja la kwanza walikuwa 15, daraja la pili 20, daraja la tatu 26, daraja la nne 91 na zero saba (7).

 

Mwaka 2024, wanafunzi wote ni 87, ambapo daraja la kwanza ni 11, daraja la pili 12, daraja la tatu 24, daraja la nne 39 na zero moja (1).

 

Huku mwaka 2025, wanafunzi waliofanya mitihani ni 113, ambapo daraja la kwanza 29, daraja la pili 44, daraja la tatu 27, daraja la nne 12 na hakukuwa na zero.

 

Matokeo ya kidato cha sita

 

Mwaka 2023, wanafunzi waliofanya mitihani ni 31, ambapo daraja la pili ni sita (3), daraja la tatu 20, daraja la nne watatu (3) na zero mbili (2), huku mwaka 2024, wanafuzi wote ni 21, daraja la kwanza moja (1), daraja la pili 13 na daraja la tatu, ni saba (7).

 

Mwaka 2025 wanafuzi waliofanya mitihani ni 35, daraja la kwanza nne (4), la pili 14, na daraja la tatu 17, ambapo mwaka 2026, wanafunzi wote ni 49, daraja la kwanza wakiwa watano (5), la pili 21 na daraja la tatu 23.

 

Mwalimu huyo anasema, mwaka huu 2026 wanaotarajiwa kufanya mitihani ni wanafunzi 35 wa kidato cha nne, na mwaka 2027 watafanya mitihani wanafuzi 64 wa kidato cha sita.

  

Katika mikakati yake ya kuifanya skuli hiyo inakuwa bora kwa Tanzania nzima, kwanza amekuwa akitafuta njia ya kutatua matatizo kwa walimu wake.

 

"Nilipofika katika skuli hiyo nilikuta kuna mpasuko kidogo, hivyo nilirekebisha kwa kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi, ikiwemo kupatiwa maslahi bora," anasema.

 

Hilo limewapa nguvu walimu na hamasa ya kuwafundisha wanafunzi kwa juhudi zote, jambo ambalo anajivunia hadi sasa.

 

Mwalimu huyo anafanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji, kwani anawashirikisha walimu wake kwa kila jambo, linalofanyika na hatua inayofikiwa.

 

"Viongozi wengi wanaokuja hapa kututembelea, wanasifu maendeleo yaliyofikiwa katika skuli yetu, kwa kweli tunajivunia," anasema.

 

Anaeleza, walimu wake wanapohitaji vifaa vya kufundishia, huwapatia vilivyopo na ikiwa hakuna, basi hufanya juhudi mbalimbali, kuhakikisha vinapatikana.

 

Mikakati mingine ameanzisha masomo ya ziada, kuhakikisha wanapata muda mzuri wa kujisomea, na kuwatafutia walimu wa masomo, ambayo hayana mwalimu wa kutosha.

 

"Masomo haya ya ziada ni kwa ushirikiano wetu pamoja na wazazi wa wanafunzi, hivyo kwa sasa hata walimu wanaosomesha masomo ya ziada, nimefanya utaratibu wa kuwaongezea malipo, kwa hiyo wamepata moyo,’’anasema.

 

Anasema, huwafanyia wanafunzi majaribio ya kila wiki, kila mwezi, kufanya ushindani baina ya skuli yake na nyingine, ili kuona wanafunzi wanasoma kwa bidii.

 

"Tunatofautiana kwenye ufahamu, kwa kuliona hilo, wale wanafunzi wenye ufahamu mzito, tunawatafutia wenzao kuwasaidia zaidi, na vilevile walimu hutenga muda maalumu kuwaelewesha,’’ anasimulia.

 


Katika mipango mengine ya kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora, Serikali imewawekea Programu za kusomeshea walimu, ikiwemo ya 'Smart body TV' ambayo mwalimu anatoka chuo kikuu cha Shangai nchini China.

 

Program hiyo, inafundisha walimu wa somo la hisabati wa skuli hiyo, pamoja na kushirikiana na walimu wa skuli za Chasasa, CCK, Fidel Castro na Madungu, ili kusudi wanafunzi wao wawe bora.

 

Ipo Programu ya "But Camp' ya sayansi, ambayo wanafunzi wake, walikwenda kusoma Pujini na kupata zawadi kwa jinsi walivyofaulu vizuri.

 

Mwalimu huyo Mkuu, anasema kwa upande wa masomo ya Sanaa 'Art' pia wanafaidika na programu hizo na wanafunzi, wanafaulu vizuri katika masomo yao.

 

Mambo hayo wanayoyafanya wanashirikiana na Kamati ya skuli, huku jamii ikifurahia mfumo wake wa kutatua kesi za wanafunzi bila upendeleo.

 

Skuli ya Sekondari Utaani ina wanafunzi wanawake 712 ambao ni michepuo, na ni kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita.

 

Anasema, uongozi kwa wanawake ni changamoto kwa sababu wanaonekana ni wadhaifu, pia wanaume hawataki wala hawapendi kuongozwa na wanawake.

 

Mwalimu huyo alianza kazi yake ya ualimu katika skuli ya msingi Kizimbani Wete, na baada ya kupata elimu ya cheti na diploma, alihamishiwa skuli ya Sekondari Utaani, akiwa mwalimu wa kawaida.

 

Mwaka 2013, alipelekwa skuli ya Sekondari Chasasa, na ilipofika mwaka 2021 ndipo alipoteuliwa kuwa Msaidizi Mwalimu Mkuu skuli hiyo.

 

Mwaka 2025, aliteuliwa kuwa Mwalimu Mkuu skuli ya Sekondari ya Wanawake Utaani, nafasi ambayo anaitumikia hadi sasa.

 

Alisoma elimu yake ya msingi katika skuli ya msingi Jadida Wete, na Sekondari alisoma Wingwi katika skuli ya Sekondari ya ‘Dodeani Technical’ ambayo ilianzishwa na Jumuiya ya Wazazi.

 

Kidato cha tano na cha sita, alisoma skuli ya Sekondari Lumumba Unguja, na kwa sasa ana elimu ya chuo kikuu ngazi ya digirii ya pili (Masters) katika fani ya lugha ya Kiswahili.

 

Mwalimu huyo, nje ya saa za kazi ni Msaidizi wa Sheria Wilaya ya Wete, akiwa mshika fedha wa jumuiya yao.

 

WALIMU WENZAKE

 

Mwalimu Fatma Kombo Mbarouk anasema, mwalimu huyo ni mfuatiliaji na mpambanaji, katika shughuli zake za kitaaluma, na anawashirikisha kikamilifu.

 

Wanajivunia kuwepo kwake, kwa sababu ufaulu umenyanyuka, kwani kulikuwa na wanafunzi ambao wameshakosa muelekeo, hivyo baada ya kufika yeye kwa hekima na busara, alichangia ufaulu.

 

“Yupo vizuri kusimamia kila kwenye kasoro kurekebisha, unapofanya kosa anakuelekeza, anaondoa migogoro, itayotendeka baina yetu,’’anaeleza.

 

Mwalimu Sharif Juma Fakih, anakiri kuwa, Mwalimu huyo ana sifa ya kupokea fikra, zinazotoka kwao, huzipima na kuzifanyia kazi kwa uweledi.

 

“Ana ile hamasa ya kutaka kuleta ufaulu mzuri katika skuli yetu, anafuatilia na kusimamia mahitaji ya walimu, na namna gani skuli itafanya vizuri zaidi, jambo ambalo, ndio ndoto yetu walimu,”

anasema.

 

Menyekiti wa Kamati ya skuli hiyo Maulid Abdi Aweis anasema, mwalimu huyo yupo vizuri katika utendaji wa kazi na anawashirikisha walimu wenzake pamoja na kamati yao kwa kila jambo.

 

Anasema, anaweza kuongoza vizuri kwa sababu ana elimu ya uongozi na sheria, hivyo ameleta mabadiliko kwenye ufaulu pamoja na walimu kushirikiana nao.

 

“Anafanya maamuzi ya pamoja, na nikiwauliza walimu wanasema hawajapata changamoto yeyote, hivyo namuomba azidishe ushirikiano ili kusiwe na makundi yatakayosababisha kushusha ufaulu wa wanafunzi wao,” anasema.

 

Mwanafunzi Hafsa Mkubwa Salum anasema, mwalimu huyo ana hekima na upendo kwa wanafunzi wake, kwani ana tabia ya kuwatafutia walimu, na kuwaweka karibu na kuwasaidia sana wanafunzi ambao wana uwelewa mzito.

 

Mzazi wa mwanafunzi anaesoma skuli hiyo mkaazi wa Ole, Fatma Ali anasema, mwalimu huyo ana juhudi sana na alifanya mabadiliko wa watoto wao kwa sababu walisoma kwa bidii zaidi.

 

“Ukimpelekea changamoto anaitatua kwa haraka, ana moyo wa kujitolea, na nimeshukuru mtoto wangu alipata daraja la pili kidato cha nne mwaka jana,” anasema.

 

 

WIZARA YA ELIMU

 

Ofisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Mohamed Nassor Salim anasema, utendaji wa Mwalimu huyo, ni mzuri na anaongoza skuli ya wanawake kwa ufanisi na utulivu.

 

Anasema wizara, ilimchagua kusimamia skuli hiyo, baada kuona anakidhi vigezo vyote vya uongozi, ikiwemo elimu, kuwa na maadili mema, kujiamini.

 

Kumbe kilichowasukuma kumpa dhamana hiyo, ni kutokana na ubunifu alionao, ushirikiano na wadau wao wakiwemo wazazi, kamati za skuli na jamii kwa ujumla.

 

Mdhamini anamshauri Mwalimu huyo, kuwa kuendeleza uzalendo wa kweli, aendelee kuwa na nidhamu ya hali ya juu, pamoja na kujiendeleza kielimu.

 

ASASI ZA KIRAIA

 

Mratibu wa Programu ya mradi wa ‘SWIL’ kutoka TAMWA- Zanzibar Sabrina Ali Mwatanga anasema, wanaendelea kuelimisha na kuhamasisha uongozi kwa wanawake, ili waingie kwa wingi katika vyombo vya maamuzi.

 

“Naamini kwamba, mwalimu huyu ataendelea kuwasimamia vizuri wanafunzi hao, ili wafaulu vizuri, na kwa vile ni wanawake atakuwa amewasaidia, kwani miongoni mwa changamoto zinazowakumba wanawake kuingia kwenye uongozi,’’anasema.

 

Mkurugenzi wa Jumuiya ya Utetezi wa Mazingira na Jinsia Pemba ‘PEGAO’ Hafidh Abdi Said, anasema juhudi za Mwalimu Mkuu huyo, zinaleta matumaini bora kwa watoto wa kike, kujiendeleza kielimu.

 

“Lengo letu ni kufikia 50 kwa 50, hivyo naamini mikakati aliyoiweka Mwalimu huyo, kwenye skuli yake, itasaidia kutoa viongozi bora wa baadae, ambao wataleta maendeleo katika nchi yetu,” anaeleza.

 

Kifungu cha 21 (2) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kimeeleza kwamba, kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki, kikamilifu katika kufikia uamuzi, juu ya mambo yanayomuhusu mwanamke na taifa lake.

Serikali mbalimbali duniani, zimeridhia mikataba na matamko mbalimbali ya usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kwenye uongozi na nafasi za kisiasa, tangu mwaka 1948 ziliporidhia tamko la haki za binadamu.

Matamko na mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda, yanaainisha haki za kiraia na kisiasa kwa wote bila kujali jinsia, rangi au dini.

Huku Azimio la kimataifa, juu ya haki za binadamu la mwaka 1948 ambalo ndio msingi wa haki za binadamu, ikiwemo za kiraia na kisiasa, linatoa haki kwa kila mtu katika uongozi.

Skuli ya sekondari Utaani Wete imeanzishwa mwaka 1954 kabla ya Mapinduzi, ambapo ilipofika mwaka 2014, Rais Mstaafu wa Zazibar Dk. Ali Mohamed Shein aliitangaza rasmi kwamba skuli hiyo ni ya wasichana tu. 

                               MWISHO.

 

 

 

 

 

 

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...