Skip to main content

UJENZI BANDARI YA MICHEWENI NI JUHUDI ZA DK. MWINYI KUIFUNGUA PEMBA KIUCHUMI

 


NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi, amedhamiria kwa vitendo kuleta maendeleo ya kiuchumi kisiwani Pemba.

Na ndio maana, anachukua juhudi mbalimbali kuhakikisha wananchi wa Pemba, wanakuwa na maisha bora kiuchumi, kwa kuendelea kuwapelekea miradi ya kimaendeleo ya kimkakati.

Lengo ni kuona kwamba, kila mwananchi anajiajiri na kuajiriwa kupitia fusra za kiuchumi, ambazo zinaendelea kuletwa na Dk. Mwinyi katika kila sekta.

Hayo ni ya kujivunia katika kisiwa hiki, kwani kinaenda kufunguka na kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi wake.

Moja ya miradi mikubwa ambayo itakuza uchumi wa wananchi kisiwani Pemba, ni ujenzi wa bandari za kitaifa ambazo zitawaingizia kipato wananchi, kwa namna moja ama nyingine na kupata maendeleo.

Katika ahadi zake Dk. Mwinyi alizoziweka kwa wananchi kwa ajili ya kukuza kipato chao, ni ujenzi wa Bandari ya Shumba Mjini, iliyoko wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba.

Bandari hiyo ni kiungo muhimu kati ya wananchi na wafanyabiara wa Pemba, pamoja na wale wa Mombasa nchini Kenya, hivyo uchumi utaimarika kwa wananchi na serikali kwa ujumla.



Dk. Mwinyi anasema, moja kati ya vitegauchumi kisiwani Pemba, ni kujenga bandari za kisasa, kama inayojengwa Shumba Mjini, ambayo ni miongoni mwa tegemeo kubwa la kukuza uchumi.

Rais huyo, aliahidi kuendelea kuimarisha miundombinu ya bandari ya Shumba, ili kupunguza gharama za maisha na bei za vyakula, ambazo zimekuwa zikiwakabili wananchi.

Serikali ya awamu ya nane, imeimarisha bandari hiyo ambayo itakuwa ni bandari kuu kwa koa wa askazini Pemba, kwani meli kubwa za nje zitafunga gati moja kwa moja.

Bandari ya Shumba Mjini, itaongeza ufanisi wa upokeaji wa mizigo na bidhaa kutoka Tanzania Bara na nje ya nchi, ikiwemo Mombasa Kenya, jambo litakalosaidia kwa kiasi kikubwa, kupunguza gharama za chakula kisiwani humo.

Anasema, pia bandari hiyo ni hatua muhimu ya kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa muhimu, hatua ambayo itapelekea kushuka kwa bei za vyakula na bidhaa nyingine.

“Tunatambua changamoto kubwa ya gharama za usafirishaji wa bidhaa kutoka Unguja kuja Pemba, ambayo inachangia kupanda kwa bei za vyakula, na bidhaa, hivyo kupitia bandari ya Shumba itakuwa mwarubaini wa hilo,’’anasema.

Yeye ametekeleza kwa vitendo, yale aliyowaahidi wananchi, wa kuifungua Pemba kiuchumi, kwa sababu bandari ya Shumba, itakuwa kubwa ambayo meli za mizigo zitaegesha hapo.

Eneo jingine ni kwamba, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla hivi karibuni alipoitembelea bandari hiyo, alisema utakapokamilika mradi huo, utafungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Micheweni.



Akasema bandari hiyo, ina umuhimu mkubwa wa kiuchumi, hivyo itajenga ustawi bora wa maisha ya wananchi na kuingiza pato kwa serikali.

Maana bandari hiyo itafungua uchumi wa wananchi kisiwani hapa, kwa kuzalisha ajira na kukuza biashara, jambo ambalo litaimarisha pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

“Bandari hii, itakuwa na viwango vya kimataifa, hivyo moja kwa moja itakuja kunyanyua uchumi wa wananchi wa maeneo haya ya Shumba Mjini, wilaya ya Micheweni na Pemba kwa ujumla,” alieleza.

Akafafanua kuwa, bandari hiyo itaongeza ajira kwa vijana wa bodaboda, kuimarika kiuchumi kwa wajasiriamali, wanaouza vyakula, na wavuvi  kwa kupata bei nzuri ya samaki.

“Wananchi wa maeneo haya watanufaika kwa namna moja ama nyengine, mara bandari hii itakapoanza kazi, hivyo ni hatua nzuri iliyochukuliwa na Dk. Mwinyi katika kuimarisha kipato cha wananchi,”anaeleza.

Makamu huyo aliuwagiza uongozi wa Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC), kuhakikisha miamala bandarini hapo, inafanyika kwa kutumia mifumo, ili kudhibiti upotevu wa mapato.

“Mapato ya serikali ni muhimu, kwa sababu ndio inayosaidia kujenga miradi mikubwa ya kimaendeleo kama huu, na kuwanufaisha wananchi moja kwa moja,” anaeleza.

Katika kuhkikisha wananchi wananufaika zaidi, ajira ambazo hazihitaji utaalamu, wapatiwe wananchi wa Shumba Mjini, ili kuimarisha kipato chao.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar Badria Atai Massoud anasema, bandari hiyo itaiwezesha Zanzibar, kuwa kitovu cha biashara kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Jingine akasema, itakapomalizika, itachangia kuimarika kwa utalii, kukuza uhusiano mwema na mataifa jirani.

“Kwa kweli Dk. Mwinyi ana maono ya mbali na ndio maana, akajenga bandari hii, ili kuekeza na dhamira yake ya kuleta maendeleo Pemba, inakwenda kutimia si muda mrefu,”anasema.

Naibu huyo, anawashukuru wananchi wa Shumba Mjini, kwa kukubali kupisha ujenzi wa bandari hiyo, na kwa ushirikiano mkubwa, wanaoendelea kuutoa katika kipindi chote cha ujenzi.



Mshauri Elekezi kutoka Kampuni ya Anova Consulting LTD, Mhandisi Serafina Michael anasema, bandari hiyo inatarajiwa kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo, na itahudumia takribani abiria 1,500 kwa wakati mmoja.

Maana kwa awamu ya kwanza ujenzi wa bandari hiyo, utajumuisha jengo la abiria, gati, diko kwa ajili ya wavuvi, msikiti, ambapo hadi kukamilika kwake litagharimu shilingi bilioni 11.6.

WANANCHI

Hussein Rashid Hussein, anaishukuru serikali ya Zanzibar, kwa kuendelea kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo, ambayo inakwenda kustawisha maisha yao na kuwakwamua na umasikini.

“Tumeona maendeleo makubwa yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na Dk. Mwinyi, hivyo tunajivunia, kwani badari hii itaongeza ajira kwa vijana wetu,” anaeleza.



Mwananchi Shaame Ali anasema, kuwepo kwa bandari hiyo, kutawasaidia kupata usafiri wa uhakika na usalama, hivyo watajiamini katika safari zao.

“Kwa sasa hatotumia tena bandari bubu kama ilivyokuwa zamani, kwa sababu bandari itakuwa nay a uhakika na usalama kwetu,’’anasema.

Asha Shoka mkaazi wa Micheweni anasema, bandari hiyo pia itawanufaisha wafanyabiashara, kwani mizigo yao, itakuwa salama na itakuja moja kwa moja kwenye bandari hiyo.

“Bei zikiwa nafuu, biashara itauzika haraka na kwenda kuchukua mzigo mwingine, hivyo kipato chetu kitaongezeka kwa muda mfupi, na maendeleo yatapatikana,” anasema.

Mwananchi Bijuma Haji anasema, kupitia bandari hiyo, serikali itapata mapato ambayo yatawasaidia kujengewa miradi mikubwa na kimkakati, ambayo inawanufaisha moja kwa moja.

Bandari ya Shumba Mjini iliyopo wilaya ya Micheweni, ni miaongoni mwa vipaombele vya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, kupitia bajeti yake mwaka wa fedha 2025/2026.

Bajeti hiyo iliyoeleza kuwa, itaimarisha miundombinu ya bandari, ikiwemo kuanza kwa ujenzi wa bandari hiyo.

Hayo yalifahamaika, kwenye hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2026/2027 kwa bandari ya Mangapwani, Ujenzi wa bandari ya abiria na mizigo Maruhubi, ujenzi wa bandari ya shumba Mjini, uimarishaji wa bandari ya Mkoani na ujenzi wa bandari kavu Maruhubi.

                 MWISHO.

Comments

BLOG'S VISITORS

DAKTARI MWENGINE CHAKE CHAKE KULA SIKUKUU POLISI, NI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MGONJWA WAKE

NA WAANDISHI WETU, PEMBA::: DAKTARI anaetoa huduma kwa wagonjwa kituo cha afya cha serikali cha  Gombani wilaya ya Chake Chake Pemba, Is-haka Rashid Hadid, anaendelea kushikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa kaskazini Pemba, akituhumiwa kumtorosha na kisha kumbaka mtoto wa mwenye umri wa miaka 16, mkaazi wa Gombani. Daktari huyo miaka 35 ni mkaazi wa Kangagani Wilaya ya Wete mkoani humo, ambapo anadaiwa alimchukua mtoto huyo kutoka kwa rafiki yake, na kumpeleka kwenye nyumba anayoishi eneo la Kangagani. Mtoto aliefanyiwa kitendo hicho alisema kuwa, April 21 mwaka huu alikwenda kituo cha afya Gombani, kwa ajili ya matibabu na baada ya kupatiwa huduma na daktari huyo, alimuomba nambari yake ya simu. Alisema ilipofika usiku, walikuwa wanawasiliana kupitia ujumbe mfupi (sms) kwa lengo la kwenda kuchukua dawa nyingine ambazo kwa mchana huo alizikosa hospitalini hapo. "Nilikwenda hospitali kutibiwa, baada ya kufanya mapele katika sehemu zangu za siri, lakini akaniambia mpaka aje da...

Vikausha damu vya mjamzito hivi hapa, umo mchele, udongo, mkaa, chaki Uwezekano wa kuzaliwa watoto wenye udumavu, utapiamlo ni mkubwa

  NA ZUHURA JUMA, PEMBA@@@@ ‘’KILA ninapobeba mimba nimezoea kula mchele kwa wingi naweza kusamehe pilau au biriani,’’ ndio maneno ya mwanzao ya Bahati Mohamed Ali (sio jina lake halisi). Nilimfuma akiwa barazani kwake, mjini Ole wilaya ya Chake chake, pembeni yake akiwa na kibakuli cha mwazi, kwa umbali utaona amejaza chakula aina ya pepe, kumbe ni mchele wa Mbeya. Hujichotea kidogo kidogo na kuushindilia mdomoni mwake, huku akiendela kupiga storia na wenzake, bila ya kujali kuwa ujauzito alionayo na mchele huo hauna mwisho mwema. Kawaida yake akiwa mjamzito, kila anapoamka asubuhi anaroweka mchele upatao robo kilo hivi…na baada ya kumaliza kupika, yeye huchukua mchele wake kutafuna (kula). Wakati mwenza wake na watoto wao, wanakula chakula cha mchana, Bahati yeye hukaa pembeni na kibakuli chake cha mchele akiendelea kubahatisha afya yake. ‘’Mimba nyengine hupenda sana kutafuna mchele wa Mbea na nyengine hupenda mchele wa mapembe, kwa kweli huwa nina hamu (kileo), kwan...

HII KALI MBUNGE ASIYA AMKOGESHA MWANANCHI HADHARANI KISA HICHI HAPA......

  NA HAJI NASSOR, PEMBA MBUNGE wa viti maalum nafasi za wanawake mkoa wa kaskazini Pemba Asiya Sharif Omar, amewataka wananchi wa kijiji cha taifu, shehia ya Kinyasini jimbo la Gando wilaya ya Wete Pemba, kuyalinda miundombinu ya maji safi na salama, ili yawe endelevu kwao. Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kuwasili kijijini humo, na kumkogesha mwananchi mmoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji safi na salama, ulioasisiwa na mbunge wa Jimbo la Gando. Alisema, hawana mbadala kwa sasa bali ni kuilinda miundombinu ya huduma hiyo, hasa baada ya mbunge wa wao Salim Mussa Omar, kuwarejeshea huduma hiyo. Alieleza kuwa, inafahamika kuwa kwa miaka 14 waliikosa huduma hiyo hasa kwa vile viongozi waliokuwepo hawakujali kuwatatulia tatizo hilo, hadi juzi ilipofanywa na mbunge wao. “Baada ya huduma hii sasa kurejeshwa na mbunge wa jimbo la Gando, kazi iliyobakia kwenu wananchi ni kila mmoja kuwa mlinzi wa miundombinu hii,’...

'MKAPA' NA WENZAKE PEMBA WALAZWA RUMANDE

  NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@ MAHKAMA kuu Zanzibar kisiwani Pemba, chini ya Jaji Ibrahim Mzee Ibrahim, imewapeleka rumande watumuhimwa wanne wanaokabiliwa na tuhuma za kuua kwa makusudi, akiwemo Ali Mussa Omar ‘ Mkapa’ mkaazi wa Wawi wilaya ya Chake chake Pemba. Watuhumiwa wengine walioanza maisha mapya ya rumande ni mtuhumiwa Yassir Mohamed Juma miaka 23, Anuwari Mussa Omar miaka 30 pamoja na mtuhumiwa Yassir Mussa Omar ‘ Makababu ’ miaka 29, wote wakaazi wa shehia ya Wawi, wilaya ya Chake chake Pemba. Awali watuhumiwa hao waliwasili mahakamani hapo, kwa mara ya kwanza, kwa ajili ya kusomewa tuhma zinazowakabili za kumuua kwa maksudi Said Seif Kombo. Ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashtaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashataka Seif Mohamed Khamis akiambatana na mwenzake Mussa Khamis Ali kuwa, watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaia kufanya mauwaji hayo kwa maksudi. Ilidai kuwa, watuhumiwa wote kwa pamoja, walitenda kosa hilo Oktoba 16, mwaka huu, baina ya saa 7:00 m...

TUHMA ZA DAKTARI PEMBA KUCHIWA HURU: POLISI KASKAZINI KUTOA TAARIFA RASMI LEO

  NA HAJI NASSOR, PEMBA KAMANDA wa Polisi mkoa wa kaskazini Pemba, Juma Saad Khamis, amesema leo Mei 9, mwaka huu atatoa taarifa rasmi, juu ya kuendelea kumshikilia au kumpa dhamana ya Polisi, daktari wa Kituo cha Afya Gombani Is-haka Rashid Hadid, anayetuhumiwa kwa ubakaji. Alisema, kwa vile alikuwa katika mapumziko mafupi, haelewi jambo lolote linaloendelea kwa mtuhumiwa huyo, juu ya kuendelea kushikiliwa kwake kituoni hapo. Alieleza kuwa, leo Mei 6 (jana), hajapata taarifa za ndani za mtuhumiwa, huyo na kuwataka wananchi na wanaharakati, wasubirie hadi Jumatatu ijayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti Kamanda huyo, alisema hana taarifa zozote za kupewa dhamana mtuhumiwa ndani ya kituo chake cha Polisi au kuendelea kuwepo. ‘’Ilikuwa mimi sipo kazini kwa muda, kuanzia anakamatwa hadi anafikishwa Polisi, kwa sasa siwezi kueleza jambo lolote kwa mtuhumiwa huyo, hadi Jumatatu,’’alieleza. Aidha Kamanda huyo alieleza kuwa, kwa sasa hawezi kutoa uf...