NA HAJI NASSOR, PEMBA@@@@
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi Julai, 9, 2024, kwa
nyakati tofauti, wadau hao walisema bado wanawake ushiriki wao ni mdogo,
katika michezo ya aina mbali mbali, hasa soka ambapo jitihada zinahitajika kuhakikisha nao
wanashiriki.
Muhisin Omar Haji, Wawi Chake chake, alisema watoto wa kike
huishia maskulini kushiriki michezo na wanapomaliza hawajiendelezi na wala
hakuna mtu wala taasisi ya kuviendeleza vipaji hivyo.
Alisema wapo watoto wa kike wanakuwa wazuri kimichezo, kama
mpira wa miguu, kikapu, mpira wa Pete na mengine, lakini cha kuumiza ni
kuwa baada ya kumaliza skuli hawajiendelezi.
Asha Said Haji miaka 17, na Mwanaisha Haju Soud miaka 16
wote wakaazi wa Machomane, walisema kutokana na changamoto ya mavazi, kunasababisha
kudumaza kwa michezo kwa watoto wa kike kisiwani Pemba.
Walifahamisha kuwa, kama hakutozingatiwa mavazi ya stara kwa
watoto wa kike, kunaweza kukaendelea kuwa na mwitikio mdogo wa kushiriki watoto
wa kike kwa kutoruhusiwa na wazazi wao kushiriki michezo.
"Mimi nahisi kuwe na sheria ama kanuni, hasa sisi
watoto wa kike ya kuvaa vazi la heshima, wanapokuwa katika michezo, ili tuweze kufikia
ndoto zetu,"walifafanua.
Nae Salama Othman Haji wa Mtemani Wete, alisema, ili watoto
wa kike waweze kuwa sawa na wanaume kwenye soka, na hasa suala la kushiriki
michezo ni lazima Idara ya Michezo, itowe elimu, iwawezeshe kuingia michezoni.
Katibu wa shirikisho la mpira wa miguu Wilaya ya Chake chake
Jongo Juma Jongo, alisema kwa sasa ushiriki wa wanawake katika mchezo huo upo,
ingawa ni mdogo.
Alifahamisha kuwa, mwitikio mdogo wa watoto wenyewe, jamii
inavyochukulia mpira wa miguu ni uhuni kwa watoto wa kike inawafanya
wasiendelee mbele kwenye michezo.
Akigusia kwa upande wa mavazi, Jongo alisema isiwe kikwazo
kwa wanawake wani wanaruhusiwa kuvaa nguo za stara ikiwemo treki, vilemba na
kuwataka wazazi wawaruhusu watoto wa kike, kushiriki michezo ili waweze kutimiza
ndoto zao.
"Kuwazuwia watoto wa kike kutoshiriki michezo si haki kwa
sababu, dunia ya sasa imebadilika na kupiga hatuwa kwani, kuna nafasi za kusoma
nje ya nchi kupitia michezo na hatimaye kupata ajira",alisema.
Idara ya michezo na utamadini wizara ya elimu na
mafunzo ya elimu, ilisema wizara inayo mikakati mbali mbali ya kuhakikisha
wanawake wanakuwa sawa, katika ushiriki wa michezo.
Akiitaja mikakati hiyo ni pamoja na kuanzisha somo la sanaa
na ubunifu, michipuo wa michezo pamoja na kuanzisha elimu ya juu vyuoni.
Kaimu Mratib wa michezo wizara ya Habari, Utamadini na
Michezo Khamis Hamad Juma, alisema katika kuhakikisha vijana wa kike
wanashihiriki kikamilifu katika michezo inaweka miundo mbinu ya kujenga viwanja
vinne vitakavyozingatia mahitaji yote kisiwani Pemba
Alieleza kuwa, viwanja hivyo, ambavyo kila kimoja kitakuwa
na viwanja vya kuchezea michezo minne tofauti, ambapo ujenzi unaanza mwanzoni
mwa mwezi wa sita mwaka huu 2024.
Mwalimu kutoka skuli ya Sekondari Uweleni Khamis Mohamed
Ussi, alithibitisha kuwa wanafunzi wanaoshiriki katika michezo, ndio
wanavofanya vizuri katika masomo yao.
Hivyo aliwaomba wazazi, kuwaruhusu watoto wao kushiriki
katika michezo mbali mbali, ili waweze kupata fursa zinazotokea kupitia sekta
ya michezo.
Hakuna hata sheria moja, kati ya zile 17 zinazoongoza mpira
wa miguu, zinazomzuia mtoto wa kike, kushiriki mchezo, kwani kanuni ya kwanza
ni uwepo wa uwanja ya pili ni mpira, idadi ya wachezaji, vifaa vya michezo, mwamuzi
pamoja na shera ya 17 ya pigo la kona.
Mwisho
Comments
Post a Comment